Ni 'Kitchen Party' au 'Bedroom Party'? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni 'Kitchen Party' au 'Bedroom Party'?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Teamo, Mar 16, 2009.

 1. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ..............Kwamba hizi shughuli maarufu kwa jina la 'SHEREHE YA JIKONI' zinazidi kuchukua sura mpya,na pengine KUPOTEZA MAANA,au mimi ndio sijui maana.Ndio maana nimeamua KUISTIPULATE ISHU HAPA!

  katikati ya 'shughuli' nimesikia jana kipengele kinaitwa MADA,nikiwa katika mojawapo ya maeneo yangu ya kujidai pande za kimara.Kwa namna walivyokuwa wakimshauri bibi harusiu mtarajiwa UKWELI HAIKUWA SHEREHE YA JIKONI ambayo pendine ufahamu wangu mdogo ulinidadavulia ki vile.Mama zetu walikuwa wakijadili mambo ya CHUMBANI tena kwa kina sana,na katika sehemu ya halaiki,tena muda ulikuwa bado kabisa.

  Sasa mimi nilikuwa nafikiri labda hizi sherehe zingetofautishwa siku kwa kuzingatia MAADILI,na umaana wenyewe.hii itasaidia 'wadau' wa sherehe hizo kuzitafutia muda muafaka,eneo stahili na pengine kukinusuru kizazi kinachofuata kusikiliza 'mambo ya chumbani' moja kwa moja kutoka kwenye vinywa vya wazazi wao.

  Au ninakosea wadau?
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Kweli mkuu haya mambo ya chumbani shangazi au yake bibi yake anatosha tu kumwambia kwa faragha mkuu!
   
 3. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mie nazichukia hizo kitchen party, nilikuwa naendaga coz ni za watu wangu wa karibu lakini ya mwisho niliyoenda na nilisema sitoenda tena kwenye hizo party, hao makungwi walikuwa wanamuambia mtarajiwa" mafiga matatu mtoto wa kike ndio yanayohitajika ndani" "vigaloni ni muhimu kwa binti kama wewe, ndoo ya maji ikimwagika then una kigaloni,kulikuwa hakuna la maana, ni matusi mtindo mmoja, kuanzia hapo nilisitisha kwenda kwenye kitu kinachoitwa kichen party! kwa upande wangu hazisaidii, ni wamama watu wazima kabisa wanayaongea hayo badala ya kumjenga binti niliona wanambomolea kabla hata hajaingia ndani, kama alivyosema hapo juu shangazi na bibi wanatosha.
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hizi sherehe ni wizi mtupu.....siku hizi zimepitiliza maadili ya Kitanzania.
  Yaani uswahili swahili mwiiingi mkeo anapaswa kufunzwa na shangazi au bibi full stop.
   
 5. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kizazi kimeuawa na wazazi tunaowategemea kama walinzi wetu. Kitchen party imeharibiwa maana na watu wachache wasiokwua na fikra. West africa kitchen party maana yake ni kumwandaa mwali kuyakabili maisha ya ndo katika nyanja zifuatazo. Kupika, analetwa mtalaam wa kupika anatoa somo, kufua, kufanya usafi, jinsi ya kuishi na watu, wakiwemo wakwe na familia kwa ujumla. Tena kitchen party hiyo siyo ya siku moja ni zaidi ya miezi 3

  Huku kwetu wanavyopenda ngono mama watu wazima wanaanza kufundisha watoto vitu vya kipuuzi. Cha kushangaza zaidi anayetoa somo ameachika zaidi ya mara 3, unategema mtu kama huyo ataongea nini kumsaidia mwali.

  Nfikiri tufikie hatua tukatae kufanyiwa kitchen party, tuishie kwenye mafundisho ya kanisani yanatosha. Hayo mengine tutayaona huko.
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  CAROLINE YOU HAVE A POINT HAPA!hasa hasa kwenye kila silabi ya haya maneno niliyoyaquote.

  Nasikia sikia eti wazazi wengine pia wanapenda kitchen party kwa mabiti zao ili wapate vyombo.kwa sababu na wao wameshawachangia sana watoto wa wanawake wenzao,YA KWELI HAYA?

  kama ni kweli basi hii sherehe haina ladha tena!inakuwa pia imekaa kimaslahi zaidi
   
 7. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  kuna ukweli ndani yake, nakumbuka moja niliyoenda mama wa binti ni mtu wa kuhudhuria sana kwenye shughuli za watu na yeye siku hiyo watu walijitokeza kweli, alipata makorokoro mengi sana kiasi cha kwamba mama na mtoto waligawana pasu pasu.....waswahili waliongea maneno hapo ndio nikakubali kumbe sasa nayo ni maslahi tu.
   
 8. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Nimeshahudhuria kitchen party tofauti kubwa zaidi ni kumfunda bibi harusi mtarajiwa atakapoingia maisha ya ndoa azingatie mambo yapi.

  Kuna kitchen party zingine hata kwenda na mama yako ni aibu,unafundishwa shughuli za kitandani ukumbini ambapo nadhani si mahali pake.

  Pia siku hizi watu hawatoi zawadi sana kwenye sherehe kama send-off/harusi baada ya kuchangia vya kutosha kama ilivyokuwa zamani zawadi za kumwaga, hivyo kitchen party zaidi ya hayo mafunzo pia ni kweli bibi harusi mtarajiwa aondoke na zawadi ambazo nyingi ni za jikoni na chumbani.

