Nelson Mandela Was On US Terrorist Watch-List Until 2008


Nimezisoma vizuri mkuu, na nimezipitia kwenye vitabu vingi kiasi. Sina shaka kuhusu umwamba wa Mandela, na wala sina shaka kuhusu ushujaa wake, lakini hata Yesu ni shujaa lakini ana mapungufu yake!..Unaelewa kwamba kulikuwa na mikutano mingi ya siri kati ya mandela na wawakilishi wa apartheid regime miaka michache kabla ya kuachiwa kwake? Unadhani ni nini kilizungumzwa?
 

Huo umwamba ndiyo unaofanya hata wale waliomtesa wamuheshimu.
Kuhusu mikutano ya siri sijui walizungumza nini kwakuwa ilikuwa siri. Ila kama unafahamu tueleze.
 
Lakini mwaka 2004 Bush alimpa tuzo Mandela White house
 

Mkuu bora na wewe umeliona hilo, mi kuna kipindi nishawahi kufikiria kuwa huyu siye Mandela...
Haiwezekani mtu aliyekua anaitwa Madiba (Mtata) kufanya maamuzi ya kipuuzi kiasi kile..
Mi ndio maana nasema hata pa kuanzia alikua hana..
 
Mkuu bora na wewe umeliona hilo, mi kuna kipindi nishawahi kufikiria kuwa huyu siye Mandela...
Haiwezekani mtu aliyekua anaitwa Madiba (Mtata) kufanya maamuzi ya kipuuzi kiasi kile..
Mi ndio maana nasema hata pa kuanzia alikua hana..

Maamuzi gani hayo ya kipuuzi aliyoyafanya? Specify kidogo tuone upuuzi wake, yawezekana wengine hatuujui.
 
Alikuwa mbaya kupindukia. Aliwasamehe makaburu akashindwa kumsamehe Winnie Madikizela Mandela. Hii pia ni aina ubaguzi au inferiority complex kwa wazungu. Kosa ni kosa, kama alikuwa na moyo wa msamaha angemsamehe mke wake. Kuwasamehe wazungu ni kwa sababu ya ukweli kwamba aliwaogopa na akaona hawezi tene kuendelea kupambana nao.Hasira zake zikaishia kwa mnyonge wake Winnie. Ni mtu maarufu kwa dunia lakini dhaifu kwa familia yake mwenyewe. Amekwenda kinyume na charity begins at home. Naona watu wanaangalia upande mmoja
 
Hell No!!, i dont think so:tape:
ilikuaje alipokuwa rais je si angewageuka basi.. na hapa alishindwaje???
 

Naomba kukiri kuwa ninafahamu kiasi kidogo sana cha mgogoro kati ya wawili hao na sitaki kutia neno juu ya swala hilo ila naomba unisaidie, unaposema kuwa alishindwa kumsamehe unamaanisha nini, au alitakiwa kufanya nini ili ijulikane kuwa kamsamehe?
 
Hell No!!, i dont think so:tape:
ilikuaje alipokuwa rais je si angewageuka basi.. na hapa alishindwaje???

Hivi baada ya mateso yote yale, maisha ya watu wengi kupotea, wewe unadhani ni nini kilimsukuma awasamehe? Kumbuka kuna vikao vingi vilifanyika kwa siri kati yake na uongozi wa apartheid kabla ya yeye kuachiwa, unafikiri nini kilizungumzwa? Sina maneno na Mzee Madiba, katika situation aliyokuwapo hata mimi ningefanya hivyo tu, lakini aliwauza waafrika wenzake, tunayahitaji mashamba yetu!
 
