illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
Nimekwenda kituo cha polisi kuripoti taarifa ya upotevu al maarufu kama loss report baada ya kufungua taarifa nikaenda kwa muhasibu kulipia kisha nikaelekezwa au niseme nikaamriwa niende nje kwenye stationary "nikachukue" karatasi za loss report tatu kufika pale nikaomba nipewe hizo karatasi yule muhudumu akaniambia gharama yake ni sh 300 nikamuuliza unauza? Akajibu hakuna kitu cha bure kwanza hili siyo duka la polisi nikamuuliza nani kakupa mamlaka ya kuuza nyaraka za polisi? Sikupata jibu.
Kwanza siyo sahihi kuuza hizo karatasi pili ni hatari kwa hawa raia kuwa na shehena ya nyaraka za polisi ambapo kama ikitokea kama raia ana nia ovu anaweza kujipatia hizo karatasi kufanyia uhalifu. Oysterbay polisi duka hili lipo mkono wa kushoto baada ya kuingia ukitokea barabara ya Ali Hassan Mwinyi cc Mwigulu Nchemba