Nguvu ya sauti ya mwanadamu na maisha yake

Lucky Star

JF-Expert Member
Jul 16, 2017
1,109
2,000
Amani iwe kwenu wakuu. Poleni na majukumu ya kifamilia na yale ya kulitumikia taifa.

Napenda kuzungumzia maisha ya mwanadamu yalivyo,SAUTI yake na uhusiano wa sauti yake kwa familia na jamii zetu.

Binadamu huzaliwa akiwa hana uwezo wowote zaidi ya utambuzi wa mambo madogo madogo kama vile kumjua mama yake,kulia pale anapokuwa na shida ili asaidiwe na mengine machache. Aidha SAUTI yake huwa nyembamba sana. Kadri anavyokuwa huanza kupata mabadiliko mbalimbali,na hata kufika hatua ya kuanza kuomba vitu kwa kutaja.

SAUTI yake huendelea kukomaa na kuwa inayosikika tayari na watu kuanza kutamani kusikia maneno yake. Baadaya yeye kujitambua huanza kujenga ushawishi na SAUTI yake kuzidi kushamiri na hata baadhi kuikariri. Anapokomaa/pevuka......baadhi huipenda SAUTI hiyo na wengine huichukia.

Binadamu huyu baadaye hufikia hatua ya kukabidhiwa majukumu ya utu uzima baada ya kukomaa na kuaminiwa. Hapa ndipo athari za SAUTI yake huanza kuonekana,kama ni chanya au hasi.
Matumizi ya SAUTI yake kubwa ya utu uzima huweza aidha kuwaogopesha na hata kuwanyamazisha wote waliopo chini yake,lakini pia wengine hutafuta njia za aidha kumzoea,kushirikiana naye au kumkwepa.

Lakini binadamu huyu ana mwisho. Mwisho huu huja pale anapokuwa amezeeka na kuhitaji msaada au huruma ya waliomzunguka. Huu ni wakati ambao SAUTI yake ni kubwa lakini haiogopeshi tena. Na hapa ndipo watu huwa huru kumjadili kwa hisia tofauti bila woga wowote. Na hapa familia ukoo au jamii huanza kutafuta uwezekano wa kuwa chini ya KIONGOZI MPYA bila kujali umri wake na uwezo waSAUTI yake kulinganisha na mtangulizi wake. Waluomzunguka awali nao bila woga huanza kutafuta njia ya kuizoea tena SAUTI ya kiongozi mpya.

Aliyeandaa mwisho wake mzuri husindikizwa kwa furaha na kupata maombezi ya kutakiwa HERI huko alikopumzika.Aliyeandaa mwisho wake mbaya huiacha familia yake katika sintofahamu.
............................
........................................
Najaribu tu kuwaza ukubwa wa SAUTI za watawala wetu na tafakari ya mwisho wao?

Tutakiane kila la heri katika kudumisha aUMOJA,UDUGU NA MAHUSIANO MEMA BILA KUJALI TOFAUTI ZETU ZA KIDINI,SIASA,KABILA WALA KIKANDA.


Muwe na siku njema.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom