NENO LA MUNGU MTAKATIFU ALILOLIONA MWONAJI AKALIANDIKA.

NENO LA MUNGU MTAKATIFU ALILOLIONA MWONAJI AKALIANDIKA.

Joined
Aug 19, 2018
Posts
14
Reaction score
2
MIMI MTAKATIFU BWANA YESU KRISTO NASEMA; NENO LANGU LIMEGEUZWA DUNIANI NA WACHUNGAJI.

Mimi Mtakatifu BWANA YESU KRISTO nasema hivi, neno langu linavyogeuzwa na wachungaji wanaohubiri katika makanisa yote duniani na kuniudhi sana mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu, napenda kuyasema makosa yote yanayosemwa na watu hao duniani.
Kosa la kwanza, neno langu linasema watakao ingia juu MBINGUNI ni watu wachache, wakijua kwamba maneno yangu yote yameungana pamoja, hakuna hata moja linalo pingana. Watu hao wamejifananisha na mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu na kunipita wakijifanya eti nimewaruhusu kwakuwa nilisema mtafanya kazi kubwa kuliko hizi. Je, kazi kubwa ndio kuzivunja amri kumi zangu mimi MUNGU wenu Mtakatifu niliye juu MBINGUNI? Au kazi kubwa nikushindwa kulifuatwa neno langu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu Mkombozi wenu, niliyetoka juu MBINGUNI nikazaliwa kama mwanadamu, ukafika wakati nikawahubiri watu neno langu,mkanichukia mkaamua kuniua, kwa midomo ya kila mtu duniani anasema ananipenda. Lakini maneno ya mtu huyo yananikosea, matendo yake yananisaliti. Kama mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu nilichukiwa na watu wakaamua kuniua, je, hamuoni kwamba ilikuwa njama ya kuwafanya watu wote wasiniamini na wala wasilifuate neno langu? Yaani baada tu ya kufa, watu walibadilishiwa maneno yangu na kuhubiriwa kinyume, wakisisitizwa wasinifuate kabisa na kila atakaye onekana ananifuata, naye atakufa kama nilivyokufa mimi pale msalabani wakati ule ule wa kifo changu.

Mamlaka ya dhambi inayopingana na mimi MUNGU wenu Mtakatifu niliye hai juu MBINGUNI, imewadhuru hata watu wa leo ambao wamejaa hofu kama wakiwa wasabato kama mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu. Basi walivyowaza walipoamua kunipinga mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu, wakawaza yawezekana watu walioniua pale msalabani wakaweza kuwafuata huko waliko wakawaua, hofu hiyo hawaihubiri makanisani, waliokuwa wakiifahamu ni watu wa wakati ule walikuwa wakisema hawata ifuata Imani yangu katika vizazi vingi, watahamasisha watu wa kila kizazi wafanye hivyo. Basi wameendelea kila siku kunipinga mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu kwa sababu umefika wakati watu wanione mimi BWANA YESU Mtakatifu nilikosea kusema ni watu wachache tu ndio watakao ingia huku juu MBINGUNI, kwa sababu yakuwajaza watu uongo wakiogopa kukimbiwa na watu. Je, anawezaje mtu aliyetokana na mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu mtu huyo akanikataa? Basi watu wengi mmekuwa wanafunzi kama Yuda alikyekuwa mwanafunzi wangu akaamua kunisaliti. Basi napenda kuwaambia watu wote mlioamua kuliacha neno langu katika hii dunia mko nyuma ya Yuda, muutegemee moto wa jehanamu kama watu wote walionikana wanavyotegemea.

