Kuna habari ambazo hazijathibitishwa ambazo zinasema kwamba 'Mwekezaji wa Kimarekani" ameamuru ng'ombe wauawe na Land Cruiser huko Sengerema hatima yake ndiyo hao ng'ombe 65 kuuawawa. Kama kuna yeyote ambaye ana habari hizi azimwage hapa ukumbini.

Hapana ilistahili kuwekwa kwenye michezo. Wewe huoni habari ya mwekezaji aliyeingia nchini kwa mabadiliko yaliyofanywa na wanasiasa na si ajabu hana chochote cha kuwekeza bali amekuja na briefcase yake na akiondoka nchini ataondoka kama milionea au hata bilionea kuwa na kiburi cha kuamrisha dreva awagonge ng'ombe wa Watanzania kama ni siasa?
Habari hii imeandikwa katika gazeti la Mwananchi kama habari mpya, sijui kama ina ukweli kiasi gani, nilitegemea watakuwa wameshapata habari za kutosha kuhusu kilichojiri katika maujai hayo ya ng'ombe (kama ni kweli) lakini mpaka sasa hivi bado habari hiyo inaonyeshwa kama habari mpya na hakuna chochote kilichoongezwa zaidi ya "Mwekezaji Mmarekani aamuru ng'ombe wauwawe kwa Land Cruiser" sijui kama waliokufa ni hao 65, zaidi au pungufu. Kama unataka ihamishwe na kupelekwa kwenye michezo unaweza kuwaomba MODS wafanye hivyo.