Nguvu ya kufunga

Nguvu ya kufunga

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,780
Reaction score
8,155
Kufunga ni mbinu ambayobimekua ikitumika tangu zamani mbinu hii imekuwa ikitumika katika tamaduni mbalimbali duniani kama njia ya kujisafisha kiroho, kimwili na kiakili. Haijalishi wewe ni mtu wa imani gani haijalishinwew ni emtu wa imani ipi, kufunga hutoa nafasi ya ndani ya mtu kujitafakari, kutuliza akili, na kuungana na nguvu ya juu au asili ya maisha. Ni utaratibu wa kuondoa usumbufu wa kimwili ili roho ipate nafasi ya kung’aa.

Ikiwa umekuwa ukijiuliza maswali mazito maishani kama: “Ninapaswa kufanya nini?”, “Kwa nini naona kama nimepotea?”, “Mbona ndoto zangu hazijifafanui?”, “Ninapitia kipindi kigumu lakini sijui nikimbilie wapi?” basi kufunga ni moja ya njia kubwa sana ya kupokea mwanga ujumbe kutokabilimwangu wa ndanj ivyo. Kupitia mfungo, unaweza kuunganisha nafsi yako, roho yako, na mwili wako ili kupata jibu moja kamili kutoka ndani yako mwenyewe.

Kupitia mfungo ama kufunga basi basi tunaweza kupata hali ya utulivu ndani, hivyo kufunga humfanya mtu kuwa huru kiakili na kihisia. Husaidia mtu kupunguza kelele za nje na kuingia ndani ya nafsi yake.

Kufunga husaidi kuimarisha maamuzi ya mtu na kuleta uwiano kati ya mwili, akili na roho.
Kufungua mlango wa kusikia ndaniHapo ndipo majibu ya maswali yako ya ndani huanza kujionyesha kwa njia ya ndoto, sauti ya ndani, au ishara.

Mfungo wa kutafakari (Meditation fast): Kupunguza chakula na kutumia muda mwingi katika kutafakari.
Mfungo wa ukimya (Silent fast): Kutozungumza na kujitenga na mitandao na kelele ili kupata mwanga wa ndani.

Mfungo wa asili (Raw food fast): Kula vyakula vya asili pekee au maji ili kusafisha mwili na kuamsha roho.
Mfungo wa kiakili (Mental fast): Kuepuka fikra hasi, mazungumzo yasiyojenga na kutumia muda katika kujisemea mema na kujenga ndoto.

Kufunga husaidia kuvunja vunja minyororo ya ndani Husaidia mtu kuachana na utegemezi wa vitu au hisia zinazozuia maendeleo.
Kupitia kufunga tunaweza kuongeza nguvu ya kiakili na (intuition): Mfungo hufungua mlango wa hisia za ndani na ufahamu wa hali ya juu.

Huvutia nguvu za asili: Kama vile nguvu ya mwezi, jua, hewa safi na maji—kufunga hufanya mtu kuwa mwepesi na wa kiunganisho na mazingira.

Huunganisha nafsi, roho na mwili kwa usawa mmoja: Hii huleta amani, usawaziko, na mwanga wa kipekee kutoka ndani.

Kufunga husaidia
Kusikia sauti ya ndani vizuri zaidi
Kufungua uwezo wa kuota na kuona ishara
Kupata msukumo mpya wa maisha
Kupona kiroho, kihisia na hata kimwili
Kujenga muunganiko kati ya mtu na ulimwengu wa roho/asili
Kupokea majibu ya maswali ambayo yamekuwa yakikusumbua kwa muda mrefu

Kuna aina nne za mifungo ambayo ni pamoja na mfungo wa
Siku 3 – Mabadiliko ya ghafla: Ni muda wa kusafisha mwili na kuamsha akili ya kiroho haraka. Huashiria mwanzo mpya.

Siku 7 – Mzunguko wa ukamilifu: Katika tamaduni nyingi, namba 7 ni ya ukamilifu. Husaidia kusafisha kabisa mzunguko wa ndani.

Siku 21 – Kuvunja mivuto ya zamani: Hii ni namba ya mabadiliko ya tabia, kufuta sumu za zamani na kupokea mwanga mpya.

Siku 40 – Nguvu ya mageuzi: Inawakilisha ukomavu wa kiroho. Mtu anapofunga kwa siku 40 hupitia mabadiliko ya kudumu na hupokea maono mapya ya maisha.

Katika mila nyingi za kale , watu walifunga kabla ya kupokea maono, kabla ya kuingia kwenye ibada au kupokea wajibu mkubwa wa maisha. Hii inaonyesha kuwa mfungo ni njia ya kuandaa roho kwa safari kubwa au jukumu maalum.

Kufunga si suala la dini tu, bali ni zawadi ya ulimwengu kwa mwanadamu yeyote anayetaka kusafiri ndani yake, kujifahamu, kusikia zaidi, na kuungana na nguvu ya juu au asili. Ni mlango wa kutuliza akili, kuamsha roho, na kujenga maono mapya. Haijalishi unapotoka au unaamini nini, mfungo unakupa nafasi ya kubeba tochi na kuangaza giza la ndani yako mwenyewe.

Wakati mwingine majibu ya maisha yako hayapo nje,yako bali yako ndani yako. Kufunga ni funguo ya kuyafungua.
 
Mkuu tunalifanikishaje hili hatua kwa hatua adi kufikia mafanikio ya kuwianisha roho, nafsi na mwili ili niwe najisikiliza zaidi kutokea ndani yangu na sio nje?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom