Netanyahu akabiliwa na tuhuma za ufisadi

NGolo Kante

Member
Joined
Feb 28, 2017
Posts
80
Reaction score
131
dfg.jpg

MAMLAKA za dola nchini hapa zimesema zina ushahidi wa kutosha unaoonyesha Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu anahusika na vitendo vya rushwa na ufisadi ingawa yeye anakanusha akidai tuhuma hizo zinasambazwa na wapinzani wake wa siasa.

Polisi hao walisema jana kwamba uchunguzi wao unaonyesha Waziri Mkuu Netanyahu alipokea rushwa kuingilia kati katika moja ya kesi ambazo zilikuwa zikiikabili kampuni kubwa ya mawasiliano ya Bezeq.

Polisi walisema wana ushahidi huo ambao unaonyesha wazi Netanyahu na mkewe Sara, walipokea rushwa hiyo na kufuja fedha hizo kupindisha ukweli.

Katika madai hayo Netanyahu anashuhutumiwa kujichotea mamlioni ya dola katika kampuni hiyo ya Bezeq kuviziba mdomo vyombo vya habari vilivyokuwa vikiripoti kesi hiyo.

Washauri wake wawili waandamizi wamegeuka kuwa mashahidi na wanasema wamezipa mamlaka ushahidi wa kutosha unaothibitisha kuwapo vitendo hivyo.

Waandishi wa habari ambao hapo awali walifanya kazi katika tovuti ya Walla wamewahakikishia polisi kuwa walisumbuliwa na kulazimishwa kuandika habari nzuri tu zinazomuhusu Netanyahu.

Hata hivyo Netanyahu anakanusha taarifa hizo akisema zilianza kusambaa hata uchunguzi bado haujaanza kufanyika.

Kutokana na taarifa hiyo ya polisi kumeibuka wito wa kumtaka Netanyahu ajiuzulu.

“Waziri Mkuu hana tena sifa ya kuendelea kushikilia nafasi yake ni lazima ajiuzulu hata leo,” alisema Tamar Zandberg, ambaye anaongoza Chama chenye mlengo wa kushoto cha Meretz. “Israel ni lazima iingie katika uchaguzi,”aliongeza kiongozi huyo.

Hiyo ni mara ya tatu kwa polisi kutangaza mashitaka dhidi wa waziri mkuu huku mkewe akiwa ameshashitakiwa katika kesi tofauti zinazohusiana na matumizi mabaya ya fedha za serikali.

Chanzo: Mtanzania
 
sijawahi ona fisadi la kutupwa dunia hii km netanyahu
 
Mnafiki utamjua tu kwa kauli zake; isifie na demokrasia ya Israel! Ayatollah na genge lake wanavyoitafuna Iran hakuna hata wa kunyayua mdomo maana wote wataishia "shimo la tewa" kama sio kupotelea kusikojulikana wao na familia zao kupotezwa mazima!

Israel among the most democratic nations in the world; kule hakuna sijui wewe ni nani, ukizingua unachukuliwa hatua! No supreme leader (next to Gog?) in Israel; all are equal under the law.
 
Ayatollah+ shay kichwa hakina jipya zaidi ya kujilipua kumfurahisha Allah
 
Mnafiki utamjua tu kwa kauli zake; isifie na demokrasia ya Israel! Ayatollah na genge lake wanavyoitafuna Iran hakuna hata wa kunyayua mdomo maana wote wataishia "shimo la tewa" kama sio kupotelea kusikojulikana wao na familia zao kupotezwa mazima!

Israel among the most democratic nations in the world; kule hakuna sijui wewe ni nani, ukizingua unachukuliwa hatua! No supreme leader (next to Gog?) in Israel; all are equal under the law.
Kwaiyo kwenye gazeti la mtanzania Kuna maayatollah mkuu....
 
Mnafiki utamjua tu kwa kauli zake; isifie na demokrasia ya Israel! Ayatollah na genge lake wanavyoitafuna Iran hakuna hata wa kunyayua mdomo maana wote wataishia "shimo la tewa" kama sio kupotelea kusikojulikana wao na familia zao kupotezwa mazima!

Israel among the most democratic nations in the world; kule hakuna sijui wewe ni nani, ukizingua unachukuliwa hatua! No supreme leader (next to Gog?) in Israel; all are equal under the law.

ALIVYOINGIA KWA GIA KUBWA MIM NIKADHANI ATAMALIZIA TANZANIA, YEYE ANAMALIZIA HUKO AS IF ALIWAHI KUISHI HUKO WAKATI HAPA WATU WANALALA NJAA NA VIONGOZI WAPO KAZI KUTETEA PUMBA KILA SIKU KULINDA VITAMBI VYAO.
 
Back
Top Bottom