  Ila nimewahi kuhudhuria kitchen party kadhaa ambazo ni za kistaarabu sana,mfundaji anakuwa amekutana na bibi harusi mtarajiwa kabla ya kitchen party na kumpa mafunzo nyeti sana sana kuhusu mapenzi. Halafu siku yenyewe ya kitchen party ni mada za kawaida tu zinaongelewa kama heshima kwa wakwe na familia ya mume, usafi wa ndani na nje,uchumi na kujishughulisha kuingiza kipato ndani ya familia na mambo mazuri mengine ambayo ni ya kumsaidia kuhusu ndoa yake. Nia hasa pale ni kumkumbusha kwasababu lazima mashangazi na kina mama ndani ya familia wanakuwa wameshaongea na bibi harusi mtarajiwa.

  Kitchen party pia inategemea na aina ya familia na ndugu wa kike wa bi.harusi mtarajiwa mana wanaweza wataifanya kistaarabu ila kuna za kitchen party za kishangingi hapo utajua aina zote za mikao ya mapenzi na kukatika tu hamna zaidi wala mada nyingine yenye uzito!
  Pia kuna waolewaji watarajiwa wanaochagua kutokuwa na kitchen party!
   
 9. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Umasiki umekithiri, sasa wameanza mtindo mpya, kuchangisha hela nyingi eti 30,000 ili ukija uje tu wewe bila chombo wao watanunua. Unaishia kupewa khanga tena ya india hela nyingine wanatia ndani.

  Kitchen party haina maana yoyote kwa tanzania. Hivi wenzangu mmegundua wale waliofanyiwa kitchen party ndiyo wanaongoza ukihiyo na kuachika kabla ya miaka hata mitatu.

  Nakumbuka wakati naolewa 98, kitchen party zilikuwa hazijachukua sura kama sasa hivi, tuliishia kuongea na akina shangazi, na mama wadogo mpaka leto tunaduna kwa raha zetu. Kama unafanya kazi huwezi nunua hata brenda ya kutengeneza juice ya mumeo leo hii unataka michango ndiyo ikununulile tumestukia dili hatuji na hatuchangi tutaishia send off tu.
   
 10. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuubwa sasa ukifanya hivi zawadi watapataje? Siku hizi target sio yale yanayosemwa issue ni mtoto atapataje zawadi. Sasa ukisema ni shangazi na bibi mpwa watu watakosa hata mwiko.
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Sasa kunta...kama dhima ya hii sherehe imebadilika,waonaje jina la sherehe likabadilika likaendana na dhima halisi ambayo ni 'zawadi' kwa mujibu wa post yako?

  Tuiite nini?chagua hapa:
  • GIFT PARTY
  • KITCHEN UNTESILS PARTY
   
 12. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #12
  Mar 16, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ama kweli kumebadilika. Mie sijahudhuria kitchen party siku nyingi na ya mwisho ilikuwa ya kistaarab sana tofauti na picha ninayoipata hapa. Kama ni hivyo si ni bora wawe wanawaalika hao makungwi chumbani na mwali wamalizane nae then watuchangishe michango ili wanunue zawadi (vyombo) wazipendavyo?

  Nasikia siku hizi watarajiwa wanakabidhiwa mpaka vitanda katika kitchen party and then msasambuaji au kungwi anaonyesha kinavyotumiwa hadharani sijui mkuno wa nazi, sijui ah ....... aibu tupu.
   
 13. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  watu wanafuata mkumbo eti kwa vile fulani kafanyiwa na mimi nifanyiwe, anaweza akatafuta mama waheshima akakufundisha jinsi ya kuishi na mume na mambo mengine basi, siyo unafundishwa jinsi ya kuishi na mume na mashangingi ambayo hayajawahi kuolewa wala hayajui ndoa,ujinga mtupu au unafundishwa na mashoga wapi na wapi?
   
 14. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #14
  Mar 16, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  sasa na sisi akina baba wanatufunda akina nani na lini?
   
 15. Jaramba

  Jaramba Member

  #15
  Mar 16, 2009
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasemekana kuwa wengi wa hao makungwi wa hizo sherehe,hawako kwenye ndoa,hawajawahi kuolewa au wameachika,sasa najiuliza kama wao ni walimu wazuri kwa nini walishindwa kwenye ndoa zao?
   
 16. I

  Ikena JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2009
  Joined: Oct 24, 2007
  Messages: 482
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 60
  Hakuna la maana humo, ni ukahaba tu.
  Hapa kazini kuna kahaba wa waume za watu eti naye alifanyiwa kitchen part. Ivi kuna kitu gani alichokua hakijui??
   
 17. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #17
  Mar 16, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  he, he Nafikiri Kitchen Untesils Party itakuwa imekaa vizuri zaidi
   
  Last edited: Mar 17, 2009
 18. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #18
  Mar 16, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
 19. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,181
  Likes Received: 663
  Trophy Points: 280
  Kwa wanaume kuna BURGER PARTY mkuu, je hujawahi kusikia?
   
 20. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Nasikia mnakuwaga na bachelor's party kama sijakosea!
   
Loading...