Ng'enda: Sikuzaliwa kuwa katibu CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ng'enda: Sikuzaliwa kuwa katibu CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 26, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]
  [/FONT]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Saturday, 26 November 2011 08:50

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Hussein Issa

  SIKU moja baada ya Halmashauri Kuu ya CCM kumvua madaraka aliyekuwa katibu wa chama hicho mkoani Dar es Salaam, Kilumbe Ng'enda,mtendaji huyo ameibuka na kusema "sikuzaliwa ili kuwa Katibu wa CCM" .Ng'enda alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na gazeti hili kuhusu uamuzi wa kumwondoa kwenye nafasi hiyo ya utendaji ndani ya chama.

  Ng’enda alisema kuvuliwa kwake madaraka si kosa wala balaa na kwamba ni utaratibu wa kawaida katika shughuli za utendaji. “Hiyo ndio tabia ya vyeo, si kosa mimi kuondolewa lakini najipanga kupokea cheo kingine ndani ya chama changu,” alisema Ng’enda.

  Juzi Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana mjini Dodoma,ilitangaza kumvua madaraka Ng'enda kwa kile kilichoelezwa kuwa hakufuata maamuzi ya vikao halali vya chama kwenye masuala ya uchaguzi wa viti maalumu.

  Katibu wa Nec, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma baada ya vikao kuwa hatua hiyo inatokana na mtendaji huyo kwenda kinyume cha maamuzi ya vikao halali vya chama hicho.

  Alisema hata hivyo Ng’enda atapangiwa kazi nyingine ndani ya chama hichoHabari zaidi zilisema mkakati wa kujivua gamba ulioasisiwa na chama hicho Aprili mwaka huu, sasa unarejeshwa katika Kamati ya Maadili ambako watuhumiwa wa makosa mbalimbali watafikishwa na kuelezwa tuhuma zinazowakabili.

  Mpango wa kujivua gamba ulilenga kuwashinikiza watuhumiwa wa ufisadi kuachia nafasi zao za uongozi ndani ya chama hicho kinachotawala.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Good waambie, Pesa ninazo na nataka zaidi ya Ukatibu CCM
   
 3. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  hana mpya gamba naye tu
   
 4. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ni nani atakayethubutu kusema EL ni fisadi???"
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Nov 27, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu Kilumbe Ng'enda si ndiye alikuwa katika mchakato wa kumvua gamba mbunge wa kinondoni Ndg. Azzan, sasa amegeukiwa na kuvuliwa gamba yeye!!! Mchakato unaendelea: Nnape alikuwa katika mchakato wa kumvua gamba EL naona sasa naye huenda asisubiri kuvuliwa bali akajivua mwenyewe. Kitendo chake cha kukimbia na kuacha kikao kina maswali mengi kuliko majibu. Kuvuana gamba CCM ni mchakato na kunahitaji timing kama kumchinja kobe!!
   
 6. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  hayo yote yamemtoka baada ya kuvuliwa kagamba kake kadogo
   
 7. Nicksixyo

  Nicksixyo JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 949
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hakuna la maana hapo kama anatolewa mahali na kupelewa mahali pengine hii ni danganya toto mbaya sana, Kama ameoekana ni gamba hapo Dar halafu wanalivua hilo gamba na kwenda kulibandika mahali pengine huo bado ni uchafu mkubwa, Ni sawa na kutawaza makalio na kujipaka mahali pengine mwilini kinyesi hivyo...To me is still work done is equal to zero..Am done with CCM.:smash:
   
Loading...