Neno la Leo: Enyi Walimu 'Watakatifu'...

Neno la Leo: Enyi Walimu 'Watakatifu'...

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,250
Ndugu zangu,

Umezinduliwa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa ( MMMS) kwenye Sekta ya Elimu. Kwa kimombo unaitwa ' Big Results Now' ( BRN).

Kwa lugha nyingine ni mpango wa ' Mavuno Makubwa Sasa'. Na mkulima anayetarajia mavuno makubwa ya mahindi ni lazima awe amefanya makubwa matatu; kulima shamba lenyewe, kupanda mbegu bora na kulipalilia vema shamba lake.

Na jana nilipokuwa nikifuatilia ' live' TBC1 uzinduzi ule wa ' Mavuno' makubwa sasa nilijiuliza; Je, maofisa wale wa elimu wa mikoa wenye kula kiapo hadharani kuhakikisha ' mavuno' makubwa yanapatikana SASA walielewa hasa changamoto ya jukumu walilotwishwa la kuhakikisha tunapata ‘mavuno' makubwa sasa.

Maana, kiapo kile kingeweza pia kuwa ' ungamo' la dhambi tuzitendazo zenye kupelekea kila mwaka tupate ' mavuno' hapa na wakati mwingine kuambulia debe mbili tatu tu kwenye ' mavuno' yetu ya elimu.

Niaonavyo, sambamba na mpango huu ulioandaliwa kwa dhamira njema kabisa, bado kunahitajika Mjadala Mkubwa wa Kitaifa kujadili namna ya kuinasua elimu yetu kutoka hapa tulipo.

Maana, inabaki, kuwa dhumuni kubwa la maisha ya mwanadamu ni kufanya juhudi za kutafuta namna ya kuyaelewa mazingira yake na hivyo kupiga hatua za maendeleo. Na juhudi hizo za mwanadamu ndicho chenye kujulikana kama ' Elimu'. Naam, mwanadamu anapaswa aitafute elimu, hivyo basi, maarifa.

Na shule yaweza kutafsiriwa kuwa ni ' Maabara' ambamo hutengenezwa ' chanjo' ya maradhi ya kimaisha kwa mwanadamu. Wale wenye maarifa na busara za kuandaa ' chanjo' hiyo ndio wanaoitwa walimu.

Maana, shule ni mahali pa kujifunzia, ambapo yote yenye kuhusiana na maisha ya sasa na hata yajayo hufundishwa. Ni mahali ambapo hupatikana tafsiri za vitu na matukio katika jamii. Ni mahali ambapo, mbali ya mambo mengine, mwanafunzi anapaswa kusaidiwa kuweza kupata maarifa ya kujitambua na kuyatambua mazingira anamoishi.

Twaweza kabisa kusema, kuwa shule ni mahali pa ' ibada'. Na ' viongozi watakatifu' wenye kupaswa kuongoza ' ibada' hizo ni WALIMU.

Hivyo, enyi walimu ' watakatifu' , mnapaswa kuianza sasa kazi ya kuitambua nafasi yenu katika jamii. Vile vile, kulitambua jukumu lenu, vinginevyo, Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa yumkini yaweza kuwa sawa na mkulima anayesubiria ' mavuno' makubwa sasa ilihali shamba alilolima ni dogo. Amepanda mbegu dhaifu na ameshindwa hata kupalilia shamba lake.

Ni Neno La Leo.

Maggid,
 
sasa umeandika malalamiko,au mapendekezi...? au umeona siku isipite bila na wewe kupost??
 
Kila mtu awajibike kwenye nafasi yake yote npyanawezekana.
 
BRN utashindwa hata kabla haujaanza.Utatumia lugha gani kumshawishi mwalimu aliejikatia tamaa atekeleze huu mpango?Mshara unaisha tar2,hajalipwa madai yake yote kama masomo,matibabu na hata malimbikizo ya mishahara anasubiri miaka mitano!Hapa unahitaji mwalimu ashuke toka mbinguni labda ndiye ataweza kutekeleza hiyo Small/little results now.FULL STOP
 
hata mimi sielewi hapa
 
Hivyo, enyi walimu ' watakatifu' , mnapaswa kuianza sasa kazi ya kuitambua nafasi yenu katika jamii. Vile vile, kulitambua jukumu lenu, vinginevyo, Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa yumkini yaweza kuwa sawa na mkulima anayesubiria ' mavuno' makubwa sasa ilihali shamba alilolima ni dogo. Amepanda mbegu dhaifu na ameshindwa hata kupalilia shamba lake.