Tatizo lililoko mbele yenu wanadamu wote kasoro wateule, mmejiamulia kufanya mambo yenu wenyewe na kuniacha mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu Mkombozi wenu, hakika hamta pona hata unyooshe mkono siku ya hukumu. Rudini, ondokeni mlikopotea kumbukeni maneno yangu mimi MUNGU wenu Mtakatifu mliyoyasahau kwa sababu kila mtu anaye niamini kwa makosa katika hii dunia anasema kila anapoiona siku, mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu niliye juu MBINGUNI ni njia kweli na uzima. Watu wengi hawajui wanaye mfuata awaingize huku juu MBINGUNI njia yake sio hiyo na hawataki kuamini. Watu wengi wanakufa katika Imani zao hizo za kujiandaa kuingia katika moto wa jehanamu. Napenda kutaja makosa ya watu wengi wanaofanya makossa na nikaamua mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu wa MBINGUNI kuachana na watu hao, wameziacha amri kumi zote zangu mimi MUNGU wao Mtakatifu niliye hai juu MBINGUNI, hawataki kukubali kuzifuata amri kumi zangu mimi MUNGU wao Mtakatifu niliye hai juu MBINGUNI milele. Lakini ukimuuliza kila mtu katika Imani yake inayomsindikiza mtu kwenda jehanamu anakwambia nashika amri kumi, je, ni zipi? Ni zile nilizozishika mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu nikiwa msabato? Hapo ndipo ujijue kwamba wewe ni mtu unaye kwenda wapi au tabiri zangu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu zimetimia kwenu? Tabiri hizo ni za mwisho wa dunia asiye zijua tabiri zangu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu nilizowaonyesha wanadamu kupitia wanafunzi wangu, amuulize mwenzake atamkumbusha kwa sababu tabiri zote nilizo waonyesha wanadamu kupitia wanafunzi wangu zinamuhusu kila mtu. Tabiri kubwa iliyoenea dunia nzima ni watu kukosa upendo kwangu, watu wengi mpaka leo hata kama ningekuwepo duniani wangeungana kuniua na kueneza uongo na tamaa iliyowajaa na kuikataa sabato yangu na kujitenga mbali na upendo wangu mimi MUNGU wao Mtakatifu nili juu MBINGUNI.

Hakika shetani amewashikilia hapo watu wote ili mpotee naye katika moto wa jehanamu. Msitafute sababu, siku hiyo itakapofika mtakapoonyeshwa hukumu yenu kwa matendo mbalimbali uliyayafanya katika hii dunia kwa sababu msinge yasikia maneno yangu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu ninayowaambia kwa wakati huu mlionao wenye tabiri zangu zinazodi kwisha kila siku.
Ninawasikitikia watu wale waliosikiliza sauti za shetani zinazo waambia waache amri kumi zangu mimi MUNGU wao Mtakatifu, waiache Imani yangu mimi Mtakatifu BWANA YESU KRISTO. Je, utajibu nini utakapo jikuta mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu nitakapo kuambia sikujui? Kwa sababu wewe mwanadamu ndiye uliyeanza kutokunijua mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu. Je, iweje ikifika siku ya hukumu useme nakujua? Basi kama hunijui kwa mafundisho yangu niliyo yahubiri dunia mbele zenu mpaka leo, mkaniua mmeamua kunisaliti milele, hamkai katika neno langu bali mnakaa na shetani mnayachota mafundisho yake ya dhambi, mjielewe hivyo kuanzia sasa na milele. Mmeungana na shetani kuwa adui wa neno langu mimi MUNGU wenu Mtakatifu niliye juu MBINGUNI. Lakini mtu yule atakayesema leo nimeamua kubadilika na kunisubiri ili azipate ahadi zangu, mtu huyo nitamsamehe mara moja na nitampa ulinzi wangu ili awe mmoja wa wateule wangu watakao rukaruka siku ya mwisho nitakapo kuja. Na kila mtu anaye sema neno langu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu sio la kweli kwa mfano, hakuna haja ya kuzishika amri kumi zangu mimi MUNGU wake Mtakatifu eti mnasema ziliishia pale msabani, mtu huyo mfahamu kabisa sio wakuja huku juu MBINGUNI bali ni wa kwenda jehanamu.

