Ngara yazidi kuwaka moto

Ngara yazidi kuwaka moto

John Malanilo

Member
Joined
Dec 2, 2013
Posts
50
Reaction score
13
Makamanda, Nipende kuwapongeza wananchi wa wilaya ya Ngara maana wameonesha ukomavu wa kisiasa. Mwezi uliopita baada ya mkutano wa Mwenyekiti wa Taifa na makamanda wengine wa anga, tulifanya mikutano 14 kwenye ngazi ya vitongoji ambako chadema tulipata mwitiko mzuri sana. katika mikutano hiyo iliyofanyika maeneo mbalimbali kama Muchingili, Ntobeye Centre, Chivu, Kigina, Nyarutiti, Mrugalagala, Kumukaritusi, Kalemela, Chenda, na maeneo mengine, wananchi walifurahia elimu ya uraia inayotolewa na Chadema ikiwa ni pamoja na kukomesha kero mbalimbali.

  1. Tumetetea wananchi katika kesi mbalimbalikama ile ya mama mmoja aliyefiwa na mtoto wake na kudaiwa kulipa laki mbili iliaruhusiwe na viongozi wa CCM kuzikakatika kata ya Rusumo. Kesi hiyo tumeitetea CHADEMA na wamefungwa jela mwakammoja mmoja na wakitoka jela wataezeka nyumba hiyo.
  2. Tumeweza kuteteawananchi katika kata ya Nyakisasa ambakowakata mbao waliingilia misitu ya asili katika maeneo ya vyanzo vya maji.CHADEMA imeingilia kati na uharibifu huo umesitishwa na wananchi na uongozi wawilaya umeendelea kufuatilia na kuchukua hatua zaidi.
  3. Tumefungua kesi dhidi ya mtu aliyeng'oa bendera ya chama katika kata ya Mganza mpaka leoameshikiliwa na kesi inaendelea. Mpaka sasa mtuhumiwa amekiomba chama kimwoneehuruma kwa sababu chama kilichomshawishi kung'oa bendera hakimsaidii naamefahamu kuwa alifanya kosa.
  4. Kata ya Bukiriro, wananchi waliokuwawanachelewa kufika sokoni, walikuwa wanatozwa faini ya sh. 300 bila kupewastakabadhi na pesa hizo hazikufahamika zinaenda wapi. Jambo hilo CHADEMA tumelikomeshana wananchi sasa wana uhuru wa kuingia sokoni wakati wowote bila bughudha ya faini.
  5. Tumetetea wanawake wa kata ya Mrusagamba waliokuwawanatakiwa kwendaa klinik na jembe ili wamlilie nesi katika zahanati yaMagamba. Pamoja na kuwa viongozi wa CCM kama mwenyekiti wa kijiji na mtendajiwa kijiji wapo hawakitetea mpaka Chadema ilipozuia wanawake kupeleka majembe. Nanesi alipokuja juu, Chadema tukamtuliza. Mpaka leo ni marufuku kwenda na jembe klinik.

Attachments

  • Msafara ukimsubili Mh Mbowe Kumnazi.JPG
    Msafara ukimsubili Mh Mbowe Kumnazi.JPG
    33.1 KB · Views: 1,005
  • Ngara 25.2.14.JPG
    Ngara 25.2.14.JPG
    35.8 KB · Views: 963
  • Ngara.JPG
    Ngara.JPG
    31.6 KB · Views: 932
  • Wananchi wa Ngara wakifuatilia Mh Mbowe.JPG
    Wananchi wa Ngara wakifuatilia Mh Mbowe.JPG
    38.5 KB · Views: 953
  • Wazee hawakubaki nyuma.JPG
    Wazee hawakubaki nyuma.JPG
    44.9 KB · Views: 922
  • Kamanda Malanilo Akihutubia wananchi Kumnazi.JPG
    Kamanda Malanilo Akihutubia wananchi Kumnazi.JPG
    29.7 KB · Views: 910
  • Makamanda waliolinda Kajugujugu Ngara.JPG
    Makamanda waliolinda Kajugujugu Ngara.JPG
    44.1 KB · Views: 899
  • Na watoto wajue CDM Vema.JPG
    Na watoto wajue CDM Vema.JPG
    41.2 KB · Views: 900
teh teh teh, kwi kwi kwi, ahahahahahaha, Kamnda Malanilo umevunja sana mbavu zangu, hayo ndo maendeleo ya CHADEMA mnayojivunia nayo?

hahahahaha, kuwa na aibu kidogo bas Kamanda

Hahahahahaha, hayo ndo umejipanga wewe na Mdogo wako Dk Bujali kuombea kura kwa wanangara 2015?mbona weak points tuuu?

Ngoma ya wanangara wewe na mdogo wako Dk Bujali hamuiwezi, hiyo Ngoma muachieni Dk Sebuyoya aicheze
 
Hongera John Malanilo

Kazi ya ukombozi wa Mtanzania ni ngumu na itachukua muda, lakini mafanikio ni dhahiri. Waswahili husema, 'bandu bandu humaliza gogo'.
 
Last edited by a moderator:
teh teh teh, kwi kwi kwi, ahahahahahaha, Kamnda Malanilo umevunja sana mbavu zangu, hayo ndo maendeleo ya CHADEMA mnayojivunia nayo?

hahahahaha, kuwa na aibu kidogo bas Kamanda

Hahahahahaha, hayo ndo umejipanga wewe na Mdogo wako Dk Bujali kuombea kura kwa wanangara 2015?mbona weak points tuuu?

Ngoma ya wanangara wewe na mdogo wako Dk Bujali hamuiwezi, hiyo Ngoma muachieni Dk Sebuyoya aicheze

Mabunu,

Pamoja na kuficha identity yako. Nadhani una point muhimusana. Na pia unakubaliana kuwa Ngara inaweza kwenda kwa Chadema. Katika maelezoyangu uliyoyaita “weak points” sijasema Dr. Ssebuyoya hafai.
Nadhani tuwasiliane tuone namna ya kuhakikisha vitongojitunashinda ili huyo unayemtaka apate pa kupita. Hata uchaguzi wa kata uliopitatumefanikiwa kurudisha kata zetu na kuongeza moja lakini sababu kubwa yakutoshinda, ni kwa vile ngazi za msingi hatujafanya kazi nzuri sana badala yakewengi kama wewe mnaangalia ngazi ya jimbo kumbe mizizi hamjaiangalia.
Hapo hakuna ugomvinashukuru kuwa unakubaliana kuwa kazi tumeifanya na Ngara kwa Chademainawezekana. Mungu akubariki

Malanilo
 
Ukifiwa ulipe laki mbili. ..
Uende kliniki na jembe...
Ukichelewa sokoni 300...

Tanzania humu humu?!!!
Ptuu... makwata
 
teh teh teh, kwi kwi kwi, ahahahahahaha, Kamnda Malanilo umevunja sana mbavu zangu, hayo ndo maendeleo ya CHADEMA mnayojivunia nayo?

hahahahaha, kuwa na aibu kidogo bas Kamanda

Hahahahahaha, hayo ndo umejipanga wewe na Mdogo wako Dk Bujali kuombea kura kwa wanangara 2015?mbona weak points tuuu?

Ngoma ya wanangara wewe na mdogo wako Dk Bujali hamuiwezi, hiyo Ngoma muachieni Dk Sebuyoya aicheze
Huyo Sebuyoya ni Mtanzania kweli?
 
Back
Top Bottom