Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
Huyo ni Francesco Totti moja kati ya washambuliaji bora sana wa Kiitaliano kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka na kila siku atakuwa katika mioyo ya mashabiki wa As Roma.
Katika mchezo ambao As Roma waliifunga Genoa mabao 3 kwa 2, machozi na simanzi yalionekana kutawala uwanjani wakati wa kumuaga Francesco Totti.
Totti ambaye amewahi kushinda kombe la dunia mwaka 2006 aliwahi pia kushinda kikombe cha Serie A na katika michezo 783 aliyoicheza amefunga jumla ya mabao 307.
Msimu huu Totti ameichezea As Roma michezo 27 lakini karibia yote alikuwa akitokea benchi na kuisaidia Roma kumaliza nafasi ya pili wakiwa na alama nne nyuma ya mabingwa Juventus.
Tayari klabu hiyo ya Italia imeamua kumpa nafasi mpya Totti ambapo ataanza kuwa mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo kazi ambayo anaianza rasmi siku ya Jumatatu.
Shaffih Dauda