Mtu anayelifuata neno langu ndiye aliyeupata wokovu, wokovu wangu haupatikani kwa mtu yeyote aliye lipinga neno langu na sasa watu mbalimbali duniani wanasema wao wameokoka kwa kuwa wamejazwa roho mchafu aliyewakwamisha katika maneno yangu mengi mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu, watu hao hawana upendo tena na watu wale wanaolifuata neno langu kwa sababu mtu anayelifuata neno langu anaraha sana duniani, asiyoifikia mtu yule aliyeamua kuniasi na kunisaliti kama alivyofanya shetani alipoipinga amri yangu mimi MUNGU wake Mtakatifu niliye juu MBINGUNI, Nikamfukuza na kumtenga kabisa na sasa anawakosesha mmo wanadamu, anawafumba macho wasione kitu chochote yaani watu wanaofanya dhambi wanajiona wapo katika njia nyembamba kumbe wameiacha njia hiyo nyembamba. Watu wanatembea wakiwa vipofu na mwisho wake wataingia katika shimo la moto wa jehamu. Wanafunzi wangu mimi Mtakatifu BWANA YESU KRISTO wakiwa katika chumba kwa ajili ya maombi nao wakiwa kumi na moja, walikuwa wamejaa hofu ya kunikosa mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu mkombozi wao pia kumkosa mwenzao Yuda aliyejiua kwa sababu ya kunisaliti mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu, nikakamatwa na kufa. Wanafunzi wale niliwaletea ROHO Mtakatifu ili awape nguvu, walijaa nguvu za ROHO wangu mimi MUNGU Mtakatifu niliye hai juu MBINGUNI, wakanena kwa lugha kama ilivyo andikwa. Lakini leo kuna baazi ya watu wanaoiga kujazwa ROHO kama wanafunzi wangu.wanafunzi wangu walinena kwa lugha inayosikika na kila mtu aliyewasikia. Je, na ninyi mnapojazwa na ROHO wangu mimi MUNGU Mtakatifu, mnasikia kwa lugha? Kama hamsikiki, kwa nini msimwache huyo roho asiyeeleweka kwa mtu yeyote, mkaamini yule ROHO Mtakatifu aliyewajaza wale wanafunzi wangu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu? ROHO Mtakatifu anakuwepo kwenu kwa kazi nyingine ambayo nikuwahimiza mshike amri kumi, kuwakumbusha muache dhambi kwa sababu ROHO Mtakatifu hana kazi moja na mnapoendelea kujifanya mnanena kwa lugha mnawaudhi watu kwa kusikia makalele yasiyo eleweka na huku mkiwa hamshiki amri kumi na wala si wasabato, mnaniudhi pia mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu mkombozi wenu. Yaani mmeiacha Imani yangu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu. Je, mnanionyesha dhambi kwa kuchagua mnayoyapenda? Yaani mnaniringia mkisema hata kama tumevunja amri kumi na hatuna Imani yako BWANA YESU KRISTO Mtakatifu, tunaweza kufanya vyovyote na watu wengi wakatufuata. Angalieni sana ninachukia sana mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu, mnapoiga kujazwa huko kwa dhambi na kwa sababu hata ingia juu MBINGUNI endeleeni kufanya hizo fujo. Lakini watu walioamua kunifuata mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu watajazwa ROHO Mtakatifu wakiwa katika raha watakayoifikia hapa juu MBINGUNI yaani hata ukiachiwa uzungumze tu lugha yako wewe, mzungu ataelewa, heri yao watu hao msisumbukie jambo msilo liweza, waambieni hata hao wanaofanya makosa hayo wasiendelee kukosea. Mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu niliye juu MBINGUNI ninamtuma Mwonaji wangu kwenu, awaonye muache dhambi zenu. Watu wengi waliojaa duniani hivi sasa wamekubali kuongozwa na shetani, wanafanya uzinzi, ndoa zao ni uzinzi. Shetani anawaongoza kufanya matendo mbalimbali, wanazikana amri zangu mimi MUNGU wao Mtakatifu, wanaikana hata Imani yangu mimi MUNGU wao Mtakatifu wanaongozwa kufanya mambo yote ya shetani. Hapa duniani matendo yenu yananichukiza, nitawaonya ili niwahubiri kwa mara ya mwisho. Watakao nisikia watu wachache watabatizwa na kujiweka tayari kwaajili ya safari ya kuingia katika ufalme wa MBINGUNI.

