MchukiaUonevu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 207
- 79
Ndugu wadau,
Ripoti ya tume iliyochunguza tuhuma dhidi ya upotoshaji wa matokeo ya mtihani wa somo la Islamic knowledge kidato cha sita mwaka 2012 inasikitisha. Tarrifa zilizotolewa na Naibu Waziri wa Elimu Ndg.Phillipo Mulugo kuwa tume ilijiridhisha kuwa kulikuwa na hitilafu kwenye mfumo wa computer inazua maswali mengi kuliko majibu. Matokeo ya uchunguzi huu yametoa taswira halisi ya Necta. Katika hali ya kawaida,makosa hufanywa na kila binadamu,lakini pia degree,frequency na mazingira ya kosa ni kitu kingine. Ni jambo ambalo haliingii akilini makosa yafanyike halafu chombo husika kikae kimya hadi watu waandamane ndio haki itolewe. Waislam wamelalamika miaka mingi sana juu ya baraza la mitihani kumezwa na mfumo unaowanyima haki wanafunzi wa kiislam na hata shule za kiislam. Lakini hawajawahi kupewa majibu zaidi ya kukejeliwa,kudharauliwa,na kuitwa majina mabaya. Leo serikali inakuja na majibu mepesi kuwa ni hitilafu ya computer,sijui formula iliyotumika kukokotoa nk. Haya sio majibu ya kutolewa na Waziri,kila mtu anafahamu computer hufanya kazi kutokana na instructions za binadamu. Huwezi kuingiza wrong formula halafu utegemee majibu sahihi,garbage in garbage out!. Tena cha kushangaza system imechagua somo la dini moja tu la "Islamic knowledge",somo lenye vigezo sawa na somo wanalofanya wanafunzi wa dini nyingine la "Divinity".
Hatuwezi kuridhika na majibu mepesi kiasi hiki kwa makosa ya kudhamiria kiasi hiki. Sensitive issues kama matokeo ya mitihani sio kitu cha kufanyia masihara. Hii kazi haifanywi na mtu mmoja,ni jopo la watu,tena wanaofanya kazi independently,na mwisho lazima matokeo yawe reviewed na watu makini. Iweje leo Waziri aseme ni kosa la Mkurugenzi mmoja. Hatuwezi kuridhika kwa kumfukuza kazi mtu mmoja,tunataka uozo uliopo Necta uondolewe,haki itendeke na tena haki ionekane kutendeka!
Tujiulize maswali haya.
1:Utaratibu wa Necta ukoje kabla ya kuchapisha matokeo ya mtihani.
2:Ikiwa hii si mara ya kwanza kwa Waislam kulalamika juu ya mfumo kandamizi uliopo Necta,ni hatua gani zilishachukuliwa ku-address uozo huo.
3:Kwa nini watu walewale waliolalamika miaka mingi juu ya mfumo kandamizi wamekuwa proved victims wa mfumo tajwa.
4:Kama wamekiri somo moja tu kuathirika na "hitilafu kwenye mfumo wa computer",tena somo ambalo hufanywa na wanafunzi wa dini moja tu,is there any validity of the results for the rest of the subjects?
Kwa majibu ya Ndg.Mulugo,matokeo ya kidato cha sita yanakosa uhalali wa kuitwa matokeo,na hasa kwa wanafunzi wa Kiislam(huu ni mtazamo wangu).Kuchapisha upya matokeo ya somo moja la Islamic Knowledge hakuniondolei hofu juu ya madhila wanayofanyiwa Waislam na shule za kiislam na baraza la mitihani. Hatuwezi kuamini kirahisi kuwa makosa yalifanyika kwenye somo moja tu,na hasa ikizingatiwa nature ya kosa lenyewe limekuwa "too selective".Tunatakiwa tujiridhishe beyond reasonable doubt kuhusu muundo wa Necta,ufanyaji kazi wake,watumishi wake,usahishaji mitihani,na uchapishaji wa matokeo ya mitihani.
Nawasilisha!