Hii sehemu ilifaa sana kuambiwa serikali yako 'sikivu' na siyo walimu.

BRN utashindwa hata kabla haujaanza.Utatumia lugha gani kumshawishi mwalimu aliejikatia tamaa atekeleze huu mpango?Mshara unaisha tar2,hajalipwa madai yake yote kama masomo,matibabu na hata malimbikizo ya mishahara anasubiri miaka mitano!Hapa unahitaji mwalimu ashuke toka mbinguni labda ndiye ataweza kutekeleza hiyo Small/little results now.FULL STOP

Ni kweli kabisa mkuu, nahuu utashindwa kama ile mingine waliyoianzisha bila kufanya study ya kutosha kwanza.....Kabla ya kujaza mbwembwe kwenye BRN walipswa kutuambia ni wapi ilipofia KILIMO KWANZA? Au ndo uliishia kuleta ma power tillers ili tubebee maji na matofali ya kuchoma huku vijijini!

Sidhani kama maslahi ya mwalimu wanayemtaka atekeleze huo mpango kama yamekumbukwa......Tusubiri tuone!
 
Wanasiasa wa Tanzania ni wataalam sana ktk kuanzisha kaulimbiu wasizozitekeleza kwa vitendo kisha zinabaki kua nyimbo, ngonjera ama maigizo. MKUKUTA, MKURABITA, MEMKWA, SHAMBA DARASA, SEMINA ELEKEZI, nk nk na leo BIG RESULT NOW!

Si vibaya kuanzisha kaulimbiu lakini ni vema kutathmini namna ya utekelezaji utakavyokua kama vile kuwaelimisha wadau husika kwa kiasi cha kutosha, kuwawezesha kifedha na kimbinu ili kuleta matokeo tarajiwa kwa kiwango kikubwa.

Tusubiri hiyo kaulimbiu ifanye kazi pasina kuboresha miundombinu pamoja na maisha ya walimu ambao ndio wadau wakuu ktk sekta ya elimu.
 
maggid hatuhitaji hizo teminoloji sijui "BRN " na wajukuu zake,Tuna wizara iliyosheheni wataalamu na idara kibao.Hizi program ni kichaka cha ulaji tu wakati wizara ikitimiza majukumu yake vizuri hakuna litakaloshindikana.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu,

Hivyo, enyi walimu ‘ watakatifu’ , mnapaswa kuianza sasa kazi ya kuitambua nafasi yenu katika jamii. Vile vile, kulitambua jukumu lenu, vinginevyo,Tusitegemee mavuno makubwa kutoka kwa wlimu Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa yumkini yaweza kuwa sawa na mkulima anayesubiria ‘ mavuno’ makubwa sasa ilihali shamba alilolima ni dogo. Amepanda mbegu dhaifu na ameshindwa hata kupalilia shamba lake.

Ni Neno La Leo.

Maggid,

Tusitegemee mavuno makubwa kutoka kwa walimu (watendaji shambani) ambao wametelekezwa na mwajiri wao (mwenye shamba).
Tusitegemee mavuno makubwa kutoka kwa wlimu kwa mshahara unaoshindwa kuwafikisha hata tarehe 10 ya mwezi.
Tusitegemee mavuno makubwa kutoka kwa wlimu ambao maisha yao yametawaliwa na mikopo yenye riba zisizoelezeka.
Tusitegemee mavuno makubwa kutoka kwa wlimu ambao sauti yao haisikiki, na kila wakijaribu kuipaza, serikali inatumia mabavu kuwanyamazisha.
Honestly BRN is impossible from this sector because the government has abandoned teachers (the vital part for the so called BRN)
Serikali itegemee
BAD RESULTS NOW from teachers coz Haiwezi kukusanya wakati haijatawanya.
 