Kwa hiyo usije ukaona mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu ninakuonya ukashangaa niko kazini, ninafanya kazi na ninyi mfanye kazi, silahumiwi na mtu, kama ninyi ambavyo hamtalaumiwa na mtu. Watakaotaka kujua waambieni waache dhambi wakae hapa wanisikie mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu, Maisha yao yanusurike kwenda jehanamu, maonyo hayo yatawaonya wasabato wenye mioyo migumu kuamini maneno yangu na watu wa makanisa yote yaliyo jaa duniani, maonyo yangu yatawafuata mpaka makanisani kwao. Mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu nasema, sitawatuma MALAIKA watakatifu kuifanya kazi hiyo bali nitaifanya mimi mwenyewe. Na safari ya kuhubiri neno langu na watu kupata maonyo yangu itakuwa ni safari fupi ili wateule waliopatikana wasipotee tena. Basi hakuna mtu asiyejua kazi yangu mimi BWANA YESU KRISTO Mtkatifu ninapo ichukia dhambi. Maonyo ninayoyaleta kwenu ni ya aina gani? kinachotakiwa ni kukubali kuacha dhambi ili yasikupate maonyo yangu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu. Watu wa leo wamejaa dharau sana, bila kuwaonya hawawezi kutulia na kusikilia neno langu. Jirani yako au kwako ulipo ukimwona mtu ameonywa, mwambie asikilize neno langu na aache dhambi. Watu wengine watakapoonywa na watakapokujua wewe Mwonaji upo na watakukimbilia kujisalimisha na utawafafanulia kwanini wanapata mateso? Na watakaokuwa na kiburi watakufa. Nimewaweka duniani ili mnitukuze mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu niliye hai juu MBINGUNI na mniabudu mimi BABA yenu Mtakatifu niliye hai juu MBINGUNI, siku ya sabato, badala yake mnamtukuza shetani anayewadanganya na mnamuabudu shetani. Hapo ndipo wivu wangu mimi MUNGU wenu Mtakatifu niliye hai juu MBINGU ulipo na hapo ndipo hasira yangu mimi MUNGU wenu Mtakatifu niliye hai juu MBINGUNI ilipo.

Myajue hayo mashindano yapo kwa baadhi ya watu. Matendo yako unayoyafanya yako katika makundi mawili lakini sitaki watu wangu mjitolee kufa katika mkundi hayo mawili lakini sitaki watu wangu mjitolee kufa katika moto wa jehanamu wakati huu wa mwisho wa dunia, hivyo ndivyo kazi itakavyofanyika. Watu wengi wataogopa kwa sababu itafanyika ikionekana wazi kuwa watu wanalazimishwa sio kwa hiyari yao kulisikia neno langu kwa sababu wakati wangu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu umekwisha, watu wote watakao sema kuwa mwisho wa dunia haupo wataaibika sana. Mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu napenda muelewe kwa kuuleta kwenu wakati huo, nitawaaibisha watu wengi sana ambao walikuwa hawataki kukubali kwamba mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu ninaweza nikafanya kazi na mwanadamu niliyemfanya kuwa nabii, wataaibika na watashangaa sana. Wengine watajiunga muwe pamoja nao, wengine wataaibika wakisubiri kwenda jehanamu.

