Siku zote katika maisha yetu hatutakiwi kukata tamaa bali tunatakiwa kupambana hadi kufikia pale tulipotaka kuwa, tunatakiwa kupambana kwa kuwa hakuna ajuae kesho chini ya jua
Lolote linaweza kutokea kwa wakati wowote....wapo watu waliokuwa masikni wa kutupwa lakini leo hii wanaogelea katika utajiri kwa namna ambayo hawakuwahi kufikria maishani mwao....wapo watu ambao waliwakebehi wenzao kuwa wao wana uwezo kifedha, lakini leo hii tumeshuhudia anguko lao na tunawaona wakiteseka.
Katika ulimwengu huu usijaribu kumdharau mtu yoyote kwani kila mtu hapa duniani ana nafasi yake.....na ndio maana muumba akatuumba tofauti ili kila mmoja akae kwenye nafasi yake.......kila mmoja wetu ana stahili heshima si kwa rangi yake wala kwa uwezo wake kiuchumi na wala si kwa kimo chake bali kwa ubinaadamu wake.
pia tukumbuke mafanikio hayaji kama ndevu zinavyoota au nywele bali mafanikio hutafutwa kwa juhudi na maarifa huku ukifanya kwa bidii na malengo,, jambo la msingi ni kutokukata tamaa........