Dunia inapitia katika vipindi mbalimbali; Kuna jamii zilishape watu wake kwa kuweka adhabu kali sana za kuogofya kwa wale wote waliothibitika kufanya matukio ambayo jamii iliyakataa kama kuliwa na watu uliowakosea (cannibalism) kunyongwa, kuchinjwa hadharani, kutupwa kwenye mto wenye mamba huku watu wote wakimshuhudia tc lakini still hao watu waliendelea kuprevail katika vizazi na vizazi.
Zikaja Zama za dini ili kujenga upendo na kupunguza wingi wa machukizo mbele ya macho ya jamii na Mungu na sasa ni Zama za Sayansi na teknolojia. So Yale yote yanayohusiana katika kuamini uwezo wa binadamu katika kujiamulia na utendaji wake katika maisha ya kilasiku ndicho kinachopigiwa kelele sasa. Tutapinga lakini waeneza hizo ajenda wataendelea kuwepo na wengine wataongezeka na baadae zitafuata Zama gani huko mbeleni.
Yalishanenwa toka enzi na enzi, hayana budi kutokea na mengi yatafuata