Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,074
- 7,064
Timu ya taifa ya Morocco anasonga mbele katika hatua inayofuata baada ya kumuondoa Uholanzi kwa mikwaju ya penati 3 kwa 2
Morocco linemekuwa taifa la kwanza kutoka Afrika kusongea hatua nyingine
Je watafikia rekodi yao ya mwaka 2022 ya kufika hadi nusu fainali?
======
Uholanzi na Morocco zitamenyana katika Uwanja wa Monterrey kwenye mchezo wa Raundi ya 32 ya Kombe la Dunia, ukiwa unatarajiwa kuwa mmoja wa mechi zenye ushindani mkubwa kutokana na kiwango kizuri ambacho timu zote mbili zimeonyesha.
Uholanzi ilimaliza kinara wa Kundi F bila kupoteza mchezo wowote (imeshinda mechi mbili na kutoka sare moja), baada ya kuichapa Tunisia mabao 3-1 katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi, matokeo yaliyoipa morali kubwa kuelekea hatua ya mtoano.
Kwa upande wa Morocco, walionyesha uwezo mkubwa wa kupambana baada ya kuruhusu bao mapema katika dakika ya 10 dhidi ya Haiti, kabla ya kurejea na kushinda mabao 4-2. Ushindi huo ulikuwa wa kwanza kwa Morocco katika historia ya Kombe la Dunia kutoka nyuma baada ya kufungwa bao la kwanza, kufuatia rekodi ya awali ya sare moja na kupoteza mechi 11 walipokuwa wakianza kufungwa.
Hii itakuwa mara ya pili kwa Uholanzi na Morocco kukutana kwenye Kombe la Dunia. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1994, ambapo Uholanzi ilishinda kwa mabao 2-1.
Uholanzi bado haijawahi kupoteza dhidi ya timu za Afrika kwenye Kombe la Dunia, ikiwa imeshinda mechi tano na kutoka sare moja. Morocco, kwa upande wake, inalenga kupata ushindi wa pili mfululizo dhidi ya timu kutoka Ulaya kwenye Kombe la Dunia, baada ya kuifunga Scotland bao 1-0 katika hatua ya makundi.

Historia ya Kukutana