Neno La Leo: Afrika Hatugombanii Matambiko...

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Kuwasha moto ni jambo jepesi sana, lakini, kuuzima moto, yaweza kuwa ni kazi ngumu sana.

Ona, moto ulioanza kwenye nyumba moja ya nyasi kijijini, waweza kusambaa haraka na hata kuteketeza kijiji kizima. Na tangu utotoni tumetahadharishwa hatari ya kucheza na moto. Naam, binadamu usicheze na moto, labda iwe kwenye mazingaombwe.


Sisi sote ni ndugu, na hii ni Nchi Yetu. Hatuna haja ya kubaguana kwa misingi ya ukabila, dini na rangi. Tuna historia ya kujivunia. Ni historia yetu wenyewe. Kinyume na baadhi yetu wanavyofikiri au wanavyotutaka tufikiri, historia yetu haikuanzia enzi za Mwarabu , Mjerumani au Mwingereza. Historia yetu haikuanzia enzi za TANU wala Afro Shiraz.

Na dini hizi za kimapokeo zinazotufanya sasa tufarakane zimekuja na kuzikuta dini zetu za asili, na bado tunazo. Na hakika, Afrika hatugombanii matambiko. Afrika kila ukoo una tambiko lake, hivyo basi, dini yake. Kamwe hutasikia Waafrika wanagombania matambiko. Hutasikia Waafrika wakigombana kwa tofauti za matambiko yao.

Na sisi ni Waafrika. Hii leo mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa kuwafanya wachinjane ni kwenye kwenye tofauti zao za imani hizi za kimapokeo; Uislamu na Ukristo.

Naam, tusifike mahali tukagombana kutokana na tofauti za imani ama dini ambazo wala si za asili yetu. Imani au dini ambazo, kama ilivyo dini zetu za asili, nazo zinatutaka wanadamu tuishi kwa amani, upendo na maelewano.

Na hilo ndilo Neno la leo.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
0788 111 765, 0754 678 252
 
Vyema mkuu Maggid:
Ni kweli, kila koo ilikuwa na matambiko yake binafsi, lakini hayakuleta mafarakano ila tu mpumbavu anapokiuka kwa makusudi miiko!
SWALI: KWANINI HATUKUGOMBANIA MATAMBIKO?
Hapa ndipo penye matatizo na imani zetu za sasa. Matambiko yetu ya Kiafrika, licha ya kufanywa maeneo tofauti tofauti, kama vile makaburini, kwenye miti mikubwa, mapangoni, milimani, n.k. Matambiko yote yalijengwa kwa msingi mkuu mmoja uliofanana kote, iwe kwa atambikaye mtini, ama kaburini, ama vichakani, ama mapangoni, n.k. Matambiko yote yalifungwa na msingi huo mkuu na huo ukaleta MANTIKI ambayo inapokuwepo haiwezi KUKINZANA KAMWE, nao ni UTU!
Kila tambiko, liliongozwa na MANTIKI-yaani UTU! UTU+UTU = KUFIKIRIANA/MAELEWANO!
Hiki ndicho kilichokosekana katika Ukristo na Uislamu, milele na milele haitatokea Muislamu kumfikiria Mkristu vivyo hvyo mkristo kwa muislamu! Ukristo wa sasa umesimama juu ya msingi wa HULKA, sawa na kwa Uislamu! Kila imani inapigania UKUU/KUJIKWEZA! Mwisho wa siku ni mapambano yasiyokwisha! Ni KUJIDANGANYA kusema imani hizi zivumiliane! HALIPO!
Na huo ndio utofauti wa Matambiko ya Kiafrika, na haya (viini macho) tuyaonayo leo yaliyojaa ushetani na uozo kila kona!
Tulienda kufanya matambiko si kwa kila kaburi/babu/mzimu, ila ni kwa wale waliosadikiwa kuishi WEMA, tukiamini kwamba Mungu ni Roho, na roho ni Ukamilifu wa aidha WEMA(Mungu) ama UBAYA(shetani), hivyo hatukufuata mifupa ya mababu ila roho(wema waliokuwa nao) nayo ndio MUNGU! Makaburi za waliosadikiwa kuwa wabaya/waovu, yalisadikiwa kuwa na mikosi kwa kubeba ubaya ambao ni ukamilifu wa roho(tuliita shetani) tuliyatenga makaburi hayo, na hata watu walizuiwa kwenda. High Critical Thinking ilitumika kung'amua WEMA na UBAYA, tofauti na leo ambapo HISIA zetu ndizo zinazotumika kung'amua WEMA na UBAYA wa imani ama mtu! Matokeo yake ndio haya ya KUWINDANA, ni Upumbavu na Upunguani mkubwa!
Mungu wa kweli yupo kwenye UTU, msingi mkuu wa maisha ya MTU MWEUSI, sihuoni UTU kwenye imani zetu za leo!
Lets live War!
Live Logic!
Live Blood!
Live Battle!
Mungu wetu anaita sasa!
 
We are brainwashed to an extent that we can not believe even a single inch in ourselves,we have turned out to be worshipers of our own emotions,our deeds are those which appeal to our own attitude not even the so they call God
 
Back
Top Bottom