New story: My blood is green, yellow, blue and black, story ya ujasusi.....

endrizzy

Senior Member
Oct 19, 2015
186
137
SEHEMU YA PILI.

Miaka mitatu tu tangu Raisi atoke Syria lakini malalamiko yalikuwa mengi sana wengi walisema Raisi Nobert amebadilika sana amewageuka wapiga kura wake wakiwa hawajui kuwa Yule si Raisi wao, Maisha Tanzalia ghafla yalikuwa magumu sana hali a uchumi ilizidi kuporomoka sana mazao yote yalikuwa yakiuzwa nje wawekezaji walikuwa wanavuna Huku alafu wanapeleka vitu Marekani na Britain ikafika wakati wakaleta wanajeshi wakidai wamekuja kwa ajili ya kutoa mafunzo ya kijeshi lakini haikuwa ivo kwani walikuwa wanafanya wanavotaka mtaani , wanawabaka watoto wa kike, wanawaua watu ovyo.

Nirirudi zangu Tanzalia kwa lengo moja tu kuthibitisha kuwa Yule si Raisi wa Tanzalia lakini swali likaja kichwani kama Yule si Raisi je ni nani na Raisi yuko wapi, kichwani nilijua kabisa kama Raisi ametekwa basi lazima atakuwa hai maana kuna vitu wanaviitaji kumuelekeza Yule kopi.

Kazi ilikuwa ngumu sana kwani kila kona ya nchi walijaa askari wa UN wakidai wenyewe wamarekani lakini walikuwa ni askari wa USA na UK nilifanya kila mpango niwasiliane na mkuu wa majeshi ikanibidi nitumie mbinu ya ziada ili niweze kuwasiliana na mkuu wa majeshi kitu cha kwanza nilichofanya .Niliingia kwenye system ya jeshi na kuweka appointment na mkuu wa jeshi kama mwandishi wa habari kutoka usa pia nilitengeneza kitambulisho cha shirika kubwa la ccn na kujiingiza katika list ya wafanyakazi wa ccn nilifanya yote hayo ili niweze kumuona mkuu wa majeshi ili niwze kumuoji na kujua kama nay eye ni kopi au la.

Siku ikawadia nikaenda zangu hadi makao makuu ya jeshi nilikuwa nimewai sana kwa iyo sikumkuta mkuu ikabidi imsubirie,alipofika alinisalimia na kunikaribisha hadi ofisini kwake na kuanza maongezi yetu kwanza kabisa mfukoni nilikuwa na device yak u scan bugs baada ya kuingia tu ofisini kwake nikaskia beep sound I knew kabisa kulikuwa na bugs so nikawa makini sana na maneno yangu. Nilivaa miwani yenye uwezo wa kurekodi maana nilikatazwa kuingia na kamera ndani ili nirekodi nikiwa namuuliza maswali ilikuwa hivi….

Mimi. i hope you will be comfortable me asking anything?

Mkuu..yes..

Mimi. Nilimuuliza, umezaliwa au umetengenezwa ? nilimuuliza ili swali nione reaction yake tu akajibu

Mkuu..nimezaliwa katika mkoa wa pwani kwa iyo mimi ni mkwere kabisa wa kibaha. Baada ya kupata majibu yake sikuwa na haja kabisa ya kuendelea kumuuliza maana nilichokuwa nataka nilishakipata mimi haja yangu ilikuwa ni reaction yake tu maana kopi wanatabia moja kwa kuwa amekalilishwa hata ukimuuliza mara sita ye atajibu ivo ivo bila kubadilisha neno. Nilikuwa nimejiridhisha kazi ikabaki nitaongea nae vipi nikamuaga nikamuambia namuachia maswali maana nilikuwa nafanya research nikamuachia na kuondoka zangu.

Baada ya kufikiria sana jinsi ya kuwasiliana na mkuu nikapata wazo na kuamua kulala ili kesho yake nitekeleze.

Asubuhi yake nilipoamka nilienda karibu na kampuni moja ya simu na kuhack kwenye system yao nikawa nasearch namba zote zillizokuwa zimesajiliwa kwenye ile kampuni kwa jina la mkuu hadi nikaipata namba ya mkuu wa majeshi bila kuchelewa nkacreate secure line nikmpigia mkuu na kuanza kuongea nae,

Mkuu....halloo we nani mwenzangu?

Mimi....naitwa Erick mwandishi niliyekuja jana hapo ofisini kwako nina ujumbe mzito sana nataka nikuambie lakini siwezi kukuambia kwenye simu nataka tukutane najua hapo ulipo wanakusikiliza na usishtuke we kuwa kama kawaida lakini najua wanakuangalia hapo na pia wamekuwekewa tracking device inabidi tufanye haraka kabla hawaja tafsiri haya maongezi.

