Nguvu ya Edward Lowassa, Sitta, Membe na Mwandosya inatoka wapi na kwa nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nguvu ya Edward Lowassa, Sitta, Membe na Mwandosya inatoka wapi na kwa nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbavu za Mbwa, Jul 22, 2011.

 1. M

  Mbavu za Mbwa JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  Ni wazi kabisa kuwa CCM ina mpasuko mkubwa, mpasuko ambao unatishia mustakabali wa uhai wake. Na si siri kwamba mpasuko huo unatokana na makada waandamizi katika CCM kuelekeza macho yao katika uchaguzi mkuu wa 2015 wa nani awe mgombea urais kupitia CCM.

  Macho yote ya watanzania yanaangalia mpambano huo kwa kuwa bila shaka Chama kikuu cha upinzani nchini, CDM kwa asilimia kubwa kitamsimamisha Dr Slaa(labda itokee mipango mingine ya Mungu) ambaye ameonekana ni mtaji mkubwa sana wa chama hicho, hivyo sitegemei kama atakuwa na mpinzani katika mchakato ndani ya chama chake.

  Nimeanza kuandika kitabu kinachohusu mchakato wa kuelekea ikulu kupitia CCM. Pamoja na mengine mengi, nitazungumzia agenda ya kujivua gamba. Katika hili wapo wanaosema kuwa Edward Lowassa ana nguvu kubwa sana katika vikao vya maamuzi vya chama chake, CCM. Nawaletea orodha ya wajumbe wa vikao hivyo ili mnisaidie nani na nani wapo upande wa Edward Lowassa na wepi wapo upande wa mahasimu wake kisiasa ndani ya chama chake. Naombeni michango yenu iwe ni katika kujenga na si kukatishana tamaa.

  WAJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM
  1. Jakaya Mrisho KIKWETE
  2. Pius MSEKWA
  3. Amani Abeid Amani KARUME
  4. Wilson MUKAMA
  5. John CHILIGATI
  6. Vuai Ali VUAI
  7. Ali Mohamed SHEIN
  8. Mizengo Kayanza PINDA
  9. Ali Hassan MWINYI
  10.Benjamin William MKAPA
  11.Salmin AMOUR
  12.John MALECELA
  13.Nape NNAUYE
  14.Mwigulu MCHEMBA
  15.January MAKAMBA
  16.Asha Abdallah JUMA
  17.Hussein Ali MWINYI
  18.Maua Abeid DAFTARI
  19. Samia Suluhu HASSAN
  20. Omar Yussuf MZEE
  21. Makame Mnyaa MBARAWA
  22. Mohammed Seif KHATIB
  23. Shamsi Vuai NAHODHA
  24. Abdulrahaman KINANA
  25. Zakiah Hamdani MEGHJI
  26. Abdallah Omar KIGODA
  27. Pindi Hazara CHANA
  28. Steven Masatu WASSIRA
  29. Constansia BUHIE
  30.William LUKUVI

  WAJUMBE WA SEKRETARIAT YA CCM
  Wengine wapo katika CC

  • Makatibu Wakuu wa Jumuiya za Wananchi (Zinazoongozwa na CCM)
   - Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
   - Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM
   - Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi
  [FONT=&quot][/FONT][FONT=&quot][/FONT][FONT=&quot][/FONT][FONT=&quot][/FONT][FONT=&quot][/FONT][FONT=&quot]

  NB:
  (1)NISAIDIENI NIWEZE KUKAMILISHA KAZI YA KUANDIKA KITABU CHANGU KABLA YA 2015
  (2)MAJINA YA WA-NEC NIMESHINDWA KUYAAWEKA KWA KUWA NI MENGI MNO, HIVYO KUHOFU KUWACHOSHA WACHANGIAJI
  [/FONT]

  [FONT=&quot] [/FONT]
   
 2. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mbavu,
  Hivi yawezekana CCM wakawa Mabwege kiasi hicho wanachodhaniwa na kumsimamisha Lowasa agombee Uraisi 2015? Na hilo likitokea na sisi Watanzania Wapigakura tuitweje tutakapompa Lowasa kura zetu? Ashakum si matusi, sidhani kama kutakuwa na jina safi linalotufaa.
  Inashangaza kuwa bado kuna wanaoendelea kumfagilia Lowasa pamoja na Machafu yake yote yaliyopo Hadharani. Watu hupishana kwa Vipawa na Uwezo, lakini sidhani kama alivyonavyo Lowasa havipatikani kwa Watanzania wengine. Punguzeni Tuwi mtie Mchele, huyo jamaa mkimpa Urais hata Hewa atatuuzia tushindwe kupumua ana Tamaa iliyovuka mipaka. Rafiki yake alifanya makosa na kumpa Uwaziri mkuu eti sasa kuwe na Ndoto ya kumpa Urais, Ole wenu!!
   
 3. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  He the most clean,
  Most brave,
  Most intelligent,
  Tactical,
  Richest,
  And above all the meanest.
  that's why CCM will fall for him.
   
 4. zeus

  zeus JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli kama usemavyo watu hupishana uwezo ndio maana wako ukawa finyu. angalia heading ya post yako na ulichoandika humo ndani? vinaendana kweli?hii nchi ya demokrasia kama lowassa hakufai usimpe kura yako wengine tunaoona anafaa tutampa kura zetu na ole iwe kwetu na watoto wetu. kumbe unatambua kuwa kuna ana wasifu mzuri alionao ambao pia unaweza kupatikana kwa wengine? kama nafsi yako inamchukia lowasa basi baki hivyo lakini uheshimu wanaompenda sio kuendesha kampeni za chuki binafsi zisizo na mshiko.
   
 5. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mark Mwandosya for presidency under CCM ticket, hana papara, ni mchapakazi, hana makundi, ukimchafua hachafuki. Ni msomi mwenye upeo na ni mvumilivu wa personality clashes
   
 6. M

  Mbavu za Mbwa JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  Nashukuru kwa michango yenu. Wanajamvi, kama mmeisoma vizuri thread yangu ni kuwa haina lengo la kuleta ushabiki wa kisiasa wa nani anafaa na nani hafai, la hasha. Lengo langu hasa ni kufahamu nguvu aliyonayo kila anayesemwa(miongoni mwa niliowataja) katika vikao vikuu vya maamuzi ndani ya chama na si nguvu aliyonayo miongoni mwa wapiga kura. Ni matumaini jukwaa hili la siasa lina wachambuzi wakubwa wa siasa.

  NISAIDIENI KTK HILI.
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Usishangae wakamuweka na akawa rais,,,,,kashfa hizo zitazimwa kwa kupitia hawahawa waandishi wetu wa habari...........
   
Loading...