Nguzo 5 imara za CHADEMA hizi hapa!

Nguzo 5 imara za CHADEMA hizi hapa!

mpk

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
3,115
Reaction score
3,864
Tunapoelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu (2015), tunaingia na chama kikuu, imara, makini kuliko muda wowote katika historia ya nchi hii. Sababu za chama hiki kuingia kikiwa na nguvu kiasi hiki ni tano na unaweza kuziita nguzo za chama.

1. Mwenyekiti na Katibu mkuu

Mtakumbuka kabla ya uchaguzi wa ndani wa chama kulikuwa na juhudi za kuwagombanisha toka kwa mahasimu wetu (walio ndani tunajua mengi) Mbinu hiyo iliposhindikana wakaja na mbinu ya kuwazuia kugombea, wakatumia ofisi ya msajiri na kelele za vyombo vyao vya habari. Kama kawida yao viongozi wetu walitulia na kuendeleza mpango wa uchaguzi na mkutano mkuu uliofana na ambao haukuwahi kufanyika na chama chochote katika ardhi ya Tanzania. Ushirikano wao na mealewano yao ni nguzo kuu ya chama.

2. Idara ya usalama ya chama:

Kwa yoyote anayejua hujuma za siasa za Tanzania atashangaa ni kwa jinsi gani chama hiki kimeweza kukwepa mishale ya ndani ya chama na nje ya chama. Ccm wametumia kila njia kuiua Chadema, kuanzia kupandikiza mamluki, kudhuru vingozi wakuu, kufanya kila njama kuona chama kinakufa. Wakati wote idara hii mahiri imenasa mipango yao yote, pamoja taarifa za idara kukiokoa chama na viongozi lakini pia wakati mwingine hutumika kama kete za kisiasa. (hapa kuna njama nyingi, ugaidi wa Rwakatale, SMS za Mwigulu, Mauaji ya Soweto, njama za kumdhuru Dr Slaa kwenye helkopita, Khalid Kagenzi, mpango wa mapinduzi ya uongozi wa chama nk nk nk.)

3.Wanasheria wa chama:

Mahasimu wetu wamejitahidi kuwabambikiza kesi vingozi, kuzia baadhi ya harakati zetu kisheria, kutengua wabunge wetu, kuhoji baadhi ya maamzi ya chama mahakani. Kinara wa sheria nchini Tundu Lissu na timu yake kama kina Prof Safari, Mabere Marando, Kibatala, Kimomogoro, Mbogolo, Mdee mara zote wameubuka washindi katika kesi hizi. Ukienda vyuo vikuu vingi wanavyuo wanasoma sheria kwa sasa role model wao ni wanasheria hawa na hasa Tundu Lissu.

4. Timu ya mipango:

Kama kuna kitu kinawasumbua mahasimu wetu ni jinsi mipango ya chama inavyokuwa ya kisasa, inayokwenda na wakati na isyotabilika. Wakiwa wanajipaga kuhujumu mpango unaendelea uantokea mpango mwingine wa hali ya juu, maadui wetu hulazimika kurudi kwenye drawing board kujipanga upya. M4C, mpango wa kanda, Chadema ni msingi, FTP 200, na sasa timu za kampeini ni baadhi ya mipango hiyo. Wakati wanajipanga kuhujumu FTP 200, sisi tuko mbele yao maana tumeanza timu za kampeini.

5. CHASO

Hii ni jumuhiya ya wanafuzi wanachadema vyuo vikuu, hawa kwa asilimia kubwa ndiyo wagombea nafasi mbali mbali mwaka huu, wameiva kifalsafa na kiitikadi. Wamenieneza Chadema kwa nguvu zao zote, si waoga na sasa wameanza mpango wa kusambaa nchi nzima kueneza Chadema kitaaluma. Siku moja Shonza aliwahi kuhoji humu eti CHASO ya akina ZZK na Regia (R I P) Mtema iko wapi. Alishindwa kujua hawa ndiyo watumishi wa leo wako ofisini na kadi za Chadema mifukoni! Ameshindwa kujua ndiyo wanaotangaza nia ya kugombea ubunge kiasi kwamba kila jimbo la Tanzania bara lina watia nia zaidi ya watano.
 
Mkuu yapo mambo mawili makubwa sana umesahau,

jambo la kwanza la ukabila ,

pili suala la ukanda yote haya ni nguzo za chadema.
 
Hakika maneno yako Kamanda yana upako!!!Ubarikiwe kwa mada maridhawa,songa mbele Chadema adui yupo karibu SANA!!!!
 
Mkuu yapo mambo mawili makubwa sana umesahau,

jambo la kwanza la ukabila ,

pili suala la ukanda yote haya ni nguzo za chadema.

Ningeyaweka zingekuwa nguzo 7, yapo mengi lakini hapa nilikuwa nasema nguzo kuu tano.
 
