Katika maisha haya ya kila siku na kutokujua kipi kinaweza kutokea kwa wakati wowote wanadamu tumekuwa na uoga, maana hatuna uhakika wa maisha yetu japo kwa dakika moja mbele katika nyanja zote za maisha.
Hofu na uoga imekuwa sehemu ya maisha ya mwanadamu hata awe na uwezo, mali, nguvu kiasi gani bado ana uoga ndani yake. Tunahofu juu ya kazi zetu maana leo upo lkn huna uhakika kama kesho utakuwepo, tunahofu juu ya mahusiano yetu maana yanaweza kuvunjika wakati wote, tunahofu juu ya biashara zetu maana wakati wowote mambo yanaweza kubadilika hofu kila sehemu. Kutokana na hofu hiyo weengi wametafuta namna ya kuishinda wengine wamekwenda kwa waganga, wengine kwa wasoma nyota, wengine kwa wabashiri, wengine kwa wataalamu wa saikolojia nk
Lakini asubuhi ya leo nina ujumbe kwako wa tumaini yupo wa kuipeleka hofu na uoga wako. Katika kitabu cha Isaya Mungu anasema
ISA. :41:10
usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
Bwana akubariki katika asubuhi ya leo na siku ya leo ikawe ya baraka tele.