Ng'ombe Avishwa Kofia ya CMM


EMT

EMT

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Messages
14,487
Likes
1,014
Points
280
EMT

EMT

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2010
14,487 1,014 280
Kama mnakumbuka wakati wa kampeni kuna vijana wawili walikuwa wanatafutwa na polisi kwa tuhuma za kumfalisha mbwa jezi ya CCM. Pichani ni wanachama na wapenzi wa vyama vya CCM na CUF wakiwa katika harakati za kusherehekea ushindi wa CCM huko Zanzibar huku wakiwa wamemvalisha ng'ombe kofia ya CCM. Sasa sijui hawa nao watatafutwa na polisi?
View attachment 16134
 
Madela Wa- Madilu

Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2007
Messages
3,073
Likes
56
Points
135
Madela Wa- Madilu

Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Joined Mar 24, 2007
3,073 56 135
Utabiri toka mezani kwa Mtabiri maarufu wa Yale Yajayo; Shemazi Yohana.

Ng'ombe ni mnyama mkubwa mwenye misuli ya nguvu iifayo kwa minofu, hana meno na siku zote kabla hajawa kitoeo hutumia nguvu za misuli yake kufanya kazi (Serikali ya Zanzibar).


Kofia(CCM) kichwani mwa Ngo'mbe, Bendera ndogo Nirani na Bendera kubwa Nunduni ni dalili kwamba ng'ombe kapata mmiliki mpya mwenye kushika hatamu na mamlaka ya chochote kitakachotokea kwa ng'ombe, mmiliki aliye na umbo lenye kutia mashaka.


Pale kwenye nundu kuna bendela ya CUF kwa maana ya CUF kukubali kuwa sehemu ya kofia,CCM, kwa faida nono isyofika miguuni( waZanzibar).

Nani kwenuasiyependa utamu wa nyama ya nundu ya ng'ombe????


Kwenye Nira ya Ng'ombe kuna Bendera ndogo ya CUF kuashiria kwamba Mtu au watu wachache wa CUF watakuwa na sauti juu ya mwelekeo wa Ng'ombe lakini mpaka kofia akubali


Kofia(CCM) anakaa katikati ya pembe mbili Polisi na Jeshi lakini pembe zimekuwa fupi kwa sababu Wanajeshi na Polisi wengi wamechoshwa na Amri kigeugeu za kofia.Atatawala kwa maumivu ya ujinga wao hadi uovu wake utimie.


Watamchinja ng'ombe kwa tamaa, watageukiana wao kwa wao na kukabana makoo hadi kuleta mauti, wengi watakimbia na kutawanyika pande zote nne za dunia.

Mahali pao atakuja mwenye amri kuu aliyewatia minyororo ya utumwa wakaikata na kumkatilia mbali. Atatawala kupitia migongoni mwao kwa minyororo mipya laini kama sufi.Kwa miroroyake mipya atawatia katika mzigo mkuu wa utumwa mkuu kuliko ule wa mwanzo.
 
The Son of Man

The Son of Man

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2010
Messages
12,556
Likes
2,368
Points
280
The Son of Man

The Son of Man

JF-Expert Member
Joined Feb 9, 2010
12,556 2,368 280
Huku ni zenji ila sijaipenda manake haireflect chochote cha busara.
 
Madela Wa- Madilu

Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2007
Messages
3,073
Likes
56
Points
135
Madela Wa- Madilu

Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Joined Mar 24, 2007
3,073 56 135
Huku ni zenji ila sijaipenda manake haireflect chochote cha busara.
Ni Utabiri unaukubali jinsi ulivyo au unaukataa si suala la kuupenda au kutoupennda.
 

Forum statistics

Threads 1,236,898
Members 475,327
Posts 29,271,575