Ni aibu na fedheha kwa Tanzania kuagiza nje makaa ya mawe na gypsum

LAZIMA NISEME

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
240
267
TANZANIA kuna rasilimali kubwa ya makaa ya mawe ambayo mpaka sasa inafikia tani trilioni 1.5. Makaa hayo yapo ukanda wa Kusini mwa Tanzania ambayo ni Mbeya-Kiwira na Ruvuma katika ukanda wa Mto Ruhuhu. Makaa ya mawe ni nishati lakini uzoefu uliopo hayajatumika katika kuchangia upatikanaji wa nishati nchini za viwanda na majumbani.

Upande wa viwandani kuna mtambo mmoja wa Kiwira ndio unazalisha umeme,Vile vile viwandani unatumika kwenye viwanda vya saruji Tanga, Mbeya, kile cha karatasi kilichopo Mgololo na cha Dangote kilichoko Mtwara.

Katika hili nasikitika sana kwa Dangote Kuwa JIPU la kutisha nchini, Wanamkataba TANCOAL kila mwezi Tani 13,500 cha kushangaza tangu kiwanda hiki kimefunguliwa wamenunua Tani 2000 tu,Wanaingiza Makaa ya Mawe toka Afrika kusini na November mwaka jana waliingiza Tani 45,000, Agent akafanya manuva wakaclea mizigo kwa provision clearance wakapewa siku 14 kulipa VAT ama kupeleka msamaha wa kodi amabao kwa taarifa tu walishawahi kupewa na TIC lakini hadi leo daa siku kumi na nne hazijaisha, hawajalipa na hivi sasa Meli ya Makaa ya Mawe yenye Tani 36,000 kutoka Afika Kusini na na Nyingine ya Gypysum Tani 36,000 kutoka Oman bila kibali cha Importation kutoka Wizara husika Nishati na madini,Nasasa wanashinikiza mzigo ushuke Daaa!!

Ukakasi huu na hujuma mbaya kwa Taifa vinaifanya Dangote kuwa moja ya majipu ya kutisha wakisaidiwa na mzawa mwenzetu KAZIMOTO wa Pale PTA akisaidiwa na Wahindi kadhaa na wazawa wengine Majipu.

Nakumbuka Waziri Muhongo alifanya ziara nchi nzima na kuwatambua wachimbaji wadogo wenyeuwezo wa kuzalisha mamilioni ya Madini haya, aliwataka waunde umoja na aliagiza Makampuni haya kununua Madini haya kutoka kwa wazawa kuzalisha ajira na Faida kwa Taifa na alienda Mbali zaidi na kutukumbusha kwamba haya madini yanaubora kuliko madini hayo kwa kiwango kikubwa,TBS sinauhakika juu yenu kwa hili maana sina uhakika kama ukaguzi wa ubora wa bidhaa kwa yale ya November

Je ni kweli Ubora wa Dangote na ahadi zenye neema kwa nchi hasa mikoa ya kusini ndiyo hiyo,Najiuliza juu ya wakala mzawa kuwatetea wawekezaji juu ya kutolipa VAT Jipu hili ni ukakasi kwa Serikali ya Magufuli maana siku mbili tu alipopokea kijiti Amiri jeshi wetu mkuu pale Wizara ya Fedha alifoka kutotoa misamaha ya kodi lakini nakumbuka mwaka jana Bunge letu tukufu lilifuta utoaji misamaha ya VAT kwa wawekezaji wote wa TIC,hawa wawekezaji nchi zote walizowekeza wanalipa Kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na wanauwezo wa kulipa.

Gypysum inapatikana kwa wingi pale Lindi inakuwaje wanaagiza kutoka Oman,nawaita Takukuru kuchunguza Majipu ya mawakala wa namna hii,What about our National interest?
Hata hivyo moja ya Dangote kujengwa Mtwara ni matumizi ya Gesi yetu asilia,kupata pesa na kusaidia ajira Ukakasi unaikumba Dangote upande wa ajira pia kunaunyanyasaji na rushwa ya kutisha kupata ajira vinavyo fanywa na HR(Chapalwa).

Takukuru nendeni Pale ni aibu kwa Taifa,Kapwapwa na HR Chapalwa anatumika katika kuwawahujumu waliokosa vigezo kupata ajira ndani ya kiwanda wafunga Tulubai za magari yanayopakia Sementi wanakatwa posho zao malalamiko yako hadi kwa Wenyeviti wa maeneo husika yanayozunguka Majirani wa Aliko Dangote.