Mkuu... we ni mtanzalia mbona unaaongea Kiswahili vizuri ivo na tukutane wapi sasa.?

Mimi....Mama kafa bibi mzima Tupo Msibani

Hiyo ilikuwa ni code ya kijeshi ikimaanisha nyumbani ulipozaliwa. Niliamini mkuu lazima angekuwa anajua tu. Jamaa alikuwa mkwere wa pwani so fasta alishajua kilichoongelewa pale akaniambia kuku akiingia bandani akimaanisha tukutane jioni , tukakubaliana .

Nikachukua gari mpaka kibaha pwani ulikuwa mwendo kama wa nusu saa hivi nilipofika nilisubili sana maana mkuu ilibidi aage anaenda kuzika ndo wakamkubalia, baada kama ya masaa mawili jamaa alitokea na kunikuta mimi nikiwa peke yangu nikamfata fasta nikamuwekea device ya kujam signal na fasta nikamtoa ile trcking device na kumpeleka sehemu undergroung sababu hawawezi kutu track huko na kuanza kumwambia kila kitu akasema hata yeye alishagundua hilo lakini alikuwa hana jinsi ya kufanya zaidi ya kuangalia tu.

Tukapanga kitu cha kwanza tumtafute raisi halafu tujue nini kinafuata baada ya hapo, mkuu wa majeshi alikuwa mkali kwenye kombat mimi nilikuwa mkali kwenye any explosive device and kwenye computer pia nilikuwa mkali sana so tukaunda bonge moja la timu, kabla hatujaenda Syria kwanza alinambia tukamchukue mwanae alikuwa Dar es salaam. Fasta nika mpigia simu kwa kutumia secure laini hili wasiweze kunping back my location na kumpa baba ake aongee nae waliongea kwa code wakakubaliana .

Tulifika Dar es salaam kama mida ya saa 12 asubuhi hivi tukamkuta dogo alipokubaliana na baba ake nilipomuona tu nkamsearch nikamkuta nay eye amewekwa tracking device faster nikaitoa lakini sikuitupa maana nilijua ntakuja kuitumia tu, tukawa tunaelekea zetu mpakani mwa Tanzalia kupitia mbeya safari ilikuwa ndefu sana but kwa mbali kwa kuwa tayari nilikuwa nimesha hack system ya wamarekani nikaona kuna drone moja ninatufatilia nikahack ile drone na fasta nikawa naikontrol nikawaacha wafanya wanachotaka then mi nkaicontrol baada ya wao kulunch bomu, kama nilivootea wakaachia bomu and target ilikuwa gari yetu lakini kwa tayari nilikuwa ndani ya ile system ya drone nikachange destination faster na kulipua gari ya mbele yetu na kumwambia tuchange direction faster twende iringa then Malawi faster nikarusha ile tracking device kwa ile gari iliyokuwa inaungua na sie tukasepa then tukafika sehemu tukabadilisha gari hao hadi iringa , muda wote huo ikuwa na muda wa kumuangalia Yule mtoto wa mkuu dah alikuwa bonge moja la demu yani tena umri wangu kabisa lakini sikuwa na muda huo tena n ilikuwa nawaza kazi tu.

Syria.....

Rasisi nobert amefungwa katika maximum security place ambayo hata kwenye satellite haionekani wapo kati kati ya jangwa wamechimba underground ndo wapo huko na hiyo place yao ya kufa nyia mambo yao.


Iringa...

Tulifika iringa baada ya masaa kadhaa tukaunganisha mpaka songea ilitubidi tubadilishe route tuende msumbiji tulipofika songea tukasepa zetu hadi msumbiji, kufika huko tukawa tunataka kuonana na mkuu wa majeshi wa huko atusaidie mimi kama kawaida yangu faster nikahack system yao na kuingia kwenye network yao na kuplant virus ambaye anani alert kila police wanapo wasiliana ili nijue mwenendo wa police pia nikaitafuta namba ya mkuu hadi nikapata. Tukaongea nae akatuelewa tukapanga sehemu tukakutana tukamwambia kila kitu akahaidi kutusaidia na kutuambia tukae hapo hotelini hadi atakapo rudi,

Msumbiji...

Tulikaa kama masaa mawili kimya lakini mimi kama kawaida yangu siwezi kuwa sehemu bila kucontrol camera nilikuwa naona almost sehemu kubwa ya hotel nikashangaa kuona askari wa msumbiji kama mia hivi wakiwa njee ya hoteli tayari kwa kuingia ndani......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom