Ni dhahiri vyombo vya dola viko nyuma ya ujambazi nchini

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
1,583
2,697
Ni jambo la ajabu sana Tanzania imekuwa sehemu isiyokalika kutokana na ujambazi wa mara kwa mara. Leo pekee watu wawili wameuawa Dar kwa ujambazi.

Imekuwa si jambo la ajabu tena kusikia mtu kauawa kwa ujambazi, haya yote yanatokea huku kukiwa na serikali yenye vyombo vyote vya dola ambavyo havishindwi kabisa kutokomeza uhalifu huo. Sasa kwa nini ujambazi hauishi?

Kukamatwa kwa police waliohusika kuwaua wafanyabiashara wa meno ya tembo na kisha kuwapora pesa ni dhahiri kuwa vyombo vya dola ndo vipo nyuma ya ujambazi wa kutisha unaoendelea Tanzania.
 
Serikali ni katiba na katiba hairuhusu ujambazi, ila ujambazi hufanywa na watu. Ukiulizwa gover ipo nyuma ya ujambazi utaweza tetea hoja yako.
 
Hoja yako nzuri lakin hujatueleza chochote kuhusiana na matukio hayo mawili wapi nanini kimejili
 
Mkuu umeanza vizuri sana mada yako ila mwisho nahisi kuna harufu ya kujiingiza kwenye cyber crime kuwa makini na uandishi wako
 
Mkuu umeanza vizuri sana mada yako ila mwisho nahisi kuna harufu ya kujiingiza kwenye cyber crime kuwa makini na uandishi wako
sasa mkuu hapo mwisho kwani kuna uongo wowote au jamaa kaongeza chumvi??

au hukusoma maelezo yaliyoandikwa hapa jf kutoka kwenye gazeti jinsi polisi wa kuzuia ujangiri pamoja. na polisi wa kawaida walivyo waua hao wafanya biashara??

mpaka wakamgeuka jamaa aliyewapa taarifa wakaamua kumuua ili waweze kujipatia pesa??
 
Ni kweli hâta watoa taarifa(whistleblowers) wanauwawa tofauti ipo wapi kt ya police na jambazi sasa. Hii nchi imekuwa sio salama kabisa
 
Ni kweli hâta watoa taarifa(whistleblowers) wanauwawa tofauti ipo wapi kt ya police na jambazi sasa. Hii nchi imekuwa sio salama kabisa

Kuna wakati ujambazi ulikithiri sana nchi nzima na hasa Dar. ikabidi serikali ichukue hatua za haraka za kuwastaafisha makamanda wa polisi ; wakati ule ndipo makamanda wengi wa polisi wakiongzwa na IGP Mahita ndipo walipostahafishwa na ujambazi ukapungua!! Ningeshauri makamanda wa polisi waliochoka kama KOVA wapumzishwe ili makamnda wenye mtazamo tofauti waingie kukabiliana na uhalifu huu!!
 
Yaani tena mchana kweupe .. Inatia hasira kwa kweli

Sasa huo mchana kweupe ndio hao mnaohisi ni Polisi huwa wanafanya uhalifu au ndio muda uhalifu hutokea? Kitaalam,wizi wowote wa kuhusisha benki au taasisi za kifedha au uchukuaji na utoaji fedha,hufanyika mchana,ila sio kweli kuwa kila tukio utupie lawama kwa Polisi utakuwa unakosea sana
 
Ni jambo la ajabu sana Tanzania imekuwa sehemu isiyokalika kutokana na ujambazi wa mara kwa mara, Leo pekee Watu wawili wameuawa dar Kwa ujambazi,
Imekuwa si jambo la ajabu tena kusikia mtu kauawa kwa ujambazi, haya yote yanatokea huku kukiwa na serikali yenye vyombo vyote vya dola ambavyo havishindwi kabisa kutokomeza uhalifu huo,
Sasa kwa nini ujambazi hauishi?
Kukamatwa Kwa police waliohusika kuwauwa wafanyabiashara wa meno ya tembo na kisha kuwapora pesa ni dhahiri kuwa vyombo vya dola ndo vipo nyuma ya ujambazi wa kutisha unaoendelea Tanzania.
kwenu rwanda hakuna majambazi?
 
Mleta

Mleta mada naona umeuliza swali kisha ukajijibu mwenyewe.
 
Kamanda Kova na vijana wake wanahusika sana. Ukiona jambazi kakamatwa na kuuliwa basi huyo hajashirikiana na polisi wa Kova.
 
Kuna good cops and bad cops
Nafikiri mpaka hapo ntakuwa nmeeleweka

Ovaaa
 
Zaman kulikuwa na majambaz ndio lakin walkuwa cyo kama Leo. Yani wanajiamin hawaogopi utadhan hamna serekali. Angalia tukio la sista wa romani, yule mlokole mlimani city, cocacola moshi,yule muhaya muhadhir wa chuo kikuu udsm, chanika benki dakika 45 na huyu jana wa zantel. Mifano hii ni michache kati ya mengi. Serekali ipo wapi?
 
Mkuu umeanza vizuri sana mada yako ila mwisho nahisi kuna harufu ya kujiingiza kwenye cyber crime kuwa makini na uandishi wako
uoga ndo unaotuponza....
the government shud be for the ppl, by the ppl, sio opposite..sasa tukisema yanayoonekana live tunakamatwa..wTF is wrong with this country
 
Nikiangalia tukio la Sinza, nawakumbuka akina Tundu Lissu & John Mnyika walivyoipigia kelele sheria ya kulinda "Wapuliza kipyenga/Whistle blowers." Kama tukio dogo kama lile limegharimu maisha ya mpiga filimbi, vipi kuhusu kutoa taarifa kwa matukio makubwa zaidi?
 
Back
Top Bottom