Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 52,805
- 165,554
Kwa hiyo ni bora kikao kingefanyika Dodoma Rais akachukua ndege akajaza mafuta na kuruka hadi Dodoma! Tatizo ni kwamba wakati gani JK anakoma kuwa Rais na kubaki kuwa MWenyekiti wa CCM? Kutenganisha hapa inakuwa vigumu kweli. Rais analindwa na serikali kwa gharama za serikali na hakuna wakati ambapo watasema kuwa sasa Rais anafanya kazi za Chama hivyo alindwe na Chama! Hakuna wakati ambapo anauvua Uamiri Jeshi Mkuu. Kuondoa tatizo hili inawezekana tu endapo uongozi wa chama na Urais vitatofautishwa japokuwa bado Rais atakuwa akitumia vyombo va serikali wakati akihudhuria mikutano lakini itaondoa mikutano kufanyika Ikulu.
ukumbi wa mikutano wa ikulu unakodishwa, so inawezekana ccm walikodi na wamepewa risiti ili wafanyie kikao chao! hata CHAUMA nao wakitaka kufanya mkutano wao next week ruksa!
ni ujinga tu. Kwani Obama anapofanya kampeni kurudi ikulu , anahama ikulu na kukaa home kwake? Rais anaendelea kuwa mkuu wa nchi hata anapofanya shughuli za chama. ni aibu kwa great thinker kuwa narrow thinker.
... Kwani kumbi za mikutano ziko Ikulu na Dodoma tu?Kwa hiyo ni bora kikao kingefanyika Dodoma Rais akachukua ndege akajaza mafuta na kuruka hadi Dodoma!
ukumbi wa mikutano wa ikulu unakodishwa, so inawezekana ccm walikodi na wamepewa risiti ili wafanyie kikao chao! hata CHAUMA nao wakitaka kufanya mkutano wao next week ruksa!
Mkuu, naomba nikiwa nikufahamishe kuwa sina personal issue na mtu yeyote, na uandishi wangu hautawaliwi na hizo. Kama umesoma vizuri nimeuliza swali la kimsingi kuhusu kufanyia vikao vya chama tawala ikulu. Nakumbuka kuanzia enzi za TANU (ndiyo, nakumbuka vizuri sana) vikao vya chama vilifanyika katika ofisi za chama, hata wakati wa Chama kiliposhika hatamu, ndio kwanza makao makuu ya CCM Lumumba street, yakapata hadhi zaidi. Je kumekuwa na mabadiliko rasmi mapya yaliyotokea ambapo chama tawala kimeshika hatamu tena
Naomba kufahamishwa na wale wenye kufahamu zaidi, hivi ni sawa vikao vya CCM kufanyika Ikulu? Ninavyotambua Ikulu huwasikilisha serikali ikiwa ni pamoja na jamii nzima ya Tanzania.
Hivi CUF, TLP au Chadema wanaweza kufanyia mikutano yao Ikulu au katika sehemu zingine kama hizo?
Hiki ndicho chanzo cha swali langu:
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ikulu jijini Dar es Salaam (Photo by Freddy Maro).

Acha kutudanganya watu wazima.Chadema au CAF wakikodisha watakubaliwa au kupigwa mizengwe tu?
sisi ni watawala huwezi kutupangia sehemu ya kufanyia kikao. Funga domo lako
sikudanganyi mkuu, ila haiingii akilini kwa watu wazima kupageuza ikulu kuwa pango la vikao vya wanyang'anyi, haya ni matumizi mabaya ya mali ya umma. ni sawa na kugeuza benzi la ikulu daladala. its not fair kwa nyinyiemu kufanyia vikao ikulu!
Haya mawazo ya kitoto.kama sisim wanatawala wanayo haki ya kufanya vikao popote