Ni Ajabu na Kweli

JF2050

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Posts
2,085
Reaction score
45
Kuna mdada (ni mzuri) mmoja huwa tunapishana kwenye korido katika sehemu ninayofanyia kazi na tunafahamiana kama mwaka hivi. Sasa kuna siku zamani kidogo, nakumbuka tulishawahi kujikuta tupo pamoja sehemu, na watu wengine.

Sehemu hiyo yaliibuka mazungumzo yasiyo kuwa na kichwa wala miguu kuhusu mambo ya mahusiano na ndoa (kuna jamaa fulani aliyaanzisha). Mie sikuwa nachangia kitu bali niliamua kuwa msikilizaji. Kadri mdahalo uliyoendelea, mie nilizidi kuwa kimya, ghafla huyo dada akanicharukia, "sasa wee kaka mbona huchangii, unanitia hasira unajua!", mie nikajua ni utani, nilimjibu aahh mie nasikiliza tu dada, kuna vitu najifunza hapa. Alionekana kutokuridhika na jibu lakini, niliendelea kunyamaza.

Jana, tukawa tumekutana kwenye mgahawa hapo kazini, ghafla:

Yeye: Kaka mambo, za siku, wifi hajambo?

Mimi: Hajambo (ingawa sina huyo wifi yake), dah, sijakuona muda, u mzima wa afya?

Yeye: (Hakujibu salamu) Wewe mtu wa ajabu kweli umeoa! (kwa kutahamaki)? Mbona sijui, unamaanisha? (Kulikuwa na watu hapo mgahawani, niliona aibu kidogo)

Mimi: Ndio, kwani ni vibaya?

Yeye: Wa wapi mkeo? Una hata picha yake nimwone, kweli wanaume mna vituko!

Mimi: (Nikajisemea hii sasa so!) Nikamshika mkono, nikamwambia twende tukakae kule wahudumu watatuletea chai (lengo tuende mbali kidogo na watu, maana watu walishaanza kuangalia na kufuatilia movie bila kulipia). Nikaingia whatsAp nikamwonyesha profile pic ya mimi49 (mimi ni mzuri kweli kweli).

Yeye: Toa picha lako hapa bwana, utauziwa vya kichina mpaka ukome (nikasema huyu dada ana lake jambo)

Mimi: Hiki ni kifaa natural, mchina, ni wewe hapo na manywele yako (niliudhika ndio maana nikamjibu hivyo)

Yeye: (Akatema mate, akaondoka kwa hasira, huyo katokomea), Unajidai sana, ndio maana siku ile watu tunajadili mambo ya msingi, ati wewe umenyamaza (alivyosema hivyo akanikumbusha hiyo siku nikajua, mmmhh huyu ana matatizo)

Pale mgahawani watu wakawa wananiambia kaka pole, kulikoni? Nikawaambia sijajua lakini nahisi huyu dada kuna kitu kimemtibua, hatuna uhusiano wowote zaidi ya kuonana na kusalimiana.

Sasa nimeamini wakati mwingine katika muda na mazingira usiyoyadhania tegemea lolote na uwe tayari kulikabili!
 
Last edited by a moderator:
Inawezekana kakupenda na anahtaj muwe pamoja,kwa hilo hatapenda kuskia upo kwenye mahusiano
 
Nina uhakika kusingekuwa na watu hapo title ya sredi ingekuwa 'Mwenzenu nimebakwa na jimama lenye uchu wa mahaba'...

Mi namkubali dogo kwa uhodari wake wa kuanzisha thread. Baaas!
 
Mi namkubali dogo kwa uhodari wake wa kuanzisha thread. Baaas!

Hahaha mpwa inabidi afanye kolabo na Mentor ficharingi Mtambuzi watoe JF Muvi....

Halafu kwenye matangazo awepo Ndyoko
 
Simlicity mi nakikubali kipaji chako cha utunzi wa riwaya!
 
sasa ww ndo nini??? wakati ushapendwa na ww umependa unazuga zuga tu hapa hebu nenda huko
 
kusoma hujui hata picha uelewi.... ndo maana aliondoka kwa hasira angekutemea mate usoni loh!!!! wakati mwingine jifunze ukitaka kujua undani wa mambo usitumie kasoro ya mtu kujibu chochote kama hapa ulivyofanya "Mimi: Hiki ni kifaa natural, mchina, ni wewe hapo na manywele yako (niliudhika ndio maana nikamjibu hivyo)" hapa yawezekana alikuwa anataka kukutongoza ukaharibu,..... umekosa utamu ungekuja na story nyingine tamu zaidi labda ingeanza ivi kuna dada kanitongoza eh.....................................
 
Nimekukubaili mwana wewe kweli kiboko wa uzi yaani
umenishinda hata mm bi kidude
 
Kaniudhi tu kusema unajidai. Sasa hakikisha afikirie kuwa wewe muhaya, una Masters zote na una mpunga balaa. Jisifie. Atakufa kwa pressure. Kuna watu wanaudhi sasa unajidai nini hapo!!
 
duh kila siku matukio yanakukuta wewe tu mi nashangaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…