Huku kwetu wanavyopenda ngono mama watu wazima wanaanza kufundisha watoto vitu vya kipuuzi. Cha kushangaza zaidi anayetoa somo ameachika zaidi ya mara 3, unategema mtu kama huyo ataongea nini kumsaidia mwali.
Nfikiri tufikie hatua tukatae kufanyiwa kitchen party, tuishie kwenye mafundisho ya kanisani yanatosha. Hayo mengine tutayaona huko.
CAROLINE YOU HAVE A POINT HAPA!hasa hasa kwenye kila silabi ya haya maneno niliyoyaquote.
Nasikia sikia eti wazazi wengine pia wanapenda kitchen party kwa mabiti zao ili wapate vyombo.kwa sababu na wao wameshawachangia sana watoto wa wanawake wenzao,YA KWELI HAYA?
kama ni kweli basi hii sherehe haina ladha tena!inakuwa pia imekaa kimaslahi zaidi
Kweli mkuu haya mambo ya chumbani shangazi au yake bibi yake anatosha tu kumwambia kwa faragha mkuu!
Mkuubwa sasa ukifanya hivi zawadi watapataje? Siku hizi target sio yale yanayosemwa issue ni mtoto atapataje zawadi. Sasa ukisema ni shangazi na bibi mpwa watu watakosa hata mwiko.
Sasa kunta...kama dhima ya hii sherehe imebadilika,waonaje jina la sherehe likabadilika likaendana na dhima halisi ambayo ni 'zawadi' kwa mujibu wa post yako?
Tuiite nini?chagua hapa:
- GIFT PARTY
- KITCHEN UNTESILS PARTY
he, he Nafikiri Kitchen Untensils Party itakuwa imekaa vizuri zaidi
sasa na sisi akina baba wanatufunda akina nani na lini?
sasa na sisi akina baba wanatufunda akina nani na lini?