NHIF kusitisha mkataba wa huduma za Bima na SANITAS

Ng'azagala

JF-Expert Member
Jun 7, 2008
1,288
222
Wana forums, mimi kama mteja wa SANITAS nimesikitishwa sana na taarifa hizi za kusitishwa huduma za Bima ya afya. Sina hakika na matatizo yaliyojitokeza ila nadhani NHIF wanapaswa kutumia sana busara katika kufanya maamuzi yao wakijua wana athiri watu wengi sana waliokuwa wanapata huduma hapo SANITAS.

Hivi hayo matatizo yanayojitokeza hayawezi kuzungumzika na wateja wakaendelea kupata matibabu. kwanini kusiwe na fines badala ya kuzuia huduma? na ni vipi mbona bima nyingine wanaendelea kama kawaida? na ukichunguza nyingine ni kupitia mashirika mengine hapa hapa?

AGHAKAN Dar mpaka leo hawapokei bima ya afya sasa ukiongeza na SANITAS na wengine matokeo yake ni kwamba unakuwa na bima ambayo haina msaada mkubwa.

Nashauri NHIF waangalie/wapitie upya maamuzi hayo kwa kuangalia wateja wao zaidi, sioni kwa nini wanaongelea kujipanua wakati upande mwingine wanaendelea kupunguza watoa huduma wazuri. Niseme wazi, SANITAS wanahuduma bora hasa baada ya kuwa na mfumo wa ki electronic hivyo hakuna kero za kutafuta mafaili kama wakati natibiwa Muhimbili, Regency, TMJ nk. Nilidhani kuwa hata mamlaka za serikali wangeona hilo na kujaribu/kuhamasisha hospitali zingine waige.

SANITAS_NHIF.jpeg
SANITAS_NHIF.jpeg
 
Back
Top Bottom