Ni ukweli usiopingika kuwa mpango wa "Matokeo makubwa sasa " katika sekta ya elimu ni ndoto ambayo haiwezi kufikiwa kwa Maafisa elimu kula viapo wakati si wanaofundisha. Wanaweza kuwa wamefurahi kula viapo kwa sababu wametengenezewa ulaji mkubwa maana itabidi watumie sasa vifungu vya fedha za kununulia vitabu kwa ajili ya matumizi yao binasfsi kwa maana ya kuwatembelea walimu katika shule na kuwaaapisha kama ndio utekelezaji wenyewe wa mpango huu.
Ni nadra sana kwa nchi hii kuwa na watu wanaoweza kukubali kuwa elimu imeshuka kwa sababu walimu hawana morali ya kufanya kazi na hasa vijini. Mazingira ya mjini angalau unaweza kukuta walimu wanawajibika kwa sehemu lakini si kwa kujituma kwa maana ya kumfuatilia mwanafunzi na kumsaidia katika nyanja mbalimbali anazooonekana kukwama katika ujifunzaji wake.
Kwa mpango huu na hasa walimu kutohusishwa kikamilifu,mavuno hasi yatarajiwe kma tatizo lenyewe halitatafutiwa majibu thabiti na ya kisayansi na si kisiasa kama inavyofanyika sasa.
 
Kwa malengo haya:-
i) Ufaulu katika elimu ya msingi unaongezek
a kutoka 31% hadi kufikia 60%;

ii) Ufaulu katika shule za sekondari unaongezeka kutoka 43% hadi kufikia 60%; na

iii) Mwanafunzi wa Darasa la Pili ataingia Darasa la Tatu akiwa anafahamu Kusoma, Kuandika na Kuhesabu

Lazima walimu waibe mtihani au wawafanyie wanafuniz mtihani ili kufikia ufahulu huo. Lazima kuwe na mdondoko mkubwa wa wanafunzi ili kuwaondoa shule wale wasiojua kusoma na kuandika.
 
Mhh...ni masikitioko makubwa sana...yaani nchi yetu imekuwa nchi ya kuiga kila kitu na kutaka kuki - implement bila hata ya kufanya ka - utafiti kadogo.

Nakumbuka Ndugu JK alipata mpango huu kutoka Malyasia mwaka jana, na kama sijakuosea mwaka huu watu wa Malyasia wamefika hapa kutoa semina elekezi kwa watz. Lakini cha kushangaza, waalimu hawajawezeshwa kwa lolote, na wala hawajaelezwa what exactly have to be done, zaidi ya kurundikiwa rundo la form za kujaza na remedial teaching juu. Ni kama vichekesho fulani hivi.

Hakuna ambacho kinawezekana katika mpango huu bila ya kumuandaa mwalimu anayetakiwa kutekeleza ili kupata BIG RESULTS NOW, lakini watawala wao wanawezeshana kwa semina na posho kibao lakini mwalimu anasisitizwa kuandaa lesson plan, scheme of work, log book na sasa kuna maform kibao ya kujaza bila kujali ki uhalisia kama amefundisha.

Kweli serikali yetu inahangaika sana...nimeamini...MFA MAJI HAACHI KUTAPA TAPA...nothing will be possible kama Mwalimu ataendelea kupuuzwa na kuachwa kaitka mipango kama hii....!!!
 
Tusitegemee mavuno makubwa kutoka kwa walimu (watendaji shambani) ambao wametelekezwa na mwajiri wao (mwenye shamba).
Tusitegemee mavuno makubwa kutoka kwa wlimu kwa mshahara unaoshindwa kuwafikisha hata tarehe 10 ya mwezi.
Tusitegemee mavuno makubwa kutoka kwa wlimu ambao maisha yao yametawaliwa na mikopo yenye riba zisizoelezeka.
Tusitegemee mavuno makubwa kutoka kwa wlimu ambao sauti yao haisikiki, na kila wakijaribu kuipaza, serikali inatumia mabavu kuwanyamazisha.
Honestly BRN is impossible from this sector because the government has abandoned teachers (the vital part for the so called BRN)
Serikali itegemee
BAD RESULTS NOW from teachers coz Haiwezi kukusanya wakati haijatawanya.
Huna haja ya mkakati huo. Unataka matokeo makubwa? Wahamasishe (motivate) walimu tu. Utakuwa umemaliza 70% ya tatizo.
 
sasa umeandika malalamiko,au mapendekezi...? au umeona siku isipite bila na wewe kupost??

Hakika ndio hivyo ameona siku inakaribia kumalizika na haja post chochote ikabidi atupie hii kitu incomplete haraka. ameishia kwenye introduction!
 
Back
Top Bottom