Ni aibu Sana Kuwa Mtanzania

Ni aibu Sana Kuwa Mtanzania

wiseboy.

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2014
Posts
2,931
Reaction score
4,549
Ukweli unauma na ndo tabia yake,wengi wetu tunauchukia ukweli kwa kuwa tu unauma,ni aibu sana kuzaliwa ktk taifa ambalo lina kila kitu lakini bado limeshindwa kusimama kiuchumi,ni aibu sana kuwa raia wa taifa ambalo gavana wa benk kuu anafariki ughaibuni halafu eti anazikwa huko kisa serikali haina hela ya kumsafirisha,ni aibu sana kuwa raia wa taifa ambalo gavana wake wa benk kuu anadai kuwa sh imeporomoka kwa kuwa wahisani hawajatoa misaada,tangu lini uchumi ukakua kwa kuomba omba badala ya kuwa na vitega uchumi?

Ni aibu sana kuwa raia wa taifa ambalo rais wake hajui kwanini nchi ni maskini,ni aibu sana kuwa raia wa taifa ambalo dhahabu zinaenda nje na kuwaacha wananchi ktk ufukara mzito,maeneo yote ya migodi wananchi wanaishi ktk nyumba za tope,nyasi na hakuna zahanati wala shule bora,ni aibu kuwa ktk taifa ambalo bunge linapoteza muda kutunga sheria ya kuminya uhuru wa kupashana habari na kuacha mambo ya msingi kwa taifa kama kulinda raslimali,ni aibu sana tena sana kuwa mtanzania,acheni ukweli usemwe.
 
Sasa na wewe unaongeza tatizo
kulalamika lalamika nako kunaongeza tatizo

Kuna mengi ya nchii mazuri hata huko Ulaya na Marekani huyapati...

Taifa la miaka 50 ni taifa changa sana.....Hiyo Africa kusini
ilianza kujengwa na wazungu miaka zaidi ya 100 iliyopita na leo umasikini bado upo

Kennedy alisema 'usiulize Marekani itakufanyia nini,uliza wewe utaifanyia nini Marekani'
wewe utaifanyia nini Tanzania?
 
Hata kama nchi imejaliwa utajiri wa hali ya juu kama hao waliojivisha ngozi ya uongozi ni wezi, mafisadi, wapokea rushwa mikataba yote wanayosaini wanasaini gizani na kuifanya siri kubwa utadhani utajiri wa nchi hii ni wa watu wachache badala ya Watanzania wote. Kwa hali maendeleo tutayaona kwenye nchi za wenzetu tu.

Ukweli unauma na ndo tabia yake,wengi wetu tunauchukia ukweli kwa kuwa tu unauma,ni aibu sana kuzaliwa ktk taifa ambalo lina kila kitu lakini bado limeshindwa kusimama kiuchumi,ni aibu sana kuwa raia wa taifa ambalo gavana wa benk kuu anafariki ughaibuni halafu eti anazikwa huko kisa serikali haina hela ya kumsafirisha,ni aibu sana kuwa raia wa taifa ambalo gavana wake wa benk kuu anadai kuwa sh imeporomoka kwa kuwa wahisani hawajatoa misaada,tangu lini uchumi ukakua kwa kuomba omba badala ya kuwa na vitega uchumi? Ni aibu sana kuwa raia wa taifa ambalo rais wake hajui kwanini nchi ni maskini,ni aibu sana kuwa raia wa taifa ambalo dhahabu zinaenda nje na kuwaacha wananchi ktk ufukara mzito,maeneo yote ya migodi wananchi wanaishi ktk nyumba za tope,nyasi na hakuna zahanati wala shule bora,ni aibu kuwa ktk taifa ambalo bunge linapoteza muda kutunga sheria ya kuminya uhuru wa kupashana habari na kuacha mambo ya msingi kwa taifa kama kulinda raslimali,ni aibu sana tena sana kuwa mtanzania,acheni ukweli usemwe.
 
Mkuu hamia somalia hakika hutojuta. U'll never regrets to be a somali citizen.
 
Sasa na wewe unaongeza tatizo
kulalamika lalamika nako kunaongeza tatizo

Kuna mengi ya nchii mazuri hata huko Ulaya na Marekani huyapati...

Taifa la miaka 50 ni taifa changa sana.....Hiyo Africa kusini
ilianza kujengwa na wazungu miaka zaidi ya 100 iliyopita na leo umasikini bado upo

Kennedy alisema 'usiulize Marekani itakufanyia nini,uliza wewe utaifanyia nini Marekani'
wewe utaifanyia nini Tanzania?


kwa nchi hii inavyoibiwa kila kukicha haijengwi inabomolewa mkuu kwa kiasi fulani upo sahihi mkuu, yaani Tanzania ina kila kitu ambacho hata wazungu wanatuona hatunazo kwa kukimbilia kubeba mabox na rasilimali za kutosha tatizo ni waliopata kuongoza hatoi fursa kwa watanzania wenzao.south watu ni masikini lakini fursa zipo asipozitumia fursa he/she atakufa maskini nakutolea mfano mdogo kuwa na uraia tuu wa south ni mtaji tosha unaweza kukopa chochote bila hata kuweka deposit na unapewa mkopo uwe wa kujenga shule,hosptal au kampuni ya usafirishaji wenyeji wamelala wageni wanao wasouth then wanatumia izo fursa. Hapa kwetu fursa zpo kwa watu wachache ndio maana unaona watu wanakimbia kimbia.
 
Tatizo lipo kwako kama individual....usisingizie taifa
 
Hii nchi yote inabidi iwe shamba la mpunga au miwa!kusiwepo na mtu hata mmoja.
Kwa style hii ya ccm na serikali yake haitotufikisha popote
 
nimeipenda sana hii kauli yako, umefikiri sana mkuu

Unafikiri mkuu wengine tumekuwa tukilelewa kimkandamkanda mpaka mzazi anatuambia alitulea kimagumashi,kutokana na huduma mbovu ya afya nk, mzazi anaomba usitume maana itakuwa shida.
Tz bado kuna familia nyingi zinaishi kwa
kwa betting tu,mtoto Anakuwa hana uhakika wa huduma ya afya, elimu ana unga unga,chakula nayo ana ungaunga huyo akifika 15 years lazima awe kauzu
 
Back
Top Bottom