Nguvu ya saikolojia

Hata hospital wagonjwa wengi matatizo yao yameanzia vichwani..mwisho wa siku namna unavyowaza inaathiri mpaka mwili..lakini kimsingi hawaumwi kihivyo..japo wapo wagonjwa serious kwahiyo mind na body ndio kila kitu,vina uhusiano mkubwa sana!
 
Nakumbuka wakati wa utoto nilipokuwa sitaki kwenda shule basi usiku najifanya naumwa najilaza na kuvuta hisia za kujihisi naumwa,basi baada ya muda mwili unakuwa wamoto na ukinitizama unaona kabisa naumwa na panadol napewa nameza.

Ukiamini jambo kwa dhati linakuwa nyinyi watu wa dini mnaiita imani
Na hapo ndio utagundua there is no god at all
 
Wachawi na wasiojulikana hawataelewa chochote kabisa.

Hata hii comment yangu hawataielewa kamwe.
 
Aina hii ya maumivu ambayo hayaelezeki kitabibu bali kisaikolojia yanatokana na tatizo lijulikanalo SOMATOFORM DISORDER.
 
Huwa nasikia hata mtu kabla hajapata majibu ya vipimo vya HIV nakuonekana +huwa na furaha na afya tele ila tu akipima nakukutwa + akapewa majibu baaasi ndio mwisho wake na afya huanza kudorola yaani.
 
Asante kwa mada nzuri yenye kufikirisha, nadhani kichwa cha habari hii kilipaswa kuwa 'Nguvu ya Akili'
 
Sawia kabisa, hata mi nishawahi kuwa mhanga wa hili. Kuna kipindi niliugua msongo wa mawazo na ukazidi nikawa mtu wa kuwaza kuwa na huzuni na hofu masaa yote, matokeo yake nlipata physical symptoms- kuna kipindi nilikuwa naugua tumbo na kuharisha juu, kuna kipindi nilikuwa naugua meno.
Kama ni tumbo linauma hasa na kuharisha, nashukuru Mungu nilikuwa mwepesi wa kutambua ni kutokana na msongo ndo maana nimeugua namna hiyo maana tayari nilikuwa nauelewa na matokeo ya stress katika mwili hivyo sikunywa dawa bali nilijaribu kujisahaulisha na kufanya kama ninafuraha basi napona naacha kuharisha ila yakirudi tu kichwani kazi ipo au yakiondoka maswahiba ya tumbo yanakuja meno, meno ndo ilikuwa kiboko nilikuwa naskia maumivu makali haswa nashindwa hata kufanya kazi yoyote nalala tu, akili ikitulia nikawa na furaha meno yanapona ila mawazo yakirudi yanaanza tena. Bahati nzuri nikaja nikapona msongo wa mawazo nikajifunza kuicontrol akili na kuwa na furaha, nikapona sikupata tena hayo maumivu ya mwili
 
Fact sana somo la Saikolojia ni pana sana ukilifatilia kwa undani unatokea kwenye ule unaousikiaga unaitwa ulimwengu wa Roho uko ndo miujiza inakotokaga
 
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…