Nimekaa kimya mno mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu, watu nao wamejisahau wameamua kupotea katika neno langu. Wasabato walioko duniani hupotea sana, hao wengine kabisa wapo gizani. Lakini watakapojua siri ya maonyo yangu ni kuisikia HABARI NJEMA ya ufalme wa MBINGUNI, ninayo wapa kupitia Mwonaji wangu, kwa hiyo watu watakaa wakilishika neno langu na nitawaepusha na kifo kwa sababu kifo kitawapata watu wale wanaong’ang’ania kufanya dhambi. Lengo langu mimi Mtakatifu BWANA YESU KRISTO mwozi wenu niliye juu MBINGUNI, wazungu warudi washike Imani yangu wawe wasabato, wahindi warudi washike Imani yangu wawe wasabato, wajerumani warudi washike Imani yangu wawe wasabato, waarabu warudi washike Imani yangu wawe wasabato, wasomali warudi washike Imani yangu wawe wasabato, waafrika warudi washike Imani yangu wawe wasabato, wachina warudi washike Imani yangu wawe wasabato, warusi warudi washike Imani yangu wawe wasabato, wawe wasabato kama mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu wabadilike, wale walioogopa kuwa wasabato kama mimi Mtakatifu BWANA YESU KRISTO wabadilike na wakubali kutukanwa na kufanyiwa kila jambo baya kwa ajili yangu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu kwa sababu watakapo chukuliwa na MALAIKA watakatifu waingie huku juu MBINGUNI, waonekane wameingia huku juu MBINGUNI baada ya kupitia mateso, wametoka kwenye ile dhiki na nimewasafisha kwa damu yangu iliyomwagika pale msalabani. Kuanzia sasa mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu nazikemea injili zinazowadanganya watu na kuwapoteza maana injili inayohubiriwa sehemu nyingi duniani haizihubiri amri kumi wala Imani yangu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu, haihubiriwi. Injili kama hiyo haifai kusikika masikioni mwa watu kwa sababu inafanya watu wasiijue kweli yangu mimi Mtakatifu BWANA YESU KRISTO na injili inayoficha ukweli na inayohubiri uongo inahatarisha watu kwenda katika moto wa jehanamu. Nitawakemea watu wote wanaohubiri injili hizo zinazo wapoteza watu wengi kwenda jehanamu. Wakati nikifanya hivyo nitawabariki watu wale wanaohubiri injili ya kweli duniani. wanaohubiri amri kumi zangu mimi MUNGU wao Mtaktifu na Imani yangu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu. Kwa hiyo napenda mjue kwamba nitawaonya watu wote wanaohubiri injili ya uongo mmoja mmoja, hata kwa watu wanaosikiliza injili hizo za uongo nao wataonywa.

Mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu nasema wanadamu hamna shukrani, wanadamu hamna shukrani mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu nimewaonyesha upendo wangu wa kweli, nimewahubiri vizuri neno langu mimi MUNGU wenu Mtakatifu lakini leo hii ninyi manisaliti na kuhubiri kwa kuacha maneno yangu mkiulizwa kwa nini mmeacha mnasema yaligongomelewa msalabani yamepitwa na wakati. Siku zenu zimekwisha za kuhubiri uongo, nahitaji kuwapumzisha watu wasiendelee kusikiliza uongo wenu, nimewaahidi mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu nitalifanya jambo hilo. Kwa kuhubiri injili za uongo mmewafanya watu washindwe kuijua kweli yangu, mmeninyima mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu kuwapata wateule wangu duniani, mmeshilikiana na shetani kufanya kazi hiyo. Niwavumilie tu mpaka lini? Tangu sasa mfahamu kwamba ninawachukia na nitawapoteza wakati wowote mpaka mtakapojirekebisha, mkubali kuhubiri injili ya kweli, yaani muhubiri amri kumi watu wazijue, muhubiri Imani yangu mimi Mtakatifu BWANA YESU KRISTO watu waijue, mkifanya hivyo mtapona.

