NG'os zinazoshughulikia matatizo ya watoto zikowapi?

NG'os zinazoshughulikia matatizo ya watoto zikowapi?

KakaKiiza

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2010
Posts
11,902
Reaction score
9,323
Nikiwa napita katika mitaa ya Jiji la Dar es Salaam maeneo ya SERENA HOTEL Nilikutana na watoto wawili wakiwa wamelala katika lango lakuingilia katika Hoteli hii kubwa ya SERENA HOTEL..

Kwa haraka nilitambua kuwa siyo wamelala kwa raha la asha! Nikwamba walikuwa wamechoka na zaidi hawajala kitu!......Lakini nikakumbuka baadhi ya mashirika ya kusaidia mtoto yapo mengi! Je yanamsaidia mtoto yupi?au niwatoto waliopo mifukoni mwao?

Nikakumbuka kuna siku nilipoenda ofisi ya Makamu wa Rais kulikuwa na kitengo kinashughulikia kusajili Mashirika yasiyo ya kiserikali mashirika ya kuaidia watoto yalikuwa zaidi ya 100!! Ya nje yalikuwa zaidi 58 nchi nzima hivyo unaweza kuona kuwa yote haya mashirika yapo kwa mipango yao binafsi!

Nilienda Rwanda Kigali mwaka jana Mashirika ya kumsaidia mtoto lazima yamsaidie mtoto na lazima kila shirika liwe na mfanyakazi wa Serikali.Hapa ni tofauti sana!

Tazama hapa hawa watoto walivyolala na na jua linawachoma Tunaomba wanaohusika fuatilieni haya mashirika.
 

Attachments

  • 1391673584076.jpg
    1391673584076.jpg
    69.3 KB · Views: 99
  • 1391673621629.jpg
    1391673621629.jpg
    65.5 KB · Views: 90
ni wajibu wa serikali sio non government organisation!!! wasikimbie majukumu yao kama watawala
 
ni wajibu wa serikali sio non government organisation!!! wasikimbie majukumu yao kama watawala
Sasa hizo Non Government kazi yao nini?? na zinapata grand kubwa kutoka kwa wafadhili, kwa ajili ya kusaidia watoto wa Tanzania!. Hata kama serikali inahusika aslimia mia,hila na mashirika ni wajibu wao!ndiyo maana haya mashirika yapo kwa ajili ya kusaidia Serikali katika nyanja mbali mbali!.
 
Watanzania tuna tatizo la kuangalia wajibu wa wengine na kusahau wa kwetu. Mfano mtoa mada hajasema yeye amewasaidiaje baada ya kuwaoona hapo!!!! Au amewavizia akapiga picha na kuleta lawama zake kwa wengine. Tafakari Chukua Hatua
 
Back
Top Bottom