Necta na tcu wasaidieni hawa vijana wapate vyuo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Necta na tcu wasaidieni hawa vijana wapate vyuo

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by KIDUNDULIMA, Aug 17, 2011.

 1. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45

  Vijana ninaowazungumzia ni wale ambao TCU imewatangaza kuwa hawana sifa za kuchaguliwa kujiunga vyuo vikuu kwa vile hawa sifa kwa vile hawana credit tatu za O-level. Vijana hawa wengi wao ni wale waliosoma kwa taabu sana katika shule za Kata na wengine wakapata CIV-D; HIST-D; GEO-D; KISW-B; ENGL-C; PHY-F; CHEM-F; BIO-F; B/MATH-F: mwingine amepata CIV-D; HIST-C; GEO-D; E/D/KIISLAMU-F; KISW-D; ENGL-D; BIO-D; B/MATH-; na mwingine kapata CIV-D; HIST-D; GEO-F; KISW-C; ENGL-C; PHY-F; CHEM-D; BIO-F; B/MATH-D na wengine wengi amabao siwezi kuwataja. Vijana hawa waliruhusuwa na NECTA kufanya mitihani na kidato cha sita kwa sababu wengi wao walikuwa wamechaguliwa kujiunga na shule za serikali maana wangeenda shule za private wasingekubaliwa kufanya mitihani kwa vile hawana credit tatu. Kuna vijana ambao TCU wamewataja kuwa hawa wana sifa za kuomba na kuchaguliwa, baadhi yao kwa vile tu wana credit tatu za o-level baadhi matokeo yao ya O=level ni kama CIV-C; HIST-D; GEO-C; KISW-C; ENGL-F; BIO-F; B/MATH-F; na mwingine CIV-D; HIST-F; GEO-C; KISW-C; ENGL-C; BIO-F; B/MATH-F. Haya makundi ukifuatilia sana walio na credit tatu na wasiokuwa nazo ni kama sifia zao zinalingana na mara nyingine wasiokua na credit tatu kuwa na point nyingi zaidi katika ujumla wa masomo waliyofaulu (A=5, B=4, C=3, D=2, F=0). Sasa kama baraza waliwaruhusu vijana kufanya mitihani sijui kwa kigezo kipi kwa nini TCU wasiwaruhusu wajiunge na vyuo kama sifa za A level zinawaruhusu?
   
 2. Baba Collin

  Baba Collin JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ubabaishaji mtupu hapo.si mngewatangazia mapema wakatafuta utaratibu mwingine hata km ni diploma?
  Mmechelewa kuwapa majibu jm hawatapata vyuo huoni itakua kasheshe huku mitaani!
  Kibaya zaidi 2nd applicatin mmewatolea wachague vyuo ambavyo ada yake haishikiki hv kwel hizo ada na hizi shida huku uswahilini kunakusoma hapo?
  Too much politics!!?
   
 3. m

  mfukoz Member

  #3
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi ningeshauri hivi bado wanayonafasi kuna chuo kizuri ambacho nilipata kukitembelea baada ya kuona matangazo yake kiko pale ubungo Plaza kinaitwa MUGEREZI SPATIAL TECHNOLOGIES(MUST COLLEGE) hiki chuo kinatoa nafasi kwa vijana wote wa form iv na vi kwa kweli kile chuo ni kizuri kwani hata mimi baada ya kuona hizi siasa za TCU nikaona bora nitembele hicho chuo na kuona nikwanafasi gani kinaweza kumzaidia kijana wangu na kimesajiliwa na VETA ada yake ni laki 4 kwa term 3 kwa maanaya kila term laki nne,kwa hiyo bado nafasi wanayovijana tusikae na klalamika tujaribu kuangalia fursa nyingine zza vyuo kwa vijana wetu
   
 4. M

  Moesk Member

  #4
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  da ila lakini jamani wa kulaumiwa ni necta by da way kwani necta hawana uhusiano na tcu.sa waliwaruhusuje waende 4m five angali hawana hizo credit au ndo kujaza2 mashule yao da ina uma sana wanajamii
   
Loading...