Neno La Leo: Ya Dodoma Na Fikra Za Kikomamanga...

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Naiona hatari iliyo mbele yetu. Kuwa tusipokuwa na umakini, itikadi zitakufa.
2.jpg

Kwamba tumeanza kuwa na viongozi kwenye vyama wasio na misingi ya kiitikadi. Chama ni itikadi. Chama kisicho na itikadi inayoisimamia ni sawa na chama chenye moyo dhaifu. Hakitakuwa na miaka mingi ya kuishi.

Chama makini ni lazima kisimamie itikadi na sera zake, hata kama kitalaumiwa vipi.

Mimi si mwanachama wa Simba, lakini, ni mpenzi wa Simba tangu utotoni. Kwa nia ya kujenga, naweza kuishutumu klabu yangu na hata kupingana na viongozi wa Simba, lakini, kamwe, siwezi kutoa huku nikijua, kuwa ni siri za Simba kimikakati, na kuwapa watu ninaojua fika watazitumia kuifanya Simba ishindwe. Sidhani kama MwanaYanga wa kweli anaweza kufanya hivyo pia. Hata kwenye mpira kuna itikadi na misingi ya kufuatwa.

Mwanafalsafa John Rawls anasema, hata kama utakalo ni haki yako ya asili, lakini, kama hilo utakalo halina faida kwa walio wengi, basi, si haki yako kulifanya.

Katika muktadha huu wa John Rawls, kuna kinachoitwa ' Collective Leadership'. Mnaweza, kama viongozi, kujifungia na kupingana kwa hoja, hata kwa kutukanana. Lakini, mwisho wa siku, lazima mtoke na maamuzi ya pamoja.

Wengi wakishinda yanabaki kuwa ni maamuzi ya wote ikiwamo ya waliopingana nayo kwenye mjadala wa ndani. Ukitoka nje na kusema mimi simo kwenye kilichoamuliwa, basi, sentesi ya pili ni ya ' najiuzuru'. Hapo utakuwa umelinda heshima yako kama kiongozi.

Katika kuadhimisha miaka kumi ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi, CCM na miaka 20 ya Azimio la Arusha, Hayati Mwalimu Julius Nyerere alikubali kufanya mahojiano ya kipekee na ya aina yake na Mhariri wa gazeti la Uhuru. Huo ulikuwa ni mwaka 1987.

Katika mahojiano yale, Mwalimu Nyerere, akiwa mwenyekiti wa CCM, hakusita kutamka bayana, kuwa Chama alichokuwa akikiongoza kilikuwa na kasoro na mapungufu mengi.

Mwalimu aliona kupungua kwa moyo wa kujitolea. Aliona dalili za kupungua kwa maadili ya uongozi. Mwalimu aliona mioyo ya kimamluki ilivyoanza kuingia na kuenea ndani ya CCM na nchi yetu. Hayati Mwalimu Nyerere alifikia kumtamkia mhariri yule wa gazeti, kuwa;

“ Tumewapa uongozi watu wasiofaa. Nadhani wengi ndani ya Chama tumeanza kuutambua ubovu huu. Hatua ya kwanza ya kutibu maradhi ni kuyatambua.” Alitamka Mwalimu.

Maggid Mjengwa.
 
Mkuu leo umeandika kwa hekima na busara sana, hujaonyesha ukada wa ccm, hongera sana, ukiendelea hivi nitakuwa nachangia mada zako, mimi binafsi nimependezwa na hatua zinazochukuliwa na ccm kujisafisha
 
Ukitofautiana na mtakatifu chagua moja kati ya mawili... Ufukuzwe uishi au ugome upotezwe..!!
 
Mkuu leo umeandika kwa hekima na busara sana, hujaonyesha ukada wa ccm, hongera sana, ukiendelea hivi nitakuwa nachangia mada zako, mimi binafsi nimependezwa na hatua zinazochukuliwa na ccm kujisafisha

Asante,
Niseme tu, wengi siku hizi wanaingia kwenye vyama kufuata vyeo vya uongozi na maslahi binafsi yenye kuendana na vyeo hivyo. Hawaingii kwenye vyama kwa minajili ya kuwatumikia wananchi hata kwa kujitolea.
 
Walishajivuaga magamba sijui wakabakia na nini na hiki cha leo ni transition ya nini tena?
 
Mkuu leo umeandika kwa hekima na busara sana, hujaonyesha ukada wa ccm, hongera sana, ukiendelea hivi nitakuwa nachangia mada zako, mimi binafsi nimependezwa na hatua zinazochukuliwa na ccm kujisafisha
Hata mimi nimeshangaa.
 
Back
Top Bottom