Elections 2010 NEC wekeni mambo hadharani!

Ilumine

Senior Member
Dec 27, 2008
196
4
Nionavyo mimi, ingewezekana kabisa NEC watuwekee link kwenye mtandao wao ili tuweze kuona waziwazi:
1 Majimbo yote ya Uchaguzi katika mikoa yetu,
2. vituo vyote vya kupigia kura vilivyo katika jimbo Fulani la uchaguzi,
3, na kisha tuweze kubofya KITUO, ili orodha ya wapigakura na ID zao zionekane.

Kwa uelewa wangu mdogo wa mambo haya ya IT hii ni kazi ndogo sana kwa sababu Baraza la Mitihani wamekuwa wakiweka hadharani majina yote ya wanafunzi kwa utaratibu mzuri na wa wazi, ambapo, tunaweza kubofya-bofya tukaona kila kitu.

Wakuu hili mnalionaje? Tungeweza kupunguza ‘doubts' ambazo zinaendelea kujitokeza.
Nawasilisha!
 
Back
Top Bottom