Ni heri iwe hivi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,679
Ni heri Kuoa/Kuolewa na mwanamke/mwanaume aliyatoka familia ya kimaskini na mwenye fikira ,mawazo na moyo wa kitajiri kuliko kuoa/kuolewa na mwanamke/mwanaume aliyetoka familia ya kitajiri ,mwenye fikira,mawazo ya kimasikini.

Watu wengi tuna dini ila hatuna imani.Wanaume wengi tunatumia pesa nyingi kwenye kutizama mpira Bar na kutoa nusu konzi ya sadaka kwa Mwenyenzi Mungu Kanisani/Msikitini.

Mwanamke anayemkataza mumewe ya kuwa anafuja pesa bar kwenye mipira yeye anatumia Tsh 50,000/- saloon kila weekend na 50,000/- kwenye sale za kitchen party,kanisani/msikitini anatoa sadaka nusu konzi.

Mungu anatutendea mambo makubwa na mazito kama zawadi ya uzima na afya ila tunampa kidogo na kwa masikitiko.

Sasa mwaka 2019 tuanze kumuomba atupe hekima na busara sababu pesa ametupa lakini tumekosa hekima na busara.

Hakuna jambo jema kama kuwakwaza wanadamu na kumfurahisha Mwenyezi Mungu...It is very simple to happy ,but it is very difficult to be simple.

Sasa wewe jidai fundi wa kuwalizisha wanadamu huku unamkosea Mungu wako itajulikana siku ya kiama
 
Mkuu ushauri wako umetukuka sana.. lakini sisi tumeumbwa kusahau... na hicho ndicho tutakachokwenda kuteketea nacho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni heri kuolewa au kuoa na mtu unaempenda hayo mengine Mungu akipenda ila cha kwanza ni kumpenda
 
Pamoja sana mkuu
Ngobekezela NKOSI Ngobekezela
 
Shida nn mzazi

Ngobekezela NKOSI Ngobekezela
Haipeleki chaji yaani kwenye ICON ya chaji wameandika NOBATTERY IS DETECTED ina maana imekuwa kama desktop tu umeme ukikata na PC inazima au kwenye soketi nikizima na PC nayo inazima hadi niwashe kwenye skoketi au umeme urudi.
 
Umeshajaribu battery nyingine? Possible battery is damaged
Haipeleki chaji yaani kwenye ICON ya chaji wameandika NOBATTERY IS DETECTED ina maana imekuwa kama desktop tu umeme ukikata na PC inazima au kwenye soketi nikizima na PC nayo inazima hadi niwashe kwenye skoketi au umeme urudi.

Ngobekezela NKOSI Ngobekezela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…