Ni bora tu nipewe Limbwata...

Ni bora tu nipewe Limbwata...

Sodoku

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2016
Posts
1,277
Reaction score
2,933
Sometime nakuwa na wivu wa kijinga sana. Usiku wote sikulala kuna msg iliingia kwenye simu ya wife inasema "honey nakutakia usiku mwema na uniote" basi nikapaniki kwel kuangalia vizuri jina kumbe ni msusi wake wife mwajuma. Nikajiona fala nina wivu wa kijinga sana.

Mara nyingi tu zinapigwa simu usiku mkali wife anaamka anaenda kuongea sebuleni ili asiniamshe.nami of koz sina tabia za kike kusikiliza eti anaongea na nani. Huwa ananambia ni rafiki zake sometme wanampigia simu usiku mkali wampe ubuyu.

Sasa jamaa yangu mmoja anatabia za umbea anadai wife anatembea na jamaa mmoja hivi pale mtaani. Kumbe hamna lolote waswahili tu wakiona mnaishi vizuri hawakosi maneno maneno.

Mwanzon nlianza kuona wivu lakin baadaye nikaona aargh maneno tu. Unajua si wengine tukipenda tunapenda kweli kweli asikwambie mtu. Jana nikawa naongea na wife namshauri ili watu wasitugombanishe basi ajaribu kunitafutia hata limbwata aniwekee. Niwe sisikii sioni zaid yake.

Sasa najiuliza limbwata ya wapi ni nzuri?kuna watu wanasema ya tabora,wengine tanga na kunamwingine anasema ya pemba au mombasa na lamu. Mi sijui lakini ndo nahangaika hiv kuuliza kama kuna mtu kawahi wekewa au mwekea mwanaume. Ila isiwe ya kunifanya niwe mwehu.

Lengo langu niishi kwa amani nisione mapungufu yake. Maana binadamu tuna mapungufu. Pia sitak kufa kwa kihoro nampenda mke wangu.nlipata shida sana kumpata watu hawajui tu.

Nasikia ukiwekewa limbwata unakuwa na amani sana kwenye uhusiano. Nami nataka niwe na amani nichape kazi tu na si kumhisi hisi vibaya au kusikia maneno ya wachongefu.

Mimi binafsi sitak hata nitamani mwanamke mwingine. Sitak kabisa na siku ilitokea nikamsifia dada mmoja ilibidi nirudi home kumwomba msamaha wife kuwa nimekosea sana huko barabarani.

Nashukuru amefuata ushaur wangu wa kuniwekea limbwata asub yote hii anapiga simu kwa wenzie kuulizia atapata wapi limbwata nzuri. Nimewambia tu aniwekee wakat sijui.
 
Huo mchezo unaotaka kuufanya ni sawa na kujilipua kwa kujitoa mhanga.....ugaidi huo.
 
Njoo chukua limbwata la kipogoro huku Malinyi-Morogoro
Yaan utaishi kwa aman miaka yote
Pia limbwata la kwetu hali expire mapema
Yaan utampikia, kumfulia chupi, kumpa na kondomu ili asikuambukize, utawafukuza ndugu zako, utampa mshahara wote ili ahonge wanaume wengine, utakuwa unalala sebulen ili room uwaache wajichane na mkeo
Kama umelipenda bas krb malinyi nauli kutoka Moro twn had malinyi ni 23000
 
Mkuu hujui kuwa mwangosha anaseviwa mwajuma, davy anaseviwa diana.
Utakufa kwa presha
 
Njoo chukua limbwata la kipogoro huku Malinyi-Morogoro
Yaan utaishi kwa aman miaka yote
Pia limbwata la kwetu hali expire mapema
Yaan utampikia, kumfulia chupi, kumpa na kondomu ili asikuambukize, utawafukuza ndugu zako, utampa mshahara wote ili ahonge wanaume wengine, utakuwa unalala sebulen ili room uwaache wajichane na mkeo
Kama umelipenda bas krb malinyi nauli kutoka Moro twn had malinyi ni 23000
chukua hio
 
Ha ha ha kijana hapana chezea Limbwata ya Tabora au Ifakara,yaani unakuwa ndondocha kabisa,na kazini huendi wewe unashinda ndani tu,wewe ndiyo utakuwa mpishi wa nyumba...limbwata ya huko itakufaa sana..
 
Siku hizi utashangaa mwanamke mwenzake anakugongea wife material.Limbwata pekee nenda kakope Bank au Pride hutajuta..
Hahahh mambo ya kusaga na kukoboa wabaya sana walee
 
Ha ha ha kijana hapana chezea Limbwata ya Tabora au Ifakara,yaani unakuwa ndondocha kabisa,na kazini huendi wewe unashinda ndani tu,wewe ndiyo utakuwa mpishi wa nyumba...limbwata ya huko itakufaa sana..
Sasa kuna raha gani ya kumfanya hivyo mumeo
 
Pole we mzee apo penyewe upo kwenye limbwata tosha, na mtu anaekufanyia limbwata hakupendi unamlogaje mumeo!
 
Mpe Yesu Maisha Yako na uokoke kwelikweli...hiyo ndo limbwata pekee...mengine ni yakichina
 
Back
Top Bottom