Nitayatimiza yote niliyoyasema mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu kuanzia sasa. Ole wake mtu yule atakayepata maonyo nitakayoyaleta mimi mtakatifu BWANA YESU KRISTO atajuta ni heri asingezaliwa duniani. Watu hawataki kujifunza neno langu, wamejaa dharau na kujiona wanaweza kufanya jambo lolote mbele zangu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu kwa makosa makosa. Muda mrefu nimenyamaza na nikiwaangalia na hamkutaka kujirekebisha lakini sasa nitawaadhibu, kwa sababu ninataka kuwahubiri upya. Bila kuwapa maonyo hamuwezi kunisikiliza mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu. Pazeni sauti za vilio kwenye nyumba zenye watu wenye viburi, vinavyofanana na shetani. Kila mtu atakayeingia katika kanisa lake lililoacha Imani yangu atalia, hilo ni onyo langu litakalowafuata makanisani watu wote mlioiacha Imani yangu. Atalia kiongozi, watu wengine mtaomboleza kwa sababu zamu yenu imefika na ninyi kuomboleza, lakini kwa sababu onyo langu litaenea sana mtakuwa mkilia huku mkifikilia kuwa mmenikosea nini mimi MUNGU wenu Mtakatifu niliye hai juu MBINGUNI? Mambo hayo yatakayotokea duniani kuanzia sasa yatawashangaza sana. Lakini lengo langu mimi MUNGU wenu Mtakatifu niliye hai juu MBINGUNI nikuwasaidia baadhi ya watu wasiwe ni watu wanaopotea katika moto wa jehanamu. Maonyo yangu ni ya kuwaokoa watu wachache, watakapo hubiriwa na kuijua kweli, waiache Imani ya shetani, mkae mkilijua hilo. Kuanzia sasa msishangae kusikia ndugu zenu wamekufa wanaoabudu katika Imani za shetani kwa kuwa mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu niko tayari kufanya kazi hiyo kuanzia sasa. Kama mkisema tuko nyumbani hapa duniani, hakuna haja ya kwenda sehemu nyingine, maana yake mkotayari kufanya dhambi ili mwende jehanamu, lakini kama mkisema hatujafika nyumbani kwenye makao yetu yapo juu MBINGUNI, mjitahidi sana kuacha dhambi, kwa sababu mnaikumbuka ahadi yangu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu niliyowaahidi siku moja nitakayokuja duniani nitawachukua muingie huku juu MBINGUNI. Kwa sababu kuna makao mengi, kwa hiyo angalieni mnapofanya dhambi. Wanaowazia ufalme wa MBINGUNI na wanaoamua kuacha dhambi duniani ni watu wachache sana. Mtu yeyote anayekubali kuniamini mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu na kunifuata ni mtu ambaye anafanana kama wanafunzi wangu walivyoniamini wakanifuata, wakishika amri kumi, wakishika Imani yangu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu yaani wakiwa wasabato. Lakini kama mtu haniamini mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu kama wanafunzi ukashika amri kumi zangu mimi MUNGU wako Mtakatifu na ukashika Imani yangu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu ukiwa msabato duniani, kama unasema unaniamini bila kufuata hivyo, Imani yako inapingana na mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu. Nilijua kuna watu ambao watakuwa na Imani zinazopinga na Imani yangu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu, nikawaagiza wanafunzi wangu nikawaambia, enendeni ulimwenguni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu mkiwabatiza kwa jina la BABA na MWANA na la ROHO Mtakatifu na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Inaonyesha watu wengine wamekataa kuwa wanafunzi wangu, hawataki kufundishwa ili wawe wanafunzi wangu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu, sasa duniani wamekuwa wengi wanajiandaa kuingia na shetani katika moto wa jehanamu kwa sababu ya kuwa na kiburi. Ubarikiwe kwa kunisikia mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu, wewe ukabari kuwa mwanafunzi unayeshika amri kumi zangu mimi MUNGU wako Mtakatifu na uwe na Imani yangu mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu mpaka nitakaporudi siku ya mwisho wa dunia nikukute ukifanya hivyo ili nikuchukue uingie juu MBINGUNI. Ubarikiwe kwa kunisikia mimi BWANA YESU KRISTO Mtakatifu niliye hai juu MBINGUNI katika kiti changu cha enzi.
Luka19:26-27
 
Back
Top Bottom