Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,352
- 14,381
Luka 13:1-5-''Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao.Akawajibu akawaambia.Je,Mwadhani ya kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote,hata wakapatwa na mambo hayo? Nawaambia:sivyo;Lakini msipotubu,ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.Au wale kumi na wanane,walioangukiwa na mnara huko Siloamu,ukawaua,mwadhani kwamba wao walikuwa Wakosaji kuliko watu wote waliokaa Yerusalemu? Nawaambia:sivyo;Lakini msipotubu ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.''
A:TAFAKARI.
Wapendwa wana Taifa la Mungu Tumsifu Yesu Kristo.....!!!,Katika sehemu hii ya Maandiko Matakatifu tunapata kujifunza juu ya Matukio haya Makubwa mawili;Tukio la Kwanza ni la Pilato kuwaua Wagalilaya waliotoa Sadaka za Wanyama katika Hekalu la Yerusalemu,Kwa jinai hiyo damu ya Wagalilaya na damu ya dhabihu(damu za wanyama waliochinjwa kwaajili ya sadaka) zilichanganyika.Pilato alitenda dhambi ya Uuaji na kukufuru Hekalu.
Tukio la pili ni kuhusu habari ya Mnara uliobomoka na kusababisha vifo pale ulipowaangukia watu;Katika jamii ya Wayahudi walifikiri kwamba kufa kwa watu hao kulikuwa ni adhabu ya Mungu kwasababu ya dhambi zao.Walidhani kwamba bila shaka Wagalilaya hao walikuwa wakosefu wakubwa,hivyo waliadhibiwa kwaajili ya dhambi zao.Kanuni yao ya Imani ilisema kwamba,''Hakuna adhabu bila dhambi,kila teso au ajali ni adhabu kwaajili ya dhambi iliyotendeka''.Yesu Kristo alipinga vikali Mtizamo huu wa Kiimani,na kwamba Watu waliouawa kwa Upanga wa Pilato au kwa Mnara uliobomoka hawakuwa Wakosefu zaidi kuliko watu wengine.Yesu anakazia sana suala la Wongofu na kusisitiza kuwa sote tusipotubu tutaangamia.
B:JAMII YETU INA MTIZAMO UPI JUU YA WATU WENYE SHIDA/MATATIZO??.
Ukichunguza vizuri katika jamii ya sasa haina utofauti sana kimtizamo na jamii ya Wayahudi wa kipindi cha Yesu;Imekuwa ni jamii ya kuhusisha Matatizo yanayompata mtu na dhambi zake;Kwa mfano,Mtizamo uliojengeka ktk jamii juu hawa ndugu zetu,rafiki zetu na Wapendwa wetu walioathirika na Virus vya Ukimwi-VVU ni mbaya wengi hudhani kuwa labda kuwa walikuwa wazinifu sana kumbe sivyo kwani wapo ambao hawakuambukizwa kwa Uzinzi,Fikiri juu ya mtizamo wa jamii yako juu ya Mwanamke aliyeachika ktk Ndoa(WASIMBE),Jamii yetu huwachukulia km watu wasioweza kumudu maisha ya Ndoa kwasababu ya Nidhamu mbovu,lkn sivyo;Fikiri juu ya Familia ambazo watoto wao wamekosa maadili,Jamii yetu hukimbilia kuwahukumu wazazi wao kwamba hawakuwalea vizuri,hakika sivyo maana wapo wazazi waliojitahidi kimalezi lkn Dunia imewaharibu watoto wao;Hivyo ndugu zangu tuache kuhukumiana kwa misingi ya Matatizo na Mikasa inayowakuta wenzetu.Kuna msemo niliwahi kuusoma kwenye gari moja kubwa la Mizigo nao unasema hivi,''CHEKA SANA,SIMULIA SANA,LAKINI OMBA MUNGU YASIKUKUTE''.Tuombe Neema ya Mungu kuwa na Huruma kwa wenzetu wanaokumbwa na mikasa na shida za Kimaisha na kisha tuwaombee kwa Mungu ili awapunguzie mateso yanayowapata kutokana na shida hizo,Hakika Mungu atatubariki na kutuzidishia kuliko kuwahukumu.
C:SALA YA KUAGIA
Ee Baba Mungu,Mwamba wangu na Ngome yangu ninakushukuru kwa wema wako kwangu,kwa kunijalia Afya njema;Baba ninawaleta Mikononi mwako wote wenye shida za magonjwa,ulemavu,shida ktk ndoa,na matatizo mengine uwajalie Neema zako ili waondokane na matatizo hayo;Ee Mungu kunilinda mimi si kwamba mimi ni Mwema kuliko hao,tena yawezekana mimi ni mdhambi kuliko hao walio katika shida,najua nipo hivi kwa Neema zako wala si kwa ujanja wangu,Ninakuomba unihurumie mimi mwenye dhambi,Uwahurumie na Wakosefu wenzangu,tujalie Neema zako tupate kukurudia wewe.AMINA.