NEC yabariki kampeni za CHADEMA Maswa kusitishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC yabariki kampeni za CHADEMA Maswa kusitishwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mafuchila, Oct 30, 2010.

 1. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2010
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  NEC yabariki kampeni za Chadema Maswa kusitishwa

  Na Joseph Mwendapole
  30th October 2010


  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imebariki uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Uchaguzi ya Jimbo la Maswa Magharibi mkoani Shinyanga ya kusimamisha kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Mkurugenzi wa Nec, Rajab Kiravu, alisema jana kuwa NEC ilipitia kwa makini uamuzi uliochukuliwa na kamati hiyo na imeridhika kuwa hatua iliyochukuliwa ni sahihi.

  "Kamati ya Maadili ya kitaifa imeridhika na hatua iliyochukuliwa baada ya kupitia kwa makini mwenendo wa shauri lile hivyo NEC imekubali chama hicho kisifanye kampeni zozote ndani ya jimbo lile," alisema.

  Vile vile, Kiravu alisema Nec imepokea rasmi malalamiko ya CCM dhidi ya Chadema kutokana na mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Temeke, Dickson Amos, kumkashifu mgombea wa urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, wakati wa mkutano wa kampeni Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.

  Kiravu alisema ingawa siku zimekwisha NEC itajadili malalamiko hayo ya CCM kwa kina na kisha itatoa majibu kwa chama hicho.

  Akizungumzia matokeo ya urais, Kiravu alisema yatakuwa yakitangazwa kwa umma kadri yatakavyokuwa yakiletwa kutoka majimboni na baada ya majimbo yote kuwasilisha matokeo yatajumlishwa na kutangazwa.

  CHANZO:
  NIPASHE
   
 2. c

  chanai JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna umakini wowote hapo. NEC si wale wale. unategemea nini zaidi?
   
 3. T

  The King JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila dhuluma ina mwisho wake.
   
 4. minda

  minda JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  well, mwisho wa kampeni ni leo, it makes no difference!!!
  muamuzi wa mwisho ni mwananchi wa jimbo hilo.
   
 5. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2010
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sijui Hawa NEC, yaani Lewis Makame na Rajabu Kiravu, wataaminikaje na wananchi kwamba watatendea haki kura zetu tutakazowapia Slaa. wagombea Ubunge wa Chadema na madiwani wao. Obviously biased against Chadema.
   
 6. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hata wafanyeje, Shibuda atashinda tu!!!
   
 7. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,788
  Likes Received: 6,293
  Trophy Points: 280
  Hebu badilisha title ya Thread ieleweke ni MASWA pekee. Please MODS do the needful. Heading ya post hii inapotosha
   
Loading...