Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira nchini NEMC limeifungia kampuni ya El-hillal Minerals katika wilaya ya kishapu mkoani Shinyanga kuendelea na shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini ya Almasi kutokana na Mgodi huo kushindwa kufuata taratibu za uhifadhi na utunzaji wa mazingira katika eneo hilo.
Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi na kufikia hatua ya kufunga shughuli za Mgodi huo, afisa mazingira mkuu wa NEMC Dk Yohana Mton, amesema baraza hilo limebaini shughuli za uendeshaji wa mgodi huo zimeathiri kwa kiasi kikubwa viumbe hai na mazingira katika eneo.
Naye mwakilishi wa kampuni inayoendesha mgodi huo Bw Amour Nassor, amekili kuwa shughuli za mgodi zimesababisha uharibufu mkubwa wa mazingira lakini amesema kutokakana mgodi huo kuajiri watu wengi hivyo ameomba serikali kuwapa muda wa kufanya marekebisho yanayohitajika.
Chanzo: ITV