Udereva unatoa laki 3 na wafunga turubai wako katika vikundi wanatozwa 5000 kwa kila Lori linapolipa ujira wake wa 15,000 kufungiwa ikumbukwe Kiwanda kinauwezo wa kuzalisha kwa siku Tani 7500 hata kuingiza zaidi ya Maroli 500 kwa siku. Mmoja wa Wenyeviti analalamika anasema Toka wakati wa ujezi HR huyu amehujumu wananchi wetu wengi ni aibu hapa mtu huyu,uliza dada yoyote hapa atakupa sifa zake,Wizi wa Mafuta uliokithiri vinatia doa nchi yetu kwa wawekezaji. Serikali ya Tanzania ilitoa msamaha wa kodi lita zaidi ya milioni 2 kwa Dangote wizi huu kwa siku unaihujumu Dangote lita 1000 kila siku unafanywa na wazawa washirika wa HR Takukuru Mpoo????

Pongezi za dhati kwa Waziri wa Fedha kwa kulinda maslahi ya Taifa na Pongezi Prof. Muhongo kwa kuthamini wachimbaji na kusimamia Taratibu, Sheria na Maslahi mapana ya Taifa Letu baada ya kubaini Jipu hili la Dangote na kuchukua hatua kali dhidi ya hujuma hii kwa Taifa. Sisi Wazawa wachimbaji wadogo wadogo tuko pamoja nanyi tutapigania haki na maslahi ya Taifa letu Tunapongeza juhudi za Rais wetu katika Vita dhidi ya Rushwa, ubadhirifu vilivyolitafuna Taifa letu kwa kiwango kikubwa.
 
Kweli sio jambo la kawaida namnahii tunajilaani wenyewe mali nying Mungu ametupa tunashindwa kuzitumia tuinuke sasa watanzania kumekucha sio wakati wakulala tena
 
Mleta mada Hamna mwenye huruma katika taifa hili. Watanzania ni wabinafs selfish and greedy. Watanzania wengi wana ukarim wakinafik. Wewe jijali mwenyewe
 
Hii ndiyo Tz bhana,Jana nimeona kwenye supermarket moja majani ya chai toka Bhuttan
 
Inawezekana changa Moto ni usafiri wa reli wa hayo makaa ya mawe toka Huko ruvuma to mtwara labda watu mie Meli via itungi , halafu Tazara hadi dar , halafu Meli hadi mtwara
 
Gharama ya makaa ya mawe ya Mbeya unaijua? Hivi kuna mfanyabiashara yeyote anayeweza akaacha makaa ya mawe ya shs 50 akanunua ya shs 100 wakati yana ubora sawa? Inabidi mpunguze bei yenu ya chokaa na makaa ya mawe hamna jinsi!
 
Gharama ya makaa ya mawe ya Mbeya unaijua? Hivi kuna mfanyabiashara yeyote anayeweza akaacha makaa ya mawe ya shs 50 akanunua ya shs 100 wakati yana ubora sawa? Inabidi mpunguze bei yenu ya chokaa na makaa ya mawe hamna jinsi!
hivi ina maana makaa ya mawe ya mbeya yana bei kuliko ya south Africa? plus usafirishaji maana south kwa tani najua haivuki dola 100 ina maana Tanzania bei yetu inaweza zidi dollar100?
 
Inawezekana changa Moto ni usafiri wa reli wa hayo makaa ya mawe toka Huko ruvuma to mtwara labda watu mie Meli via itungi , halafu Tazara hadi dar , halafu Meli hadi mtwara
Hapana mkuu, kitaalam ni kwamba ubora wa makaa ya mawe ya Tanzania ni hafifu kulinganisha na ya south Africa.
ubora wa makaa ya mawe unapimwa kwa ASH CONTENT. the higher amount of ash content the weaker is your makaa ya mawe. muwekezaji anapata hasara coz anapata energy kidogo akitumia makaa yetu ni faida zaidi kutumia ya south Africa.
(hapa nadhani chemical engineers, mechanical engineers na mineral processing engineers mnanielewa vizuri).

waliambiwa kushusha bei, lakin gharama za uchimbaji ni kubwa na nihasara kuoperate kama wakiuza kwa bei walio calculate wenye viwanda vya saruji.

kumbuka sio dangote tu, hata tanga cement wanatumia makaa ya mawe kutoka south Africa.
Fanyeni argument kitaalam na sio kisiasa zaidi.
 
Meli ya Makaa ya Mawe yenye Tani 36,000 kutoka Afika Kusini na na Nyingine ya Gypysum Tani 36,000 kutoka Oman bila kibali cha Importation kutoka Wizara husika Nishati na madini,Nasasa wanashinikiza mzigo ushuke Daaa!!

