Bambushka
JF-Expert Member
- Jan 9, 2020
- 3,956
- 7,209
Asipokuwa imara na akawa na misimamo tofauti tutanyongeka SANA,Kwa sababu ya sacrifice ya maisha yake, Watanzania wamekuwa masikini zaidi katika Kipindi cha uongozi wake na wataendelea kuwa masikini katika uongozi unaoanza leo. Uongozi unaoanza leo ni wa Awamu ileile ya Tano inayoishia mwaka 2025 lakini bahati mbaya, Kikatiba unaruhusiwa kugombea kuongoza Awamu ya Sita ya miaka 10. Rais mpya akisaidiwa na Makamu na Baraza la Mawaziri lililopo, kwa sababu nyingi tu, atalazimika kuendeleza misingi mibovu iliyowekwa na sacrifice ya mtangulizi wake. Makamu wa Rais anategemewa kuteuliwa na Chama kinachosimamia utekelezaji wa Ilani yake kupitia sacrifice ndo maana tulikuwa na Serikali ya Magufuli, Tanzania Mpya ya Magufuli, CCM Mpya ya Magufuli na Wapiga Kura wake. Binadamu yeyote ana manufaa kwake na Jamii akiwa hai!
Kiukweli naomba awe na washauri wazuri wenye nia dhabiti dhidi ya watanzania wa kawaida siyo watu wa mijini tu!
Arudishe mzunguko kwenye biashara za kawaida, aachane na sera kandamizi za kukamua ng'ombe wasio na malisho.
Aangalie HESLB! TRA! Ajira e.t.c
Aelewe shida zetu! Biashara kati ya watanzania, na majirani zetu!
Aondoe uchafu uliojaa barabarani kwa jina la umachinga!
Vibanda viondolewe biashara zifanyike maeneo halali!
Everyday is Saturday................................