Mkuu yapo mambo mawili makubwa sana umesahau,

jambo la kwanza la ukabila ,

pili suala la ukanda yote haya ni nguzo za chadema.

akina baba tunapoongea akina mama mnatakiwa muwe kimya subiri post za vigodoro vya ccm na mwanae mpendwa act ndio uchangie sawa mama ?
haya nenda jikoni ukapike saa saba tule
 
Kila lililojema huwa limebarikiwa na Bwana !! Endeleeni kwenda mbele kwa kubuni nia yenu na yetu ifanane ili watu watanzania tujikwamue na uonevu , umasikini na unysng'anyi Wa lasiliamali zetu kwa vigogo wanaoihujumu nchi yetu Tukufu iliyobarikiwa , jitahidini walau tupate kupumua na democracy tuipate !!
 
I like this!
 
CCM na Mchepuko wake wanapatwa na presha

Naona mmewe kakatuma kamchepuko kake eti kaje kuomba urafiki na jeshi la Ukawa kwa kuandika barua,CCM wamebakiwa pigo moja la mwisho wakate roho ili litajiri July
 
Hiyo number One tunaijua sana, ndiyo muhimili wenu mkuu. Tulijaribu mapema sana kumpandikiza kijana wetu kwenye nafasi ya Uwenyekiti lakini mkatuzima mapema mno kwa kigezo eti muda wake utafika na ataongoza chama hicho miaka ijayo, pia hoja nyingine mkasema ataweka mpasuko kipindi hicho chama kinakuwa kwa kasi.

Ni kweli hiyo nguzo ndiyo msingi Imara wa chama chenu, tumejaribu mbinu nyingi - But this combination is very strong. (nimeongea umombo kusisitiza kauli yangu )
 
Mkuu yapo mambo mawili makubwa sana umesahau,

jambo la kwanza la ukabila ,

pili suala la ukanda yote haya ni nguzo za chadema.

Fikra za watu wenye upeo mdogo na wanaofikiria posho zaidi kuliko ukweli halisi.Nafikiri ni vizuri ukajipanga kabla hujachangia mada yoyote.
 
Hiyo number One tunaijua sana, ndiyo muhimili wenu mkuu. Tulijaribu mapema sana kumpandikiza kijana wetu kwenye nafasi ya Uwenyekiti lakini mkatuzima mapema mno kwa kigezo eti muda wake utafika na ataongoza chama hicho miaka ijayo, pia hoja nyingine mkasema ataweka mpasuko kipindi hicho chama kinakuwa kwa kasi.

Ni kweli hiyo nguzo ndiyo msingi Imara wa chama chenu, tumejaribu mbinu nyingi - But this combination is very strong. (nimeongea umombo kusisitiza kauli yangu )

Hii ni combination ya mtu mmoja msomi na mwadilifu na tajiri mwadilifu, hakuna wa kununua hapo.
 
Mkuu yapo mambo mawili makubwa sana umesahau,

jambo la kwanza la ukabila ,

pili suala la ukanda yote haya ni nguzo za chadema.

kama ni ukabila huu ni wimbo ambao tumeuzoea,lakini pia ebu tuambie ni ukabila katika mkoa gani maana cdm kiko Tanzania nzima.kina uongozi katika ngazi zote tena wa kuchaguliwa sio kuteuliwa.

huko ACT juzi gari la kampeni lilipata ajali huko tabora cha kushangaza dereva wa gari lile ni mtu aliyekuja kutambulika kama mdogo wake na zitto kabwe

mwenyekiti wenu ACT ni msingida,think tanker wenu ni msingida wajumbe wengi halmashauri ni waha je huu tuuite ni u-nini?:A S-rap:
 
Mkuu yapo mambo mawili makubwa sana umesahau,

jambo la kwanza la ukabila ,

pili suala la ukanda yote haya ni nguzo za chadema.

Dada Mwajumanne mbona hizo nyimbo za zamani zimeshachuja,nyimbo ni cdm ni chama cha magaidi baada ya kukutwa na zana za kivita ambavyo ni MANATI,MABUTI,VISU,KOFIA na TSHIRTS,teh teh teh teh hamna rangi mtaacha ona nyie magamba.
 
Mkuu yapo mambo mawili makubwa sana umesahau,

jambo la kwanza la ukabila ,

pili suala la ukanda yote haya ni nguzo za chadema.

Duuuh Dada mbona huendani na kasi ya mabadiko? watu walishahama kutoka analogy tupo digital , pole sana hizo kauli zishakua mfu.
 
chadema ni chama kikuu cha upinzani na kina nguvu sana mambo mengine ni porojo ti
 
Dolla imepanda sana aisee daah!! Wakuu wa nchi wamekaa tu kimya, walaji wa chini tunaumia sana
 
Chadema imewezesha wananchi kujiamini na kukataa kukandamizwa na mkoloni mweusi, mwananchi wa leo hawezwi burutwa na kiongozi yeyote kwa ujinga
 
Back
Top Bottom