Ng'ombe azaa ndama mwenye kichwa cha binadamu

Ng'ombe azaa ndama mwenye kichwa cha binadamu

Habari kutoka Halmashauri mpya ya Busokelo Wlayani Rungwe zimenifikia jana, kwamba katika Kijiji cha Mbigili hapo juzi ng'ombe mmoja aliyekuwa na mimba amejikuta akizaa ndama mwenye kichwa cha binadamu. Ng'ombe huyo alikuwa anaendelea kuzaa kwa kutanguliza miguu ya ndama, lakini ghafla akashindwa kuendelea na kukaa chini. Akaishiwa nguvu na kulegea kabisa. Waliokuwapo jirani wakataka kumsaidia, lakini kichwa cha ndama kiligoma kutoka hadi walipolazimisha kutoa kichwa, na kushitukia wanaonana na kichwa cha mtu kabisa. Ng'ombe mzazi hakuendelea kuishi, akafariki muda mfupi baadaye.

haijajulikana bado kwa kina ni nini mazingira yaliyopelekea jambo hilo kutokea. Wenzetu walioko Busokelo watatufaa kutuletea naelezo zaidi. lakini labda kwa sababu ambazo wengine wanajiuliza uhusiano, Malkia wa mfalme wa eneo hilo anayejulikana kwa jina la Chief Kabakuli Mwaiswelo alifariki dunia siku hiyohiyo na makazi yake yanapakana na mmiliki wa ng'ombe huyo. Jambo linaloashiria kwamba huenda ni tukio lenye mizizi ya kimila. Mungu aiweke roho ya marehemu Malkia mahali pema peponi.

Huyo ng'ombe atakuwa alibakwa na binadamu
 
Hivi nyny mnoomba muwekewe picha hamuogopi kuona ng'ombe mwenye kichwa cha binadam? Ama kweli dunia imekwisha
 
Haiwezekani bin adam ku conjugate na mow, namba za cromosomes hazilingani, hili ni eneo jipya la utafiti.....
zamani mmi niliaminishwa kuwa albinos hawafi ila wanapojigundua wamekaribia kufa hupotea,mpaka hivi karibuni matukio ya kukatwa viungo ndugu zetu ndio nikashitua inawezekana waasisi wa msemo huo wa kuwa albino hawafi ndio hao hao wanaojihusisha na biashara hiyo, hivyo na hili naweza kuaminishwa kwa sasa lakini baadae tukaja jua chanzo.
 
Back
Top Bottom