Mandela na Winnie walikuwa wana ndoa, wazazi wa watoto wao wawili, lakini pia walikuwa wana chama cha ukombozi cha ANC. Mwaka 1998 Nelson alimtaliki Winnie. Hapana shaka kulikuwa mgogoro wa kifamilia. Mandela Nelson alishindwa kuuhimili kuusuhisha hata kusamehe hadi kifo chake. Alipaswa kuendelea kuishi naye hadi kifo kama biblia inavyotuasa kufanya. Kitendo cha kumtaliki mkewe kinaonyesha udhaifu kinyume kabisa cha anavyoelezwa katika vyombo vya habari. Ukumbuke Nelson, kutokana na harakati zake za kisiasa alimwacha Winnie akiwa na umri mdogo na familia changa akihangaika pasipokuwa na mzazi mwenzake. Hii peke yake ilikuwa ni adhabu. Leo anapata mafanikio anakula Graca na kumtupa aliyesaidia mafanikio yake. Nilisoma kwenye vyombo vya habari jinsi viongozi wa dini walivyojaribu kumsihi asimwacha Winnie, lakini hawakufanikiwa. Yesu aliwaambia watu walikuja kumshitaki kwake mwanamke malaya, 'ASIYEPATA KUTENDA DHAMBI NA AWE WA KWANZA KUMTUPIA JIWE MWANAMKE HUU
Naomba kukiri kuwa ninafahamu kiasi kidogo sana cha mgogoro kati ya wawili hao na sitaki kutia neno juu ya swala hilo ila naomba unisaidie, unaposema kuwa alishindwa kumsamehe unamaanisha nini, au alitakiwa kufanya nini ili ijulikane kuwa kamsamehe?
 

Them true hypocrites!
 

Mkuu, tuambie waliongea nini kwenye hiyo mikutano ya siri?
 
tunaheshimu hisia lakini huwezi fanyia kazi hisia, ikumbukwe kama ni hisia basi kila mtu anazo hisia zake.

vikao vingi??????aliachiwa lakini akawa rais, je iweje asiwageuke, alishindwa nini?
mandela alichagua njia sahihi zaidi, kwani ilihusu jamii nzima ya wanaafrika kusini bila kujali rangi zao. wazungu hawakuwa foreigners bali wenyeji pia na raia halali wa afrika kusini.
tafakari nchi yenye jeshi (vita+polisi)la wazungu peke yao, ajira wanatoa wao,uchumi wanamiliki wao, na katiba inawa-favour wao. lakini rais tu ndiye mweusi(mandela), ungefanya nini? je ungewaa kulipa kisasi kwa ajili ya wazalendo waliochini ya mfumo?. je utawala wako ungedumu?
 
hii haina tofauti na hap kwetu kwania akina serikali ya TZ wanamlilia Mandela wakati wao wanawaua wapinzani wao na kuwang'oa meno bila ganzi.

huu wetu nao ni ubaguzi ambao Mandela alipigana nas sana kuutokomeza.
definately Yesssssssssss
 
Ukisoma historia vizuri utagundua pia hata wazulu si mahala pao kule south africa nao wanatakiwa kurudi kwao baada ya kuvamia south africa karne ya 9, si ajabu hata wewe utajikuta kwamba historia inakurudisha kwenu Nigeria na Cameroon au Sudan kama una asili ya Nilotes. Kwa kulijua hilo ndio maana Mandela akasema hivi "We are not anti-white, we are against white supremacy … we have condemned racialism no matter by whom it is professed."



 
Hell No!!, i dont think so:tape:
ilikuaje alipokuwa rais je si angewageuka basi.. na hapa alishindwaje???

lete ushahidi mezani kwamba kulikuwa na maongezi ya siri kati yake na serkali ya kikaburu
 
Hawa wakubwa wanatuzuga tu, mara nyingi inategemea wanachokitaka toka kwako.
 
lete ushahidi mezani kwamba kulikuwa na maongezi ya siri kati yake na serkali ya kikaburu
sina ushahidi wa maongezi ya siri, nachojua kulikuwa na makubaliano kati ya mandela na serikali ya kikaburu. hivyo siamini kuwa mandela alikuwa na siri yoyote isiyo na maslahi kwa wananchi wa SA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…