NECTA kuwasaka wenye vyeti bandia

Mkuu mbona hilo lilianza kufanyika miaka miwili iliyopita, wakati serikali ilipotoa agizo la uhakiki wa sifa za kila mwajiriwa nchini. Unajua kilichofanya zoezi likasitishwa ghafla, kwa sisi tunaofuatilia mambo nchi ilitaka kusimama hii, JWTZ kuna vigogo walitikiswa huko, sasa unadhani ni rahisi kumng'oa mtu mwenye siri za kijeshi na kiserikali kweli.

Tusijidanganye kuna baadhi ya nyadhifa kama viongozi walitumia vyeti feki kukaa hapo walipo hakuna ujanja wa kuwaondoa kiurahisi. Cha kufanya tusiruhusu hilo lijirudie tena.
 
na haya mambo ya kuomba kazi sijui zoom sijui wapi unaweza kuta mtu alichukua cheti chako akaombea kazi na kupata bila wewe kujua...
 
Wakimariza Idara Hizo Nawaelekeza Maeneo Mengine Waje Wakague Idara Hz, 1.TPA. 2.BOT 3.TRA 4.TANROAD 5.WIZARA YA FEDHA.6.WIZARA YA MIUNDOMBINU. Katika Ukaguzi Wao MADEREVA WA MAGARI WA IDARA HIZO WENGI HAWANA VYETI VYA FORM 4 BALI WAMETUMIA VYA NDUGU NA WAMEAJIRIWA KWA VIMEMO.MASEKRETARI WA IDARA HIZO WAWACHUNGUZE WATAGUNDUA NUSU YAO NI VYETI AMA Ni Feki Au Ni Vya Ndugu Zao.Na Wameajiriwa Kwa Vimemo.Maeneo Mengine NITAENDELEA KUWASAIDIA KWA KUWATAJIA MAENEO YALIYOKITHIRI KWA UTUMIAJI WA VYETI BANDIA.KWA SASA Wafanyie Kwanza Hayo Maeneo Kisha Watoe Mrejesho.
 
Elimu, ujuzi, maarifa na weledi vipo kichwani mwa mhusika, Vyeti makaratasi tu! Utamtambua mtu mwenye vyeti bandia kwa kuchunguza uwezo wa kichwa chake!
 
Kwani kuna ulazima wa msako wakati idara zinazofahamika kwa kufoji vyeti zinafahamika hata na mtoto aliyezaliwa leo......
Mkuu ufanyaji kazi wa NECTA kulingana na Sheria ya Bunge No. 21 ya 1973 iliyotumika kuianzisha ni tofauti na Polisi au PCCB.

Kazi kuu ya NECTA ni Kuendesha Mitihani na kutoa Vyeti stahiki kwa kila Ngazi husika ya Elimu. Na ndio maana jana Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa NECTA alichosema ni mafanikio yao waliyoyapata katika KUDHIBITI NA KUONDOA TATIZO LA UDANGANYIFU KATIKA MITIHANI YA KITAIFA.

NECTA kulaumiwa kwa kutokudhibiti vyeti feki mitaani bila kupewa ushirikiano na vyombo vya dola itakuwa ni uonevu. Na ushirikiano huo unakuwa mgumu kwa sababu vyombo hivyo hivyo vinavyotakiwa kutoa ushirikiano ndani yake watu wamekalia viti vya kuzunguka kimagumashi.
 
Wakawaulize polisi, magereza na jeshi walivyotaka kuhakiki vyeti ni nini kilitokea na hilo zoezi liliishia wapi!
 

Yeye mwenyewe huyo kwenye picha vya kwake vikoje?! Cheti bandia kinaendana na mfumo mbovu wa elimu. Huu ni utafiti mzuri kuangalia je wenye vyeti bandia wana better performance kazini kuliko wenye vyeti sahihi!!
 
Ingekuwa vyema sana ukafika ofisi za NECTA na kutoa taarifa hizo ili wao NECTA washirikiane na mamlaka husika katika kuwabaini wezi hao. NECTA haifanyi kazi kwa kuvamia, ila mwajiri mwenyewe ndiye anapaswa kuwasilisha NECTA vyeti vyote vya waajiriwa wake kwa uhakiki.

Na ikibainika udanganyifu ni jukumu la mamlaka husika kuchukua hatua kwa aliyehusika na udanganyifu.
 
Jamani tuache masihala hivi wakikagua kweli na hutu tu vyeti twangu feki ka form 4 na form 6 hivi sinitapumulia mashine...anyway naaamin kuna wenzangu wenye influence watakwamisha zoezi.......Ila ngoja tusubiri.
 
Hahahahahaaaa......yaani mwizi anapewa kazi ya kumsaka mwizi.....hahahaaaaaaaaaaaa
 

Wakianzia huko Nadhani nchi itatikisika na itabidi zoezi liwekwe kiporo!
 
Na ualimu hasa MEM imeingiza wengi sana. au watangaze bingo waone watakavyopata watu wengi
 
Stop!!! Necta. Mnapaswa kudhibiti sasa wanao ingia na siyo waliomo! Msituletee balaa zenu mlikuwa wapi zamani? Nasema hizo ni fujo! Mshika bunduki umwambie una cheti feki, mtafika!?
 
Stop!!! Necta. Mnapaswa kudhibiti sasa wanao ingia na siyo waliomo! Msituletee balaa zenu mlikuwa wapi zamani? Nasema hizo ni fujo! Mshika bunduki umwambie una cheti feki, mtafika!?

Unafahamu majukumu ya NECTA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…