ngassa atwaa kiatu cha dhahabu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
BAO la kisigino la kiungo wa Yanga, Nurdin Bakari lilitosha kufuta ndoto ya Simba ya kutetea ubingwa wake pamoja karamu ya mabao 4-1 dhidi ya Majimaji na kutawala kadi nyekundu na kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Nurdin akiwa amelipa mgogo goli alipokea mpira uliokuwa ukizagaa kwenye eneo la 18, kupiga kisigino na kumwacha kipa wa Toto Afrika, Hussein Tade aliyeingia kuchukua nafasi ya Wilbert Mwate akiruka upande wa kulia na mpira ukipata alipotoka kuipa Yanga bao la tatu.

Kipa Tade aliingia uwanjani dakika ya 83 kuchukua nafasi ya Mweta aliyekuwa kikwazo kikubwa kwa Yanga, akidai kuumia paja.

Mabingwa hao wapya walianza mchezo huo taratibu na kuifanya Toto kutawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza, lakini mambo yalibadilika nusu ya pili na kufanikiwa kupata mabao matatu muhimu.

Kabla ya kiungo Bakari kuipatia Yanga bao la kuongoza dakika ya 46, kwa mpira wa adhabu nje ya eneo la 18, uliogonga ukuta na kutinga wavuni.

Naye mshambuliaji Davies Mwape alifunga bao lake 8 msimu huu la pili kwa Yanga dakika 63, akiunganisha krosi ya Shadrack Nsajigwa, katika harakati za kumzuia nahodha huyo wa Taifa Stars, beki wa Toto Laban Kambole aliumia na kutolewa nje.

Awali mshambuliaji Mwape nusura aifungie Yanga bao la mapema dakika ya tisa baada ya shuti lake kugonga mwamba na kutoka nje.

Kipa wa Yanga, Yaw Berko alipewa kadi ya njano dakika 22, baada ya kudaka mpira nje ya 18, baada ya kurudishiwa pasi fupi, lakini aliweza kuokoa faulo hiyo.

Mwape aliipangua ngome ya Toto na kupiga shuti kali lililopanguliwa na kipa Mweta na kutoka nje.

Kipindi cha pili kocha Sam Timbe alimtoa Kigi Makassy, Idd Mbaga na kumwingiza Jerryson Tegete na Omega Seme.

Jijini Dar es Salaam; Vijana wa Partick Phiri waliopoteza dira mwishoni mwa msimu huu waliingia Uwanja wa Taifa kwa nia moja ya kupata mabao mengi ili kutetea taji lao ndicho walichofanya kwa kufanikiwa kupata mabao manne kabla ya Okwi kukosa penalti dakika 90.

Mshambuliaji Shija Mkina aliifungia Simba la kuongoza dakika ya 11 akiunganisha pasi nzuri ya Emmanuel Okwi kutokea upande wa kulia. Kabla ya Okwi kuipa Simba bao la pili dakika 24, kwa shuti kali kutoka nje ya 18, akipokea pasi Ally Ahmed Shiboli.

Majimaji walijitutumua na kupata bao la kusawazisha dakika ya 42, kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na Kassim Kilungo baada ya Mohamed Kijuso kuchezewa vibaya na Meshack Abel ambaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi Alex Mahagi kwa kitendo hicho.

Dakika 52, Kilungo nusura aipatia Majimaji bao la pili, lakini shuti lililokuwa likielekea nyavuni liliokolewa na Jerry Santo wakati huo Kaseja alikuwa ametoka golini.

Mwamuzi Mahagi alitoa kadi nyekundu ya pili kwa mchezaji Paul Ngalema dakika 43 baada ya kumcheza vibaya Mkina. Majimaji walipata pigo zaidi dakika 82, baada ya Kulwa Mob kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Santo.

Okwi aliifungia Simba bao la nne dakika 89 na kukosa penalti dakika 90 baada ya Santo kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Mshambuliaji Mbwana Samatta aliiyeingi kutokea benchi aliipatia Simba bao ka tatu akiunganisha krosi ya Okwi
Kocha wa Simba, Patrick Phiri amewatoa Aziz Gila, Mkina Shija na kumwingiza Nico Nyagawa na Mbwana Samatta.

MOROGORO
Mshambuliaji Mrisho Ngassa amefanikiwa kutwaa kiatu cha ufungaji bora msimu huu baada ya kufunga bao lake 16 na kuisaida Azam kuichapa Ruvu Shooting kwa mabao 2-1.

Ngasa alifunga bao hilo baada ya kuwahi mpira uliokuwa ukirudisha kwa kipa na beki Mangasin Mbonos kabla ya kumpiga chenga kipa Godhard Misweku na kufunga bao hilo dakika ya 75.

Mshambuliaji John Boko alifunga bao lake la 12 msimu huu kwa kuunganisha vizuri krosi ya Ngassa aliyewazidi ujanja mabeki dakika ya 48, Shooting walisawazisha dakika mbili baadaye kupitia kwa Jumanne Juma aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Saidi Madege.

Wakati huo huo, Uwanja wa Manundu wenyeji Mtibwa Sugar waliutumia vizuri uwanja wao na kufanikiwa kupata ushind wa mabao 2-0 dhidi African Lyon magoli yote yakifungwa na Thomas Moris kwa mkwaju wa penalti dakika 14 na jingine kwa kichwa dakika 72.
TANGA
Uwanja wa Mkwakwani, JKT Ruvu walilazishwa sare ya bao 1-1 na Polisi Tanzania kwenye mchezo uliokuwa na upinzani mkubwa.
JKT walikuwa wa kwanza kupata bao la mapema dakika 13, kupitia kwa Mwinyi Kazimoto kabla ya Bantu Nsungwe kuisawazishia Polisi dakika ya 55.
BUKOBA
Mshambuliaji Gaudence Mwaikimba ameshindwa kutimiza ndoto yake ya kuwa mfungaji bora baada ya timu yake ya Kagera Sugar kulazimishwa sulugu na AFC Arusha kwenye Uwanja wa Kataiba.

Sosthenes Nyoni, Burhan Yakub, Allan Goshashy, Juma Mtanda.

Orodha ya Mabingwa
2000 - Yanga
2001 - Simba
2002 - Simba
2003 - Simba
2004 - Simba
2005 - Yanga
2006 - Yanga
2007 - Simba
2008 - Yanga
2009 - Yanga
2010- Simba
2011- Yanga
 
Back
Top Bottom