Ni kitu gani hiki ??

SirLuke

Member
Joined
Dec 1, 2014
Posts
75
Reaction score
8
Jamani naomba mnisaidie wake. Mini Nawaamini Sana. Mimi natumia simu ya Tecno h6. Tatizo ni kwamba napodownload au kuweka pic au videos kwa njia yeyote Ile, baada ya Muda mfupi inakataa kufungua. Ikiniandikia hv CANNOT GENERATE THUMBNAIL na video inaandika CAN'T PLAY THIS VIDEO.
 

  • mbona simpo tu?CANNOT GENERATE THUMBNAI=haiwezi kutengeneza kucha ya kidole gumbaL​



 


Hiyo simu ina virus, scann kwa kutumia computer via Usb cable.
 
Hiyo simu ina virus, scann kwa kutumia computer via Usb cable.

Mollel jamaa kaweka sentensi hii sijui ni makusudi au la.
 
Kama alivyosema ymollel ni kuwa Simu yako imeongiwa virusi. Kirusi au computer Virus ni aina ya program zilizoandikwa kwa nia ovu - kufanya computer, simu au kifaa chako chenye au kinachotumia computer kisifanye kazi tarajiwa na Kukupa majibu yasiyotarajiwa au kuharibu kabisa kifaa chako!

Program hizi Za virusi huandikwa Kila siku lakini uzuri Pia ni kuwa kuna Watu na makampuni makubwa huandika program zinazoweza kung'amua hivyo virusi na kuvitoa kabisa. Program Hizo huitwa Antivirus. Hizi antivirus Pia zinatakiwa Kila Mara kupokea viimarisho (updates) hasa Kutoka ktk mtandao wa internet kwa ajili ya kutambua aina ya virusi vipya vinavyotumwa ktk mtandao wa internet Kila siku!

Kwa hiyo tafuta computer ambayo ina Antivirus ambayo ni hai (updated), Tumia USB Cable iliyokuja na Simu yako, chomeka ktk Simu na kisha chomeka Kwenye computer. Kwenye Simu yako ruhusu computer iitumie Simu yako kama "storage media". Tumia antivirus ya computer kuscan (na kutoa) virusi.

Ikimaliza kabla chomoa Simu yako lakini kabla hujafanya kitu nenda play store na tafuta antivirus yoyote (mfano avg antivirus) uinstall ktk Simu yako.

Fanya hivyo itakuwa imekusaidia kuondoa Hilo tatizo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu asante sana umenifanya nijue maneno mengi yaliyokuwa yananitatiza kiswahili chake,na pia jinsi ulivyofafanua hata ambaye hajawai kushika smartphone au komputer amekuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…