Tunapaswa kuwa makini isije kuwa humo kuna vipandikizi vya kutupunguza ili mbele ya safari wajimilikishe nchi
 
Hapana mkuu, kitaalam ni kwamba ubora wa makaa ya mawe ya Tanzania ni hafifu kulinganisha na ya south Africa.
ubora wa makaa ya mawe unapimwa kwa ASH CONTENT. the higher amount of ash content the weaker is your makaa ya mawe. muwekezaji anapata hasara coz anapata energy kidogo akitumia makaa yetu ni faida zaidi kutumia ya south Africa.
(hapa nadhani chemical engineers, mechanical engineers na mineral processing engineers mnanielewa vizuri).

waliambiwa kushusha bei, lakin gharama za uchimbaji ni kubwa na nihasara kuoperate kama wakiuza kwa bei walio calculate wenye viwanda vya saruji.

kumbuka sio dangote tu, hata tanga cement wanatumia makaa ya mawe kutoka south Africa.
Fanyeni argument kitaalam na sio kisiasa zaidi.
Mkuu hayo majivu huwa wanadispose wapi?
 
Tunapaswa kuwa makini isije kuwa humo kuna vipandikizi vya kutupunguza ili mbele ya safari wajimilikishe nchi
Tatizo kubwa la Tanzania NA ambalo naliita donda NDUGU Kwenye utungaji wa sheria zetu Ni pale ambapo kila sheria mpya inakuja NA uanzishwaji wa Taasisi mpya. Matoke yake serikali imejaa utitiri wa Taasisi ambazo zinaiongezea gharama serikali pasipokuwa NA umuhimu wowote.
C&P
Sheria Za EPZ, SEZ. PPP, strategic Inversor, zote zinaainisha aina tofauti ya incentives wanazopewa wawekezaji pale wanapoomba kuwekeza katika maeneo mbali mbali. Mwanzoni zote zilikuwa chini ya usimamizi wa TIC. Kwangu Mimi Ni Windows Za approaval ya inventives Kwa wawekezaji. Miradi yenyewe katika madirisha HAYA Kwa mwaka wana register sio ZAIDI ya 10. Kwa Hiyo kufanya appraisal ya miradi hii huitaji ZAIDI ya staff 2 Kwa miradi yote.
Sasa ona yaliyotokea:
1. Baada ya sheria ya EPZA kutungwa, badala ya kuiwekea desk officer pale pale TIC wao wakaunda chombo kipya NA magari NA majengo NA madreva NA ma secretary NA wafagiaji NA .... Wakaenda kukaa External.
2. Baadae wakatunga sheria PPP badala ya kutengeneza desk la PPP Hapo Hapo TIC wakakimbia kuingoa. Sasa WAKO buzzy NA kutafuta CEO ili aombe magari NA majengo NA secretary NA walinzi na ....

Sasa ona matokeo yake. Hizi branches zinazozaliwa NA TIC zote zinaduplicate hicho hicho anachofanya TIC. Eti WOTE wanatenga bajeti kwenda nje kufanya promotion. WOTE wanafungua one stop centers kutafutia wawekezaji vibali serikalini. WOTE wanajenga himaya ya kutoa incentives Kwa kuzuia wawekezaji wasivuke kwenda kwingine. WOTE wanafanya juu chini kufanya branding Kwa kugharamia roadshows nje NA kusafiri NA mawaziri Kwa lengo la kuvutia Uwekezaji.
Mwisho UNAJIULIZA iko wapi value ya duplication ya hizi overhead costs Kwa serikali kuhudumia utekelezaji wa sheria hizi wakati Kwa uhalisia wake zinatakiwa kutekelezwa NA desk officers wasiozidi 6 wakiwa chini ya CEO mmoja. Mbaya ZAIDI ikizitenganisha hizi sheria kiutekelezaji unazalisha Tatizo la baadhi ya miradi mizuri Kwa taifa kutokutekelezwa Kwa kukosa kukidhi viwango vya dirisha husika NA kuishia kukosa incentives.

Ningekuwa Mimi ningerudisha TIC ya zamani NA sheria zote hizi nikaziweka chini yake Kama units Za approvals ili promotion NA facilitation ya investment zote hizo iwe Ni shared resource.
Donda ndugu hili liko kote. Kila ukiona Watu wanaenda NA mapendekezo ya sheria mpya Dodoma basi ujue nyuma yake Watu wameshajiandaa kuwA ma CEOs Tena nyingi Eti wanazifanya presidential appointment wakati ki uhalisia zilitakiwa KUWA NA special desc officers tu. Dr. Kyaruzi kaandika toka mtandao mwingine
 
I hate people like you. hivi ni ukosefu wa shule au matatizo ya kisaikolojia??????
upload_2016-6-3_14-41-41.png
 
Back
Top Bottom