Ashura9
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 740
- 485
NHIF mnatukatisha watanzania tamaa kabisa, Yaani mnawatenga watanzania, wanaofanya kazi serikalini wanalipa asilimia 3% ya mshahara kuchangia na dependants 6, watu binafsi mnawaambia watoe sh 950,000 hivi kwa mkupuo na dependants 4 tu, hii si haki kwa maana watu wa kawaida wataipata wapi hiyo milioni moja, na kuchangia karibu laki kwa mwezi, ni wakati muafaka kuliangalia hili suala upya.
Na pia hata ukilipia hiyo milioni unaambiwa hutapata baadhi ya matibabu mpaka mwaka uishe sasa kuna maana gani ya kutoa hela yote hiyo halafu bado unatoa hela mfukoni kwa baadhi ya magonjwa/vipimo
Mimi nilidhani Bima ya Afya ingekuwa ndio mkombozi nchini kwa kila mtu, badala yake mnabagua watanzania, sasa huyu mtu binafsi anaepokea 200k kwa mwezi anasaidiwa na nani katika matibabu??
Pia suala lingine. Ruhusuni vijana wanao anza kazi ( wasio na familia) kuandikisha ndugu zao kwani wanachangia hela zao sio zenu! Nyie jalini idadi yenu (6) na mtu aruhusiwe kubadili mtu au watu ndani ya mwakammoja hata mtu 1 au wawili.
NHIF iwe kwa ajili ya wananchi wotw na sio watu wachache kama ilivyo sasa; hivi sasa ni kwa ajili ya wafanyakazi wa serikali zaidi, kwa hiyo basi ibadilishwe iwe kwa watu wote sawa, maana watu binafsi waliajiriwa na makampuni binafsi ndio wanaolipa kodi inayolipa mishahara ya serikali. Watu binafsi walete salary slip nao wachangie 3%
Zaidi ni kwamba Watanzania walio wengi hawaitambui NHIF kwa maana hawako serikalini
Soma zaidi hapa --->>>>Watanzania Wengi Hawaitambui ‘Bima Ya Afya’ Na Huduma Zake | Fikra Pevu