Zero IQ
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 13,917
- 24,674
Hatua kwa hatua jinsi ya kupika mboga aina ya kabichi
Kabichi 1/2 kilo
Nyanya ya kopo 1/2
Kitunguu 1
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Chumvi
Olive oil
Matayarisho
Kwanza kabisa bandua magada ya juu ya kabichi, kisha ioshe na uikaushe maji baaba ya hapo katakata kabichi (inapendeza zaidi kama ikikatwa nyembamba) kisha saga pamoja nyanya na kitunguu.
Baada yahapo tia katika sufuria ya kupikia, ipike mpaka maji yote yatakapokauka kisha tia chumvi, curry powder na mafuta pika kwa muda kiasi kisha tia kabichi na upunguze moto.
Pika mpaka kabishi itakapoiva kisha ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila kwa wali au ugali.
*********
Jinsi ya kupika kabichi kwa mayai
Habari mdau wa jinsi ya kupika. karibuni tena katika jiko letu. Leo tuandae mboga ya kabichi. Mboga hii yaweza kupikwa kwa nyama, njegere, yenyewe tu kwa viungoviungo, na aina tofauti tofauti, lakini sisi leo tuipike na mayai, ni nzuri sogea karibu tuandae wote.
Mahitaji
- Kabichi 1
- Mayai 4
- Mafuta robo
- Vitunguu 4
- Nyanya 5
- Karoti kubwa 1
- Pilipili manga kiasi
- Chumvi kiasi kwa ladha
Jinsi ya kupika kabichi hatua kwa hatua
- Andaa kabichi uikatekate kisha uikoshe.
- Bandike jikoni iive kidogo kisha iweke pembeni.
- Menya nyanya, kata vitunguu na karoti uviweke tayari kwa mapishi.
- Bandika sufuria jikoni utie mafuta, yakipata moto tia vitunguu ukaange mpaka vibadilike rangi kisha tia nyanya ukaange.
- Tia karoti kaanga kidogo, tia kabichi, pilipili manga na chumvi, vunja mayai uyapige uyatie. koroga hadi likauke, hapo linakua tayari.
***********
Kabichi ya nyama
Mahitaji
- Nyama ya ngombe 1/2 kilo
- Vitunguu maji viwili
- Nyanya nne
- Pilipili hoho nusu
- Kabichi 1
- Viazi vinne
- Karroti 1
- Njegere nusu kikombe
- Mafuta vijiko vitatu vya supu
- Kitunguu saumu
- Pilipili manga kiasi
- Kata nyama,osha,weka chumvi,kitunguu saumu na pilipili manga acha chemsha na uikoroge ili viungo vikolee,ongeza maji kuifunika nyama,acha iive
- Kata kabichi kama vile unavyokata la kachumbari lioshe na maji ya vuguvugu,Tayarisha kitunguu,nyanya,karoti,viazi vigawe mara mbili.
- Injika chungu jikoni,weka mafuta yapate moto,kaanga kitunguu mpaka kibadilike rangi kiwe hudhurungi,weka nyanya,viazi,supu ya nyama na nyama uloichemsha,acha nyanya iive mpaka ipondeke.Na mchuzi uwe mzito.
- Weka carrot na njegere pamoja na kabichi.Acha viendelee kuiva sosi ya kwenye kabichi ikikaribia kukauka weka pilipili hoho acha vichemke dakika kadhaa kisha epua.
- Ongezea chumvi ikiwa haijatosheleza
Mchango wa mdau
Hivi ni nani aligundua kwamba kabichi ni Mboga asee,
Mbona tunatesana hivi si ni bora aliyegundua mrenda japo unatereza lakini ni mwake na ugali kitu kinaenda.
Hivi ugali na kabichi kuna ambae anauelewa kweli ?
Tuache tuseme tu ukweli ni bora nile ugali bila mboga kuliko kula ugali na kabichi.