Neno la Mungu ni lazima litimie

Midazolam

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
295
500
Amani ikae na watanzania wote.

Mtu wa Mungu ana hekima, mtu wa Mungu ni mpole, Mtu wa Mungu anapenda amani, mtu wa Mungu ana upendo na Kikubwa Mtu wa Mungu, hana maneno machafu kwa watu wake, mtu wa Mungu ni mpatanishi, anapendwa na kufuatwa kwa mazuri yake

Pia mtu wa Mungu hana upendeleo kwa watu fulani, hugawa sawa sawa kwa pande zote na Mtu wa Mungu anampenda hata adui yake.

Kwa maisha ya kawaida na la kiroho zaidi,maisha ya Tundu lisu ni ushuhuda wa kweli na huponya kwa wanaoamini matendo makuu ya Bwana Mungu wetu.

Lisu alipopigwa risasi kwa akili ya wanadamu ni vigumu kujua Kama mpaka leo hii huyu jamaa anatembea na kushukuru kwa mabaya yaliompata.

Waaumini tunasema kama Mungu anakupenda hakuna wa kukutoa uhai, vita ni vya Mungu achana Mungu apigane nao

Ni vizuri umuombee adui yako ili unapofanikiwa adui yako ajionee kwa macho,

Mungu alituumba kwa mfano wake na nafsi zetu zina huruma, na ndio maana unapofanya jambo baya lazima nafsi itakusuta tu.

Ukweli ni kwamba waliomshambulia lisu hawana amani ya moyo na hii itawatesa mpaka siku ya kufa kwao labda tu wajitokeze na kusema na kuomba msamahaa,msamahaa una nguvu sana na Mungu anasamehe kwa mwenye uhitaji wa msamahaa

Dhambi unayotenda leo usije ukasahau halitakuacha litakutafuna na mpaka na kizazi chako,kimbilio lake ni kutubu tu.

Watumishi wa Mungu ni watu wenye mamlaka makubwa sana mbele zake Mungu, usije ukapuuuza neno analotoa mtumishi wa Mungu. Waumini wanaelewa ninachomaanisha .

Natabiri kwa yoyote atakayepindisha matokeo ya uchaguzi, Mungu atalipa kwa muda mchache sana na watanzania mtaona huu utabiri. Naona kama kifo kwa mtu atakayefanya hivyo,

Mungu ana nguvu sana.

Tanzania utabiri unaenda kutimia.
 

Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
13,051
2,000
Na Mungu siyo Bagonza wala Mwingira au Gwajima!

Mungu ni yeye yule jana leo na hata milele,!

Ndio yule yule aliembadirisha Sauli kutoka kuwa muuaji hadi kuwa huyu tunaemsoma kwenye nyaraka za biblia!

Maana yangu ni ipi?

Ccm itashinda tena kwa kishindo kikubwa sana huku Lisu akipata asilimia 20 tu.

Tusijifanye sie kina Mwamakula, Bagonza na Mwingira kama ni wacha Mungu sana hapa.
 

kurlzawa

JF-Expert Member
Jan 23, 2018
12,499
2,000
Na Mungu siyo Bagonza wala Mwingira au Gwajima!

Mungu ni yeye yule jana leo na hata milele,!

Ndio yule yule aliembadirisha Sauli kutoka kuwa muuaji hadi kuwa huyu tunaemsoma kwenye nyaraka za biblia!

Maana yangu ni ipi?

Ccm itashinda tena kwa kishindo kikubwa sana huku Lisu akipata asilimia 20 tu.

Tusijifanye sie kina Mwamakula, Bagonza na Mwingira kama ni wacha Mungu sana hapa.
Mungu sio mpumbavu kama CCM mnavyodhani mauji ya wapinzani kuwanyanyasa ala Mungu awe na nyie labda kama mna ubia nae.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom