DUNIANGUMU JR
Member
- Apr 20, 2011
- 43
- 14
SERIKALI NA NGUVU YA VYOMBO VYA DOLA-POLISI,JESHI, USALAMA WA TAIFA NI KUWAPA SUGU WANANCHI.
Serikali yoyote inayotumia vyombo vya dola kunyamazisha watu kwa nguvu mwisho wa serikali hizo huishia katika machafuko ya vita wenyewe kwa wenyewe au watu huchukuwa utawala kwa nguvu baada ya vyombo vya dola kushindwa nguvu na nguvu ya wananchi.
UNAFAHAMU ni kitu gani nimejifunza na kilichonishangaza kuliko vyote maishani? Ni kushindwa kwa matumizi ya NGUVU kukupatia kitu chochote endelevu ambacho ni kizuri. Nimegundua kwamba, mwisho wa yote, hata bunduki,mabomu, makoleo ya kungoa meno na fizi husalimu amri kwa ukweli. NI lazima watawala wajue kwa Hakika, ukweli na Haki ni zaidi ya Risasi, mabomu, virungu na makoleo ya kutolea meno.
Umuhimu wa serikali kusikiliza kero za wananchi na kuzifanyia kazi kwa usikivu ndiyo njia pekee ya kuleta upendo wa jamii katika utawala wowote, ni nadra sana nguvu ya vyombo vya usalama kuleta amani na utulivu au kulazimishia wananchi kile wasichoamini, wananchi wale watakuwa sugu na mabomu, kungolewa meno, kupigwa Risasi ndiyo wakati huo wananchi watachukuwa nchi yao na nyie watawala mtakuwa wananchi.