Ni haki pesa za nauli za watumishi(walimu) kutumika katika matatizo binafsi ya mkurugenzi?

chama mpangala

JF-Expert Member
Sep 3, 2015
514
710
Hili limetokea Halmashauri ya Mji Bariadi. Mkurugenzi alisababisha ajali siku ya Jumatatu ya Tarehe16 /09/2019 saa tatu usiku.

Alikuwa na NOAH ambayo iligongana uso kwa uso na Pikipiki na kupelekea kifo cha kijana aliyekuwa anaendesha Pikipiki papo hapo.

Kabla ya Ajali hiyo siku ya Alhamisi ya tarehe 12/09/2019 Idara ya utumishi ilitoa agizo kwa watumishi waliomba likizo wajaze form za Vendor kwa ajili ya malipo,watumishi walijaza na kusubiria malipo yao.

Wiki iliyofuata waliyotamka kuwa watalipa ikatokea hiyo ajali mbaya iliyosababishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Bariadi na kupelekea kifo cha kijana.


Hvyo mpaka hivi sasa watumishi(walimu) hawajalipwa Pesa zao hivyo basi inasemekana hiyo pesa imetumika katika kughalimikia mazishi.

SINA HAKIKA ILA INASEMEKANA NA LISEMWALO LIPO KWA SABABU MPAKA SASA HAKUNA ALIYELIPWA NA WALISEMA WATALIPA MAPEMA.

JE, HII NI HAKI?
 
Correlation vs causation.

Beware na hizo unsubstantiated claims.

Pesa za serikali zinaacha trail kote ziendako. Ukweli utajulikana tu.
 
pesa ya umma haitumiki kienyeji kiasi hicho, kama huko halmashauri yanafanyika hayo basi hatuna serikali wa bunge, nchi iko kwenye 'autopilot'.
 
SINA HAKIKA ILA INASEMEKANA NA LISEMWALO LIPO KWA SABABU MPAKA SASA HAKUNA ALIYELIPWA NA WALISEMA WATALIPA MAPEMA.

JE, HII NI HAKI?



Uzuri ni kwamba miongoni mwa washiriki wa uovu ndiyo hufichua siri, hata hili litajiweka wazi muda ukifika
 
Back
Top Bottom