lipo tatizo kubwa na tatizo dogo; kubwa ni matumizi ya raslimali za serikali kwa ajii ya CCM. Watumishi wanaowahudumia ni wa serikali, vinywaji (I suppose) ni vya serikali n.k Lakini tatizo hili kubwa vile vile linakuja pale ambapo muda wa kazi za serikali unafanywa na kiongozi wa serikali kufanya kazi za chama kwenye jengo la serikali.
Ukubwa wa tatizo hili unaweza kuja hivi zaidi - kiongozi wa chama cha siasa (sema cdm) anaweza kuitisha kikao cha chama kwenye ofisi ya serikali na kikahudumiwa na raslimali za serikali? NIna u hakika mkubwa watu wengi watakataa kuwa haifai lakini tukifuata mfano wa Rais leo (na ameshawahi kufanya hivyo huko nyuma tukazungumza) jibu ni kuwa kuanzia sasa ni ruhusa kwa viongozi wa kisiasa (bila kujali vyama) kufanya vikao na mikutano yao sehemu zao za kazi. hili ni tatizo kubwa.
Tatizo dogo - nani atamwambia Rais ukweli huu kwa sababu hili linawezekana kwa sababu moja tu - anayefanya hivyo ni Rais; kiongozi mwingine hawezi kufanya hivyo akaachiliwa!
Hili linatuleta kwenye swali jingine angavu: je Rais anaongozwa na sheria/taratibu nyingine ambazo zinafuatwa na viongozi wengine wa umma? Do we have another set of laws zinazompa Rais impunity rais ya kufanya lolote?
Baada ya kusoma posti hii, nimeijua historia ya Tanzania.
Rais kaona ni bora kufanyia kikao ikulu ili kuepusha gharama za yeye kufanyia kikao Lumumba au Dodoma. Ingebidi achome mafuta mengi, posho za wasaidizi wake, pamoja na gharama nyingine za usalama. So akaamua kufanya kikao white house kama best strategy, au vipi?
siku za mwisho za marehemu mtashuhudia mambo ambayo alipokuwa mzima kasingeweza kuyafanya na anajua si ustaarabu.
1.atajisaidia kitandani.
2.atawasahau hata watoto wake.
3.atauza kila kila kitu kama hatakuwa na msimamizi mwernye kuielewa hali yake.
4.atahitaji ushauri wa kiroho zaidi si ajabu akaomba kuitiwa padri(mchungaji) au sheikh.
ukishaona dalili hizi anza mipango ya kurithi kama urithi unakuangukia.
lol kweli maboksi yanadatisha, hivi unayabebea kipande ipi kwa obamaphil?
Lol, naona napewa shule. Siku hizi mna hasira sana. Anyway, maboksi nayapiga kama kilometer mbili hivi kutoka ofisini kwa mjaluo.
Hamna majungu mkuu. Juzi aliwaita CHADEMA na kufanya mazungumzo nao pale. Rais ana ukumbi wa kufanyia mazungumzo.
Watanzania mna mambo mengi ya kulalamika. Lakini hili sio moja.
Nakubaliana na wewe kuwa nadandia tu. Lakini mpaka sasa hamjaonyesha kuwa kitendo kilichofanyika ni kuvunja sheria au utaratibu.
Another ill formed argument example. Tokea lini kosa la mtu likahalalisha kosa la mtu mwingine?....tumwache Nyerere Mkapa alifanya na Mwinyi alifanya.Tujenge utamaduni wa kuthamini utendaji wa watu tusiowapenda si kuwalaumu kwa kila kitu
da hayo maboksi ya huko mbona mepesi, mambo ya white collar jobs tu huko ndio maana unasumbua watu na sarcasm humu!
hivi kweli ukisikiliza haya ya wakuu utaacha kupatwa na hasira kweli: ''Sizitaki mbichi hizi'' Spika kutogombea ubenge katika jimbo lake. - YouTube ?
Kwani Hitler alivyoua watu zaidi ya milioni sita alivunja sheria yoyote ya Ujerumani?
Duh ndio maana mna hasira. Anasema mimi Mkristu sidanganyika. Wakati anayoyasema ni uongo mtupu. Yaani tayari amesha-imply kuwa yeye sio mkristu.
Inaonyesha ni mtupu kikatiba na vifungu vyake, pia ni mtupu kwa masuala ya sheria ya vyama vya siasa.Kwa masitakabari huo si vyema kundandia mambo usiyo yafahamu waachie wachambue mada wanaofahamu.Kuita wawakilishi wa vyama vya siasa ni katika msitakabari wa kiutawala katika kuandika katiba mpya ambayo yeye ndo msimamizi mkuu na amekula kiapo kuilinda.Hivyo kuwaita ikulu ni katika masuala ya kiutawala hata kama anakutana na wakulishi wa vyama vya siasa.
Kufanyia vikao vya kichama ikulu si sahihi kwa sheria ya vyama vingi.Ikulu ni kiutawala na si mambo ya kisiasa ya chama fulani kufanyia vikao vya kichama mahala pale.Huko ni kukiuka kutumia amali za watanzania na fedha za watanzania kukidhi masuala ya chama fulani ni kinyume .Kama kuna uthibitisho anapaswa kushitakiwa kutumia madaraka vibaya kukidhi haja ya kisiasa kinyume na kiapo na katiba ya nchi kwa kuvunja sheria ya vyama vingi inayokataza kufanya mambo ya kisiasa kwa kutumia mali ya serikali na kwenye ofisi za serikali kama ikulu.
Nimesoma. Hayo ndio mambo tunayolalamika hapa Marekani. George Bush alipokuwa rais, Democrats walikuwa wanasema anatumia F1 kwa safari za kisiasa. Sasa hivi yupo messiah Obama. Yeye anafanya yale ya Bush.
ukisoma haya maneno ya jirani yake ndio utazidi kukasirika: Yahoo! Groups
Clinton alikula uroda na Monica Lewinsky wapi? Oval Office.
Walikuwa wanafanya hivyo kama marais au wenyeviti wa vyama vyao?
JK Aongoza Kamati Kuu Ikulu Leo February 27, 2012
Mkuu msamehe tu huyo kilaza,unajua watu wengine wana ubongo wa kuku